TAZARA wanaweza kufanya safari ya Dar - Mbeya kwa masaa matatu tu, suala ni kuwa na mikakati mikubwa ya muda mrefu

Tatizo sio speed tu bali ni huduma bora na dhamira ya kweli mbali na siasa.

Kama huduma ingeimarishwa na kuwa bora watu wanasafiri tu kwa treni.
Mfano:pakiwa na mabehewa masafi ya first class na second yenye huduma bora za chakula ,vyoo na malazi kwa nini watu wasipande kwa ajili ya utalii pia.
Lakini huduma ni mbovu nani atahangaika kupoteza muda

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni point niisema kuhusu SGR, kwamba SGR peke yake sio suluhisho, inaweza kuja kuwa white elephant
 
hiyo reli ina kona nyingi sana na milima ya kutosha pamoja na mahandaki zaidi ya 18 ngumu kutumia saa 3 kutoka Dar kwenda Mbeya. Pia station moja kwenda nyingi ni mwendo wa dakika 20 - 30 - 45 si rahisi sana kwa muda huo uliotoa kufika mbeya
Achana na masaa matatu, hatujazoea mwendo wa namna hiyo, hata masaa nane yatatosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri lakini nikuambie utengenezaji wa hizo reli unategemea na treni mnataka likimbie kwa spidi ipi, mfano hiyo reli wanayoimba kila siku standard gauge speed ya treni inatakiwa isizidi 160km/h, likivuka 200km/h lazima lianguke.

Sasa hiyo unayowaza wewe ya treni kwenda 250km/h ni level nyingine cost yake ni kubwa, ipo na reli inayoruhusu treni likimbie 600km/h maximum hiyo ni ghari zaidi matengenezo yake. Lakini yote kwa yote hakuna lishindikanalo kama pesa ipo.
 
Hata watu binafsi wenye mitaji mikubwa wanaweza kupewa kwa utaratibu maalum,,
Kwa mfano reli ya kati unakuta zaidi ya kontena 20 zina chata ya azam,,,tena kila treni ya mizigo behewa ni azam,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiyo reli ina kona nyingi sana na milima ya kutosha pamoja na mahandaki zaidi ya 18 ngumu kutumia saa 3 kutoka Dar kwenda Mbeya. Pia station moja kwenda nyingi ni mwendo wa dakika 20 - 30 - 45 si rahisi sana kwa muda huo uliotoa kufika mbeya
Yeye ametumia hesabu za km/h kwa speed ya hizo treni wewe unakuja na ubishi wako wa kienyeji nani kakwambia kwamba kona zilizopo zina ongeza idadi ya umbali halisi wa dar mbeya ? Jamani msiwe mnaleta ubisahi wa vijiweni hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawashangaa sana watu wa TAZARA. Wanakubali kufiwa na shirika mikononi na siku zote kuwa na mikakati midogo sana ya kuifufua kampuni (mediocre strategies). TAZARA wanahitaji kufikiria kikubwa - think big - ikiwa wanataka kuendelea kuwapo.

Kwa mfano, umbali wa reli ya TAZARA toka Dar hadi Mbeya ni km 860. Treni za kasi za kampuni ya DB ya Germany zinazosafiri kati ya nchi ya Germany, Ufaransa, Belgium na Uswisi, spidi yake ya wastani ni km 250/hr, lakini zinaweza kwenda hadi spidi ya 300km/hr.

Kwa hiyo ikiwa reli ya TAZARA ambayo ni "heavy gauge" ikiboreshwa kutumia umeme na kuondoa kona kali, TAZARA watakuwa na uwezo wa kufanya safari kati ya Dar es Salaam na Mbeya kwa muda wa saa 3, kutia ndani na kusimama vituo vikubwa vya Ifakara na Makambako.

Gharama ya maboresho hayo ya TAZARA kufikia kiwango hicho hayawezi kufikia gharama ya kujenga SGR kati ya Dar na Morogoro. Yatafanya soko la TAZARA likue sana. Na nikweli safari za ndege Dar - Mbeya zitakosa soko, lakini si ajabu. Pia TAZARA wakifanya hivyo itapunguza sana utitiri wa mabasi njia ya Dar-es-Salaam hadi Mbeya. Watu wa Dar - Iringa au Dar- Songea wanaweza kuwa wanapanda mabasi toka Makambako.

Inawezekana, suala ni mipango tu, labda ubia na wachina kwa mradi kama huu ili kuinusuru TAZARA ambayo bila mkakati mzito itakufa. Think big TAZARA, acheni mipango ya maboresho ya kipwagu na pwaguzi, haitawapeleka popote. TAZARA wanaweza pia kufikiria kuendeleza reli hii kwenda Kyela na Malawi toka pale Vyawa (Mbozi) - ukifikiria suala la kupatikana mafuta ndani ya ziwa Nyasa.

View attachment 1043252
Kuna watu mna mawazo mazuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KUna tatizo gani mkuu, milima? Niliona zamani walikuwa wanaunga vichwa viwili viwili. Ila waliponunua vichwa vya Germany waliambiwa sio lazima, vile milima vinapanda kama kumsukuma mlevi
Kufunga vichwa viwili inategemeana nguvu ya hicho kichwa. Huwa vinazidiana mkuu.
 
