Tazama ufalme wake umefitinika

mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,434
5,535
Neno lililomjia nabii Mogul enzi za mfalme jiwe.

Hata ifikapo mwisho wa juma Mfalme huketi na kutafakari juu ya watenda kazi wake kama ilivyo desturi yake.

Tazama hata siku ya pili yule mkuu wa watoza ushuru alipanda hadi ng'ambo ya bahari kushuhudia kama vitu vya mwanamfalme vipo na alipoviona akasimama akajipiga kifua akisema hakika iwe jua au mvua nitaviuza hivi vyote na kuutwaa ushuru wake.

Ndipo yule mkuu wa Watoza ushuru mwana wa Mpango alisemama akapaza sauti mbele ya makutano akisema hakika niko tayari kuacha enzi yangu na mamlaka yote kama ushuru wa vitu vya mwanamfalme hautakusanywa.

Ndipo habari zikaenea nchi nzima hata Mfalme na Mwanamfalme wakazisikia.
Mwanamfalme akagadhibika sana akajiuliza huyu ni nani hadi atake kumzuia mwanamfalme juu ya mali zake akaenda hadi kanda ya ziwa katika sinagogi.

Naye mkuu wa makuhani alipomuona mwanamfalme ameingia hekaluni mwake akastaajabu akasema kumetokea nini hadi mwanamfalme kuingia hekaluni tena katika kisinagogi hiki.

Ndipo kuhani akainamisha kichwa chake akamsalimu mwanamfalme akamkaribisha katika madhebahu yake.

Mwanamfalme akiwa amejazwa hasira moyoni mwake akasimama na kusema NA ALAANIWE YEYOTE ATAKAYE NUNUA MALI ZA MWANA WA MFALME NA YULE ALIYETOA AMRI YAUZWE NI HERI ANGEJIFUNGA JIWE LA KUSAGIA AKAJITUPA BAHARINI KULIKO KITAKACHOMPATA.

Makutano wote pamoja na wana wa nchi ile wakastaajabu juu ya nguvu na mamlaka alizonazo mwanamfalme wakasema huyu ndiye mpakwa mafuta wa mfalme tazama ananguvu kuliko mfalme.

Naye mfalme alikuwa katika siku za maombolezo alipoyasikia yote akatatua joho lake kisha akakuna kichwa chake akasema HAKIKA UFALME NA ENZI YANGU IMEFITINIKA
Ndipo mfalme akawaita makutano akanena nimesikia kilio chenu na cha mtoza ushuru mkuu fanyeni kama mlivyokusudia ili ushuru ulipwe.

Lakini makutano wakanung'unika na kufedheheka miyoyoni mwao wakisema HAIKUMPASA ADHABU KALI NA HUKUMU YA PAPO HAPO HUYU MWANAMFALME MBONA AMEFANYA MAKUFURU MENGI NA MACHUKIZO MBELE YETU NA HATA MBELE YA MFALME PIA?

Lakini kwakuwa haijafika siku ya sabato ambayo mfalme hutumia kuteuwa au kutumbua watendakazi wake kama ilivyo desturi yake makutano na watu wa nchi ile wanasubiri kushuhudia neno lilonenwa na manabii AUAE KWA UPANGA NAYE.
 
Back
Top Bottom