Ulishawahi kukaa chini na kuhisi kama unasindikiza muda huku duniani?

proton pump

JF-Expert Member
Apr 30, 2017
5,363
6,903
Ni asubuhi uamkapo kunako pambazuka aa Usiku kabla ya kulala ndio mda ambao mtu ubongo unapata nafasi ya kuwaza au kutafakari unayoyafanya na utakacho kifanya kesho yake.

Kuna wakati unaweza fanya mambo yako yakagoma kabisa au yakaenda ndivyo sivyo. Kila unalojaribu linagoma au haliendi jinsi utakavyo.

Ogopa la kujilinganisha uwe umesoma au hujasoma. Unashangaa majamaa zako mliokuwa mnacheza wote utotoni mambo yao ni mazuri hadi unashangaa wao wana bahati gani. Hapa kukata tamaa panapo anzia. Huna mke au mme, watoto nyumba n.k.

Unaamka asubuhi hujui uende wapi au ufanye kazi gani, unajikuta umekaa kijiweni hadi jioni huna hili wala lile.

Unakaa na marafiki haupendwi au kutengwa basi tu damu yako haindenani na watu.

Ukicheki afya yako hauwezi kufanya kazi fulani. Mf mwili mdogo kuonewa na watu, mtu mfupi sana, mrefu sana, mnene sana, mwili ambao hauna nguvu (yaani hata ule nini, 𝐄𝐂𝐓𝐎𝐌𝐎𝐑𝐇𝐒).

Ukijiangalia kwa namna fulani unaweza ukajicheka au kuhuzunika na ukaona kana kwamba huna bahati au huwezi lolote.

kama Mungu amekupa akili timamu kaa chini fikiria endekea kuomba usikate tamaa. Pambana tu hadi mwisho.

Ulivyo leo sivyo ulivyokuwa jana. Ulikuwa unaumwa ukapona. Ulikuwa na hofu na sasa una amani.

Sikiliza 𝐦𝐞𝐝𝐢𝐭𝐚𝐭𝐢𝐨𝐧 𝐬𝐨𝐧𝐠𝐬. Usijiingize mazingira hatarishi ulevi, uzinzi, uraibu wa madawa n.k

Fanya vinavyokufurahisha, kucheza mpira n.k
 
Yani kijitu kama Grand P kinatobowa Kwa nini wewe usitobowe?
 

Attachments

  • FB_IMG_1701092175576.jpg
    FB_IMG_1701092175576.jpg
    68.2 KB · Views: 3
Back
Top Bottom