Tazara Flyover...!

Tazara Flyover...!

Mimi nangoja ianze kutumika nione suluhisho la foleni litakuwaje ndiyo ntakuja kutoa sifa au la!

Ova
Ni wazi foleni itapungua. Ila haiwezi kwisha na hamna mji mkubwa duniani usio na foleni.
 
Wewe unaamini Japan wametoa huo mkopo/msaada bila kupitia au wao kufanya upembuzi yakinifu wao? Hivi kwanini tunapenda kujifanya tuna akili kuliko hata wataalam wanaotekeleza hio miradi?
Mkuu mkopo ni biashara wa Japan watatoa tu mkopo hata ukiwapa utafiti wa uongo hawata kukutalia....ila mie naawakika daraja kama hilo hawawezi kilijenga kwao
 
Sasa nitalifaje? Wenye magari ndio mtakufa sana mtataka kukimbizana kule juu
kwahiyo wewe mwenye bicycle unaamini kuwa utabaki salama ""!!? maana kule juu " ni mwendo WA kasi kubwa ukipita kule na bicycle yako " siitakuwa waiweka roho yako " mashakani
 
Ni kazi sana kuwa kiongozi Tanzania
Ila ni rahisi kuwa mtawala Tanzania
 
Mkuu mkopo ni biashara wa Japan watatoa tu mkopo hata ukiwapa utafiti wa uongo hawata kukutalia....ila mie naawakika daraja kama hilo hawawezi kilijenga kwao
Hawawezi kulijenga kwasababu hawana uhitaji au kwanini?
 
daraja mnaita fly~over ila tumejitahaidi
Soma soma kidogo kabla hujapayuka.
Screenshot_2018-07-22-09-23-02.png
Screenshot_2018-07-22-09-23-18.png
 
Tumekuja makamanda kupinga na kuponda Kama kawaida yetu.
 
On a positive note nafikiri ni mwanzo mzuri, tunapoendelea kutekeleza miradi ya aina hii huu uwe ndiyo "benchmark" yetu. Tuangalie tulipokosea ili kuboresha miradi kama hii inayofuata. Pongezi za dhati kwa wote waliofanikisha mradi huu. This is something tangible!
 
Ushauri kwa serikali yangu pendwa sikivu na tukufu.Hili najua serikali imeshaliona.Barabara ya Magomeni hadi ubungo doube road njia mbili haijafikisha hata miaka30.Je wakati wanaanza kujenga hawakupiga hesabu mbele hadi kufikia walivobuni mwendo kasi ikawa usumbufu tena bomoa bomoa katikati?.Sisi waafrika tuna tatizo moja tu.Tukipanga kitu anayekipanga anakipanga kwa span ya miaka20 mbele hata kumi tu.Wenzetu weupe plani ikiwekwa inapigiwa hata miaka300 mbele anaye plan hataona ila ni vilembwe lembwe vyake.Je mji wa London na New york umeshawahi sikia watu wanaambiwa nyumba zao zibomolewe kupisha upanuzi wa barabara?.USHAURI KUNTU:-Bahati nzuri serikali yetu imeshaona hili tayari na imeanza mkakati kutekeleza.Mji wa Dodoma tunaoujenga tuupigie hesabu za miaka mingi mbele.Tuandae Satelite towns mapema kuanzia sasa.Kwa Dar hali kadhalika tuandae Sattelite towns jambo ambalo kiukweli silaumu serikali yetu linafanyika sasa.Tutakuwa
na miji midogo ya pembeni mfano Kigamboni city,Mlandizi city,Kibaha city,Kibiti city(hapo siweki utani),na miji mingine nchini iwe hivyo hivyo.Haina maana kila mtu atake kung'ang'ania kukaa katikati ya jiji kama nyuki wanavyolundikana kwenye sega lao na hata nyuki wakiwa wengi ndani ya mzinga wanateua malkia mwingine wanakwenda kuanzisha mzinga mwingine.Hizo sattelite towns zitakuwa na supermarkets na ila kitu mtu hataona haja ya kwenda Kariakoo kununua tu mchicha.Ushauri wa mwisho vile Dodoma toka enzi ya mwalimu kulikuwa na plan ya kuhamia huko na plan ikawa inasua sua ila kwa sasa imewezekana basi kuzunguka jiji la Dodoma pajengwe Ring roads kuzunguka jiji lote la Dodoma hizi barabara zitasaidia magari madogo kwa makubwa yote yanayokwenda mikoa inayopakana na Dodoma kutokuingia mjini kuzidisha msongamano na usumbufu.Hii itasaidia Tusipate tabu sana ya adha mbali mbali.Naomba kutoa hoja
 
Nilitegemea angalau kwa kuanzia kitu kama hiki pale Tazara lakini .. hapa Ni Bangkok ndiyo walikuwa wanaanza baada ya magari kuwa mengi.
Swali, kweli daraja hili litapunguza msongamano Tazara?
upload_2018-7-22_7-12-54-jpeg.815435
itapunguza kwa 80%,mambo makubwa yanakuja ubungo interchange ya gorofa tatu,kuingia dar itakuwa mpaka upate semina elekezi ya mishale vinginevyo utajikuta unarudi kimara kwa kukosea njia
 
Yes, kwa ufinyu wa barabara zetu you can equate it to Bangkok. Hivi magari yanayotoka Buguruni/Mbagala msongamano utapunguaje maana hiyo flyover ni along Nyrere road! Nieleweshe please
Foleni inakuwa kubwa wakati magari ya Mandela Road inabidi yasubiriane na ya Nyerere Road ili kupita Tazara. Sasa kusubiriana kupita hapo Tazara hakutakuwepo tena hivyo flow ya traffic itakuwa ni nzuri. Tatizo Pekee ninaloliona ni kwamba pale Buguruni patakuwa panatia giza na Tabata Dampo pia.

Tiba
 
Back
Top Bottom