Tazara Flyover...!

Tazara Flyover...!

Foleni inakuwa kubwa wakati magari ya Mandela Road inabidi yasubiriane na ya Nyerere Road ili kupita Tazara. Sasa kusubiriana kupita hapo Tazara hakutakuwepo tena hivyo flow ya traffic itakuwa ni nzuri. Tatizo Pekee ninaloliona ni kwamba pale Buguruni patakuwa panatia giza na Tabata Dampo pia.

Tiba
nadhani uko sahihi, ngoja nione yakitoka Buguruni kwenda Mjini au airport yatakuwa hayakwami? hivyo hivyo kutoka airport kwenda Ubungo/Mbagala yatakuwa hayakwami? tibangayuka
 
bangkok walijenga flyover all the way from City centre to Airport
Duh kumbwa kweli sisi tumejenga daraja la mita 100 ndotunaliita flyover ......badala ya kuweka nguvu zetu kwa vitu tutakavyo weza tunatafuta kiki za kisiasa tu....hizo pesa tungeziweka katika miundombinu ya usambazaji maji Dar, aibu ya jiji kuu kukosa maji safi na salama ingepungua kama sio kuisha kabisa
 
Nilitegemea angalau kwa kuanzia kitu kama hiki pale Tazara lakini .. hapa Ni Bangkok ndiyo walikuwa wanaanza baada ya magari kuwa mengi.
Swali, kweli daraja hili litapunguza msongamano Tazara?
upload_2018-7-22_7-12-54-jpeg.815435
Labda siku za baadae itajengwa nyingine ikianzia kupanda vetenary na kupita juu ya hii ya tazara na kushuka huko mbele darajani.
 
Duh kumbwa kweli sisi tumejenga daraja la mita 100 ndotunaliita flyover ......badala ya kuweka nguvu zetu kwa vitu tutakavyo weza tunatafuta kiki za kisiasa tu....hizo pesa tungeziweka katika miundombinu ya usambazaji maji Dar, aibu ya jiji kuu kukosa maji safi na salama ingepungua kama sio kuisha kabisa
Wizara ya maji na Wizara ya ujenzi kila moja ina bajeti yake. Umeambiwa miradi ya maji imesimama kwasababu ya hio flyover? Kabla ya hio flyover maji yalikuwa yanatiririka nchi nzina sio?
 
Siku Hizi Nikipita Tazara Nashangaa Askari Wameanza Tena Kuongoza Magari Wakati Ilipofunguliwa Mambo Yalikuwa Sawa
 
Back
Top Bottom