Tayari nimepata chama cha siasa

Tayari nimepata chama cha siasa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Nimepata chama cha siasa cha kujiunga nacho. Chama chenye Katiba,Kanuni na Taratibu zinazovutia kuzifuata.Chama chenye viongozi shupavu na uongozi wa kuthubutu. Chama chenye sifa ya kuwa msemaji wa mtanzania na mtetezi wao wote. Chama kinachojali uwezo,weledi na uzalendo.

Nilichukua muda mrefu kujisomea katiba za vyama mbalimbali. Kufuatilia yanayoendelea vyamani. Mikutano mbalimbali nilihudhuria. Kimsingi, nilitafiti vya kutosha. Nililenga kupata chama cha kujiunga nacho ambacho nafanana nacho. Nimekipata. Nitajiunga mapema mwezi wa nne. Na nitakitumikia kwa utii na ubunifu. Kwa kufuata taratibu zilizopo.

Ee Mwenyezi Mungu asante kwa kunionesha chama cha maisha yangu. Niongoze sasa nitimize malengo yangu kupitia chama hicho. Kwa mwelewa,ni rahisi kujua ni chama gani.Kipo kimoja tu Tanzania chenye sifa hizo. Nitaweka hapa kadi yangu nitakapojiunga rasmi.

Ni CHADEMA......

cc Lyimo, WILLY GAMBA na wengineo
 
Last edited by a moderator:
Kwa fasihi yako hii, unafaa kuwa mtunzi mzuri wa RIWAYA za kusadikika.
 
Nimepata chama cha siasa cha kujiunga nacho. Chama chenye Katiba,Kanuni na Taratibu zinazovutia kuzifuata.Chama chenye viongozi shupavu na uongozi wa kuthubutu. Chama chenye sifa ya kuwa msemaji wa mtanzania na mtetezi wao wote. Chama kinachojali uwezo,weledi na uzalendo.

Nilichukua muda mrefu kujisomea katiba za vyama mbalimbali. Kufuatilia yanayoendelea vyamani. Mikutano mbalimbali nilihudhuria. Kimsingi, nilitafiti vya kutosha. Nililenga kupata chama cha kujiunga nacho ambacho nafanana nacho. Nimekipata. Nitajiunga mapema mwezi wa nne. Na nitakitumikia kwa utii na ubunifu. Kwa kufuata taratibu zilizopo.

Ee Mwenyezi Mungu asante kwa kunionesha chama cha maisha yangu. Niongoze sasa nitimize malengo yangu kupitia chama hicho. Kwa mwelewa,ni rahisi kujua ni chama gani.Kipo kimoja tu Tanzania chenye sifa hizo. Nitaweka hapa kadi yangu nitakapojiunga rasmi.
Ama kweli we ni mwana siasa, kutaja tu chama mpaka uimbe taarabu!? kazi unayo!
 
...jiunge na makamanda...hakuna chama makini kama chadema TZ,NJOO wasubiri nini?
 
Alliance for Cowards and Traitors.....ndio kitakuwa tayari April..........
 
Ama kweli we ni mwana siasa, kutaja tu chama mpaka uimbe taarabu!? kazi unayo!

hahahahah, nimecheka sana, huyu bwn kwa haraka haraka ni muoga sana, sina shaka atakuwa ni gamba ila anasoma alama za nyakati upepo uko vipi, kuwa kamanda siyo lelemama, unatakiwa jasiri kama simba
 
Ungenijua usingesema hivyo Mkuu
 
hahahahah, nimecheka sana, huyu bwn kwa haraka haraka ni muoga sana, sina shaka atakuwa ni gamba ila anasoma alama za nyakati upepo uko vipi, kuwa kamanda siyo lelemama, unatakiwa jasiri kama simba
si unajua sasa kuna wapiga propaganda mitandaoni kibao, dizaini ya huyu jamaa, kama kutangaza kujiunga na chama unachukua wiki nzima, kuwavua gamba mfisadi si utachukua miaka elfu moja...naililia sana hii nchi, nanaione huruma jinsi ilivyo na watu wenye akili fui kiasi hiki, hivi huu kweli ni wakati wa kuchisifia umechagua chama kwa mbwem,bwe za kike!
 
