nyumbamungu
JF-Expert Member
- Mar 3, 2017
- 997
- 828
Kinachonisikitisha zaidi ukiwa unaangalia matangazo Mubashara kupitia televisheni ya taifa muonekano wa picha hauna mvuto, tofauti na Azam tv, ITV, Star tv na Clouds tv.
Huwa najiuliza sana tatizo ni mitambo ya kurushia matangazo au Kamera, kama itakuwa Kamera kwanini wasinunue? naambiwa Lens zenye uwezo gharama yake inaanzia 30,000,000.
Tena wanasema hizo hata wanaopiga picha binafsi kwenye shughuli za harusi wanamiliki.
Kitu kingine ninachojiuliza! lile gari la Matangazo ya nje mbona ni mara chache sana huwa linatumika? tena pamoja na kutumika kwake matangazo yake huwa yanakatika au sauti inakosekana, Nakumbuka Mh Rais alipofanya ziara mkoa wa Pwani aliwaagiza TBC 1 warushe matangazo kila atakapokuwa anahutubia mkutano wa hadhara, walirusha matangazo lkn kidogo yalikatika.
Kupitia kampeni ya Uzalendo inayoendelea ingekuwa vizuri wao kama Televisheni ya Taifa wahamasishe kwakufanya matangazo Mubashara maeneo mbalimbali ya nchi (hadi mikoani), sio muda wote wanaendesha vipindi vya kuwa Mzalendo, Tunatekeleza na Tanzania Mpya, ndani ya Studio tu, ikiwezekana wawezeshwe waende mikoani .
Wiki iliyopita nilimuona Mkurugenzi wa TBC alipokuwa kwenye Maonesho ya Sabasaba, akipokea maoni na kujibu maswali ya watazamaji na wasikilizaji wa TBC kuhusu uboreshaji wa vipindi upande wa Redio na Televisheni, hongera kwa hilo lakini tunaomba uyafanyie kazi kwani ulisema yapo yanayojibika na mengine yanahitaji utekelezaji tu.
Mwisho: Hili kama utakuwa na bajeti tunaomba uandae kampeni ya wazi au mjadala kwa Watazamaji, Wasikilizaji na Wadau mbalimbali wanapenda nini toka Televisheni na Redio yao halafu peleka kunakohusika subiri maamuzi yao.
Pia peleka Dokezo kwa Wakuu waunde Tume kupitia Utendaji wa Star Media ikiwezekana hata mkataba wao uangaliwe upya kama kuna manufaa au hakuna kw aTaifa, Je TBC ikiwezeshwa itashindwa kufanya wanavyofanya wao ili iweze kujitegemea? Star Media ibaki kuuza Ving'amuzi tu, na kiundwe Chombo kitakacho simamia Chaneli.