Nimepata chama cha siasa cha kujiunga nacho. Chama chenye Katiba,Kanuni na Taratibu zinazovutia kuzifuata.Chama chenye viongozi shupavu na uongozi wa kuthubutu. Chama chenye sifa ya kuwa msemaji wa mtanzania na mtetezi wao wote. Chama kinachojali uwezo,weledi na uzalendo.
Nilichukua muda mrefu kujisomea katiba za vyama mbalimbali. Kufuatilia yanayoendelea vyamani. Mikutano mbalimbali nilihudhuria. Kimsingi, nilitafiti vya kutosha. Nililenga kupata chama cha kujiunga nacho ambacho nafanana nacho. Nimekipata. Nitajiunga mapema mwezi wa nne. Na nitakitumikia kwa utii na ubunifu. Kwa kufuata taratibu zilizopo.
Ee Mwenyezi Mungu asante kwa kunionesha chama cha maisha yangu. Niongoze sasa nitimize malengo yangu kupitia chama hicho. Kwa mwelewa,ni rahisi kujua ni chama gani.Kipo kimoja tu Tanzania chenye sifa hizo. Nitaweka hapa kadi yangu nitakapojiunga rasmi.
Ni
CHADEMA......
cc
Lyimo,
WILLY GAMBA na wengineo