Mawazo yako ni mazuri ila kwa jiografia ya reli ya TAZARA ni ngumu sana kufikia hiyo kasi unayotaka.Reli imepita kwenye bonde la ufa kwenye milima na kona nyingi sana hasa kutoka Ifakara kwenda Makambako.Halafu mkataba wa uendeshaji umekaaa kisiasa maana mkurugenzi eti lazzima atoke Zambia hilo hata JPM alizungumza wakati raisi Lungu alipokuja.Kwamba mkataba wauendeshaji upitiwe upya ili apatikane mkurugenzi toka sehemu yeyote.
Hata kwenye kuchangia uendeshaji zambia hawatoi hela kwa wakati kama Tz mpaka waziri Kamwele alilalamika.
 
Nawashangaa sana watu wa TAZARA. Wanakubali kufiwa na shirika mikononi na siku zote kuwa na mikakati midogo sana ya kuifufua kampuni (mediocre strategies). TAZARA wanahitaji kufikiria kikubwa - think big - ikiwa wanataka kuendelea kuwapo.

Kwa mfano, umbali wa reli ya TAZARA toka Dar hadi Mbeya ni km 860. Treni za kasi za kampuni ya DB ya Germany zinazosafiri kati ya nchi ya Germany, Ufaransa, Belgium na Uswisi, spidi yake ya wastani ni km 250/hr, lakini zinaweza kwenda hadi spidi ya 300km/hr.

Kwa hiyo ikiwa reli ya TAZARA ambayo ni "heavy gauge" ikiboreshwa kutumia umeme na kuondoa kona kali, TAZARA watakuwa na uwezo wa kufanya safari kati ya Dar es Salaam na Mbeya kwa muda wa saa 3, kutia ndani na kusimama vituo vikubwa vya Ifakara na Makambako.

Gharama ya maboresho hayo ya TAZARA kufikia kiwango hicho hayawezi kufikia gharama ya kujenga SGR kati ya Dar na Morogoro. Yatafanya soko la TAZARA likue sana. Na nikweli safari za ndege Dar - Mbeya zitakosa soko, lakini si ajabu. Pia TAZARA wakifanya hivyo itapunguza sana utitiri wa mabasi njia ya Dar-es-Salaam hadi Mbeya. Watu wa Dar - Iringa au Dar- Songea wanaweza kuwa wanapanda mabasi toka Makambako.

Inawezekana, suala ni mipango tu, labda ubia na wachina kwa mradi kama huu ili kuinusuru TAZARA ambayo bila mkakati mzito itakufa. Think big TAZARA, acheni mipango ya maboresho ya kipwagu na pwaguzi, haitawapeleka popote. TAZARA wanaweza pia kufikiria kuendeleza reli hii kwenda Kyela na Malawi toka pale Vyawa (Mbozi) - ukifikiria suala la kupatikana mafuta ndani ya ziwa Nyasa.

View attachment 1043252
Ni wazo zuri sana hilo, hususani sisi tunaotumia route hiyo na muda mwingi tupo kwenye mabasi tu...sema itabidi waondoe obstacles nyingi barabarani kwakweli
 
hiyo reli ina kona nyingi sana na milima ya kutosha pamoja na mahandaki zaidi ya 18 ngumu kutumia saa 3 kutoka Dar kwenda Mbeya. Pia station moja kwenda nyingi ni mwendo wa dakika 20 - 30 - 45 si rahisi sana kwa muda huo uliotoa kufika mbeya
Jamaa ameongelea kona na vituo vikipunguzwa unaonekana husomi unaongea ongea tu..
Read carefuly, understand then coment accordingly.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hiyo reli ina kona nyingi sana na milima ya kutosha pamoja na mahandaki zaidi ya 18 ngumu kutumia saa 3 kutoka Dar kwenda Mbeya. Pia station moja kwenda nyingi ni mwendo wa dakika 20 - 30 - 45 si rahisi sana kwa muda huo uliotoa kufika mbeya
Wazee wa negative kazini
 
Tatizo siasa zipo kila sehemu ndani ya serikali,kwenye mabasi wamejaa wanasiasa kwa umiliki na wanasiasa wengi ndo wabunge hawatapenda hilo wazo lifanikiwe
 
hiyo reli ina kona nyingi sana na milima ya kutosha pamoja na mahandaki zaidi ya 18 ngumu kutumia saa 3 kutoka Dar kwenda Mbeya. Pia station moja kwenda nyingi ni mwendo wa dakika 20 - 30 - 45 si rahisi sana kwa muda huo uliotoa kufika mbeya
...Angalau kwa siku moja basi! Ikiondoka Dar saa Nne asubuhi saa Kumi jioni iko Mbeya! Hapo vipi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mainjinia si ndio walifanya hiyo kazi ya ujenzi mkuu?
Binafsi ninavyofahamu shida kubwa ni hali ya kijiografia ya maeneo ndio changamoto kubwa sana, nina imani hata wao walipenda iwe rahisi lakini ndio hivyo.
Jibu la swali lako lipo kwenye mradi wa SGR ya reli ya kati. Mturuki anajenga hii reli pembeni ya ile reli ya zamani ila kuna sehemu wamenyoosha kwakua speed ya train mpya ni kubwa zaidi. Reli ya zamani ilikunja kunja kukwepa changamoto za ujenzi. Kwa sasa technology ya ujenzi imekua sana ni rahisi zaidi kupita maeneo korofi bila kukwaza mwendo wa train.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom