TAZARA, TRC mmekosa nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAZARA, TRC mmekosa nini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Bujibuji, May 20, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,000
  Trophy Points: 280
  Siku za nyuma mlikuwa na nguvu haswa, lakini leo sijui mmeikosea nini serekali. Sekta ya usafiri wa reli imepewa kisogo.
  Hivi hizi ndoto za kuanzisha usafiri wa reli kwa wakazi DSM zitatimiaje bila ya uwepo wa makampuni haya mawili yenye mtandao wa reli DSM na mikoani?
  Serikali isiyafumbie macho matatizo yao, iyatatue.
   
 2. x

  xman Senior Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu labda kwa rais atakaye bahatika kuchukua kiti 2015 lakini kwa huyu jamaa ni "business as usual" sitegemei mabadiliko makubwa ata ya kati ambayo yamsingi katika hii sekta ya usafirishaji wa reli
   
 3. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Bujibuji ndugu yangu, Tz haisongi mbele kimaendeleo thats why injini zote za kutupeleka kwenye maendeleo ya kweli kama mashirika ya meli, reli, migodi ya madini na kadhalika tumeyaacha yachezewe na mbwa koko.
  Ubinafsi unaangamiza nchi.
   
 4. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwanza nikupongeze kwa kuliona hilo. Hizi ni facts: Serikali ya CCM inaishi kwa rushw kubwa inayotokana na biashara ya usafirishaji kwa njia ya barabara.

  Usafiri huu unachukua si chini ya 92% ya biashara yote ya uchukuzi, kwa kuhakikisha njia zingine za uchukuzi ikiwemo reli hazifurukuti. Mkakati ulifanikiwa wakati wafanyabiashara CCM na wafadhili wake walipojimarisha kwenye ngazi za maamuzi hasa Ikulu na Hazina.

  a. Ndio waagizaji wa mafuta na wapangaji wa bei ya mafuta nna usafirishaji kupitia kwenye mtandao wao unaoratibiwa kwa makini na ofisi za serikali hasa hazina.

  Mfano 1 kamati ya kodi kwenye biashara ya malori haitakuja kuwahi kupitisha kiwango cha kodi kinachostahili kulipwa na hawa watu Kwa sababu wanakamati watachukua burungutu zao watanyamazia.

  Mfano 2 bei ya mafuta imeshindikana kusimamiwa hata na kuwepo na mbwembwe za ewura.

  Mfano 3 mfuko wa barabara unachangiwa na mafuta yanayotumiwa na uchukuzi wa reli lakini hawapo kwenye mgao huo wanaouchangia.

  Mfano 4 hazina wanapotenga fedha za maendeleo kwa ajili ya uchukuzi 97% ya fedha zote huelekezwa kwenye barabara zingine 3% ndizo zinaelekezwa kwenye reli, anga majini. Sababu ni ile ile maofisa wa hazina binafsi kwa kuzingatia mazingira ya kimfumo ya CCM wanachukua chao kwa gharama ya kuua reli (kutoitengea fedha).

  Mfano 5 ubinafisishaji wa reli kwa wahindi 2004/05 uliambatana na Mahindra za CCM kwenye uchaguzi wa 2005 chini ya uratibu na usimamizi wa Sir Chande. Matokeo yake sisi wote ni mashahidi.

  Mfano 6 utendaji wa bandari kila mwaka unavuka uwezo lakini malengo yanakwamishwa na mrundikano bandarini kwa reli kutofanya kazi. Barabara haina uwezo kama reli kuhamisha bidhaa toka bandarini. Lakini wafanya biashara wa usafiri wa barabara wanaendeleza ukiritimba wa kuchukua mizigo kwa kuungwa mkono na wenye maamuzi serikalini kwa masilahi yao (hasa hazina na Ikulu)

  Mifano iko mingi labda tuangalie athari kwan nchi kutelekeza reli:

  1. Uendeshaji wa reli ni mzigo kwa serikali hivi sasa pamoja na uwezekano wa kujiendesha kwa faida kwa kusafirisha bidhaa nyingi kwa nchi zisizo na mlango wa bahari.

  2. Biashara ya malori itaishia kutuachia scrap wakati malori yatakapokuwa machakavu (tayari angalia kwenye service roads malori machakavu)

  3 Mipango ya nchi kufungua uchumi kando kando mwa reli imetupwa kwa maana haipo ina maana ya kukumbatia umaskini kwa eneo kubwa la nchi.

  4 Washindani kiuchumi Africa ya kusini, Kenya Msumbiji wanachekelea jinsi tulivyowasusia soko.

  5 CCM hawatatawala maisha na maamuzi yao ya kipuuzi kuhusu reli iwe kwa ujinga au makusudi yatakuwa shubiri kwa ujenzi mpya wa sekta ndogo ya uchukuzi wa reli. Kama itaingia serikali mbadala ambayo ni makini kuna watakaonyea debe hadi kifo chao kwa hujuma yao. Ni chanzo cha balaa kwa taifa

  6 Fursa ya nchi kufaidika na mchango wa reli umeahirishwa kwa kipindi kisichojulikana. Kwa sasa mchango wa sekta ya uchukuzi kwa pato la taifa ni 4% ambalo lingeweza kufikia 15% na kuwagusa kiuchumi si chini ya 40% ya watanzania kwa kufufua utendaji wa sekta ndogo ya uchukuzi wa reli.

  Chakufanya

  1 Wabunge makini washinikize marejeo ya bajeti angalau sekta nyingine za uchukuzi nje ya barabara zitengewe 40% ya pesa za maendeleo kwenye sekta ya uchukuzi kwa kipindi cha miaka mitatu tu mfululizo.

  2 Kundi la wafanyabiashara wa mafuta na malori wakiwamo Ikulu na Hazina wapigiwe mayowe kuwa hawawezi kunyonga reli kwa ufisadi kuwe na uwanja sawa wa kufanya biashara kinyume chake NGUVU YA UMMA itumike kudai haki ya kufaidika na reli.

  3 CCM imechangia kuuwa reli kwa sera zake za kifisadi vyama vingine vichukue hii agenda na viamini reli inalipa bila CCM

  Kuna wigo mpana wa sekta ndogo ya reli kuliko tunavyoielewa. Deconjestion ya bandari, kuchangia maendeleo na pato la nchi.

  UBAYA RELI KWA WATAWALA WETU SI BIASHARA WANAYOWEZA KUIFANYA. INA TASWIRA YA TAIFA TOFAUTI NA BARABARA YENYE TASWIRA YA MTU BINAFSI. Watawala wasijiamini kuwa hatujui kinachoendelea.
   
 5. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,808
  Likes Received: 524
  Trophy Points: 280
  Viongozi wetu kweli hamnazo
   
Loading...