Tazama jinsi unavyohangaika kutafuta mauaji yako mwenyewe

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,564
22,129
Naomba nianze Kwa sentesi hii tizama
"LEO VIGELEGELE, KESHO ISIWE KELELE"

Laiti kama ungeyatambua maamuzi yako uliyowahi Fanya kabla ya kilio chako Leo, usingethubutu kurudia kosa.

Hebu fikiria mtu yule aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu au kumwagiwa Maji ya moto na mpenzi/ mke/Mme wake Leo, utafakari walivyokuwa na mahaba Jana yao!

Hebu fikiria laiti kama wangejuwa watu wale waliofukuzwa kwa kufoji vyeti wangekuwa miongoni mwa watu waliobeba bango la kumnadi mgombea wao fulani na hata kushiriki njama za kuiba kura jana ili kiongozi huyo ashinde awatimue kesho.

Hebu waza unavyohangaika kumlisha chakula mbwa wako ambaye atayemng'ata mwanao kesho!

Pia tafakari unavyosumbuka kumleta house girl/boy ili aje kuwa mke/mme mwenzio.

Kwa mifano hiyo michache, ndipo utatambua kwamba pasipo kutafakari vyema unaloliamua leo, huenda linaweza kuwa ndiyo sababu ya kuharibikiwa kesho yako.

"UNAHITAJI TAHADHARI KWA KILA UNALOLIAMUA LEO KWA FAIDA YA KESHO!"
 
Usichanganye madesa,sheria ni sheria na ajali ni ajali tu naona kuna vitu umevichanganya wakati haviendani.
 
Usiumize kichwa,kuna baadhi ya mambo ni lazma yatokee ili maisha yako yafikie tamat au yaendelee ktk furaha au huzun...maisha yanaongozwa na kanuni au sheria na ufaham kwamba kutoijua sheria hakuzuii maisha kuifuata sheria au kanuni.Kuna sheria ya chanzo na matokeo,hii ndio inayoleta yote uliyoyazungumza by the way ntaendelea baadae nawah job nsije tumbuliwa
 
kama ni hivo basi hatupaswi kufanya chochote wala kuamua chochote .
Si kila baya linalokujia ni wewe umesababisha mengine unasababishiwa na watu wasiokuwa makini.
 
Hapo kwenye alacho kuku umeniacha mkuu, ufafanuzi plz
Tumezoea labda kuwapa wageni(asiye wa nyumbani) yale masazo, mabaki, makapi kwa kujua tutaonekana wema, au tutasifiwa na wengine. Lakini huwa tunakosea maana huwa tunawaza kijuu juu sana, tunawaza kwa leo.

Hayo mabaki tunayowapa wageni(mbwa, panya, paka, n.k) inabidi tuwape kuku, ambao tunafuga sisi wenyewe, ambao kesho watakuwa faida kwetu, watakuwa chakula kwetu, n.k. Na hapo ndipo tuiwazapo vema leo, kwa ajili ya kesho.

Zaidi, kuku anaweza kuwa mkeo, watoto wako, jamii yako, nchi yako, watu wema, wenye maono ya mafanikio, n.k.
Mgeni aweza kuwa, fisadi, dikteta, mlafi, mwivi, nyoka, asiye mwema, n.k.

Naamini hapo kidogo umeielewa nia ya moyo wangu.

Na hakika, "laiti wangelijua alacho kuku, wasingelimpa mgeni."
 
Laiti kama wangejua kuwa atakuwa mgombea wao Wa uraisi, wasingelimuita fisadi mkuu jana
 
"Angalia ulivyopata kilema cha maisha kwa kuvunjika mguu,kwasababu ya gari lako mwenyewe tena ulilipata kwa mkopo,laiti ungejua hata mkopo wenyewe ungeupotezea" Sasa tafakari kama kila kitu ukifikirie kwa njia hii je kuna sababu gani ya kuishi ........Vitu vingine ni lazima vifanyike ili iwe sababu ya kifo chako,maana hata kukaa ndani nayo ni kutafuta kifo chako.
 
Naomba nianze Kwa sentesi hii tizama
"LEO VIGELEGELE, KESHO ISIWE KELELE"

Laiti kama ungeyatambua maamuzi yako uliyowahi Fanya kabla ya kilio chako Leo, usingethubutu kurudia kosa.

Hebu fikiria mtu yule aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu au kumwagiwa Maji ya moto na mpenzi/ mke/Mme wake Leo, utafakari walivyokuwa na mahaba Jana yao!

Hebu fikiria laiti kama wangejuwa watu wale waliofukuzwa kwa kufoji vyeti wangekuwa miongoni mwa watu waliobeba bango la kumnadi mgombea wao fulani na hata kushiriki njama za kuiba kura jana ili kiongozi huyo ashinde awatimue kesho.

Hebu waza unavyohangaika kumlisha chakula mbwa wako ambaye atayemng'ata mwanao kesho!

Pia tafakari unavyosumbuka kumleta house girl/boy ili aje kuwa mke/mme mwenzio.

Kwa mifano hiyo michache, ndipo utatambua kwamba pasipo kutafakari vyema unaloliamua leo, huenda linaweza kuwa ndiyo sababu ya kuharibikiwa kesho yako.

"UNAHITAJI TAHADHARI KWA KILA UNALOLIAMUA LEO KWA FAIDA YA KESHO!"
Mleta uzi uko sahihi kwa mtizamo wa kutoka upande mmoja kwamba tuwe makini kwa kila tunalofanya.
Ila kwa upande mwingine hatuna uwezo wa kujua linalotokea mbele hata kwa dakika moja tu. Hivyo inakuwa vigumu kujihadhari kabla ya hatari.

Ndio maana unaambiwa mwombe Mungu akutangulie kwa kila unalotaka kufanya kwa maana tunaamini yeye pekee ndiye anayeijua kesho yako. Kwa wengine wasiokuwa na imani katika Mungu, au waliopungukiwa na imani wanaenda kwa waganga kwa lengo hilo hilo la kuchungulia kabla ya kutenda.
 
Back
Top Bottom