Mkiambiwa hakuna wapinzani muwe mnaeleewa,kitendo tu cha zitto kukimbilia kubandika mabango ya kampeni nikajua haendelei keshavuta 10% yake!!
Kuna mambo mengi nimejifunza kuhusu Asili baada ya kumsikiliza Huyu mwamba.
UPENDO DHANA ILIYOPEWA TASWIRA POTOFU
Na Mlinzi wa Urithi Wa Kushi.
Katika historia ya binadamu, dhana ya upendo imekuwa ikichukuliwa kama tiba ya kila kitu. Kauli kama “one love”, “mpende jirani yako” au hata “mpende adui yako” zimejengewa misingi ya dini, siasa, na hata harakati za kijamii. Lakini je, hii ni kweli ya asili? Au ni kitanzi kilichoundwa ili binadamu aishi katika ndoto za kudumu?
Albert Einstein aliwahi kusema: “Look deep into Nature, and then you will understand everything better.”
Hapa ndipo tunapopata siri kubwa: Asili inafundisha zaidi ya vitabu na mihadhara ya vyuo vikuu.
Toka Nimekuwa Muasili nimegundua kuwa Asili Haijawahi Kufundisha “Upendo Kwa Wote”
Jaribu kufikiria Kwa kuitazama Asili .
Simba na swala hawawezi kukaa kikao cha amani ili kuondoa tofauti zao. Simba huishi kwa nguvu za kula nyama , na swala kwa nguvu za kula Majani.
Na hata Samaki mdogo hawezi kuwaita binadamu kwenye meza ya maridhiano ili kumaliza tofauti zao maana tofauti zao zipo kiasili. Hata Nyuki mwenye sumu hawezi kuishi katika roho moja na kiumbe anayemharibu mzinga. Hii ni sawa na Fisadi /Au Papa hawezi kuishi na Mzalendo anaye kata mirija yake ambayo humuwezesha Kustawi.
Hii ni kwa sababu za Asili kuwa Kila kiumbe ana nishati yake. Wapo waliojaa positive energies wanaokuinua, wanaokupa matumaini, wanaoleta nuru.
Wapo wenye negative energies – wanaokunyonya nguvu, wanaokuangusha, wanaoeneza giza katika mapito yako
Pia Wapo walio na neutral energies – hawa hawana madhara makubwa, lakini pia hawana msaada mkubwa.
Asili imesimama katika mizani ya haki. Haki ya simba ni kula swala. Haki ya swala ni kula majani Haki ya binadamu ni kusoma mazingira yake na kuchagua anachotaka kukaribia au kukwepa.
Kosa kubwa hasa kwa viongozi, wasanii, na wanaharakati na hata watu wengine ni kuamini katika dhana ya “upendo kwa kila mtu”. Wameaminishwa kuwa kila mtu ni ndugu, kila mtu ni rafiki, kila mtu anastahili nafasi ya karibu. Huu ni ujinga wa kijamii uliovaa koti la busara. Ukweli ni kwamba Si lazima umpende kila mtu.Si lazima kila mtu akupende wewe.
Ukijaribu kulazimisha upendo wa jumla, mwisho utajikuta umekuwa mnyama mla nafsi yako mwenyewe.
Kanuni ya Frequencies na Vibrations iko wazi kwamba Kila roho hutetemeka katika frequency yake. Wakati mwingine unakutana na mtu kwa mara ya kwanza, na bila mazungumzo marefu unahisi mvuto au kinyongo. Hii siyo miujiza, bali ni mfumo wa asili katika Mitetemo.
Ukiwa na vibration ya juu (upendo wa kweli, amani ya ndani, maarifa ya asili), utaona wenye vibration duni wanakukimbia au wanakupinga.
Ukiwa na vibration ya chini (hofu, chuki, tamaa), utavutiwa na watu wa aina hiyo hiyo.
Ndiyo maana kujua frequency yako ni silaha ya maisha. Upendo wa Kimaumbile, Siyo Upendo wa Kijinga Kupenda ni zawadi, lakini kupenda kila mtu ni upofu.
Upendo wa kweli ni ule unaochagua na nilazima uwe na sababu za msingi. Achana na misemo ya kuiga eti love never ask why???
Mtu makini hasa mkushi ni lazima Ahoji
Ni lazima upande mbegu zako za upendo pale panapoweza kukua sio kila mahala hata kwenye Mwamba au Jangwa.
Lazima ulinde nafsi yako dhidi ya wanyonyaji wa kiroho na kihisia sambamba na haki ya asili.
Hivyo basi, usiwe kondoo anayeambiwa mpende adui yako maana utageuzwa kuwa 🐑 wa kafara
Badala yake, soma frequencies zako, tambua vibrations zako, na tembea katika njia ya haki ya kiasili.
Kwa sababu katika ulimwengu wa Asili upendo wa lazima sio upendo, ni UTUMWA.....
Ndimi Dereva Wa Vimondo