TBC 1 ni kweli sikio la kufa halisikii dawa?

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Hii TBC 1 kweli imeamua kupuuzia maoni ya watazamaji wake, yaani TBC1 ikishafika saa 10 usiku hakuna kitu zaidi ya mitaarabu tu; hivi hii tabia itakwisha lini? Hamuwezi kutuwekea hata movie tuburudishe akili? Sasa taarabu saa 10 usiku kiukweli haileti afya.

TBC1 enzi za Tido burudani za ku mwaga kiasi chake alijitahidi sana mzee wa watu kuifanya TBC inahotazamwa kulikuwa na maigizo kama jumba la dhahabu, yale maigizo ya yule jamaa Dude Mwizi, tamthilia kama La revancha ili kuwa safii ila TBC 1 hii ya leo OVYO SANAAAA, yaani weekend hawana content kabisaaaaa.

KWA TAARIFA YENU HII MITAARABU MNAYOWEKA INAKERA MNOOO.

NB: Hiki ni kilio cha walio wengi.
 
Hiyo channel niliangalia mara ya mwisho kwenye world cup nadhani hadi kombe lijalo tena ndio ntafungulia
 
la revancha ilikuwa moto wa kuotea mbali hata hizi za azam tv ni mashudu tu.
 
Back
Top Bottom