Na wenzako walisema hivyo hivyo walivyoiunga lakini sasa wanasema opposite!

Wewe jiunge tu hizo ngonjera nyingine achana nazo.

Tambwe Hizza alisema akihama CUF atamzini mama yake! Unajua alipo leo?
 
NJO CHADEMA TUKUMBOE NCH KW WAKUBURU WEUSI CCM.MIAKA 50 WATOTO DARASAN WANAKA CHNI.NO MAJI POOR KILIMO POOR LIFE AND etc
 
Nimepata chama cha siasa cha kujiunga nacho. Chama chenye Katiba,Kanuni na Taratibu zinazovutia kuzifuata.Chama chenye viongozi shupavu na uongozi wa kuthubutu. Chama chenye sifa ya kuwa msemaji wa mtanzania na mtetezi wao wote. Chama kinachojali uwezo,weledi na uzalendo.

Nilichukua muda mrefu kujisomea katiba za vyama mbalimbali. Kufuatilia yanayoendelea vyamani. Mikutano mbalimbali nilihudhuria. Kimsingi, nilitafiti vya kutosha. Nililenga kupata chama cha kujiunga nacho ambacho nafanana nacho. Nimekipata. Nitajiunga mapema mwezi wa nne. Na nitakitumikia kwa utii na ubunifu. Kwa kufuata taratibu zilizopo.

Ee Mwenyezi Mungu asante kwa kunionesha chama cha maisha yangu. Niongoze sasa nitimize malengo yangu kupitia chama hicho. Kwa mwelewa,ni rahisi kujua ni chama gani.Kipo kimoja tu Tanzania chenye sifa hizo. Nitaweka hapa kadi yangu nitakapojiunga rasmi.

chama cha CHAUSTA
 
Na wenzako walisema hivyo hivyo walivyoiunga lakini sasa wanasema opposite!

Wewe jiunge tu hizo ngonjera nyingine achana nazo.

Tambwe Hizza alisema akihama CUF atamzini mama yake! Unajua alipo leo?

Na ndio maana Tambwe Hiza hasikiki tena maana laana ya kumzini mama yake iko juu yake. Kwa kusema tu na kisha kuja kurudi ccm tafsiri yake tayari amezini na mama yake na laana inakaa.
 
chama chochote ni kama koti likikubana unalitema.
hakuna chama cha siasa kwenye dunia ya tatu kinachoweza kufaa wakati wote,kama ccm ilivyotufaaa ikiwa kijana na kutokufaa wakati kilipozeeka ndivyo na vingine vitakavyokuwa.
jiunge na chama kinachotaka kuleta mpinduzi ya kimaendeleo na kupinga ufisadi.
chama ambacho kitahakikisha elimu bora kwa mtoto wa kitanzania.
 
teh.....teh....teh......teh......teh.......teh.....kwiiiiiikwiiiiiii.....kwiiiiiiikwiiiii....sasa naanza kuelewa sisi watanzania ni watu wa aina gani, yaani unaanzisha thread ili kutufahamisha kuwa mwezi wa nne utajiunga na chama ambacho ni siri yako?.....teh......teh......teh......kwaaaakwaaaa, kwaaaakwaaaa, mwe. ila angalao nimecheka kidogo maana pumba zako zimeongeza siku zangu za kuishi maana nimecheka.
 
si unajua sasa kuna wapiga propaganda mitandaoni kibao, dizaini ya huyu jamaa, kama kutangaza kujiunga na chama unachukua wiki nzima, kuwavua gamba mfisadi si utachukua miaka elfu moja...naililia sana hii nchi, nanaione huruma jinsi ilivyo na watu wenye akili fui kiasi hiki, hivi huu kweli ni wakati wa kuchisifia umechagua chama kwa mbwem,bwe za kike!

mkuu una busara sana, kwa kweli huo ndo ukweli mtupu bila chenga bila hila yoyote ile
 
Back
Top Bottom