Juzi juzi niliomba usafiri wa taxify toka Buzuruga mpaka City Council na kuelezwa safari yangu itagharimu wastani wa Tshs.3000. Nilipofika mwisho wa safari yangu dereva akanionyesha gharama kutoka kwenye simu yake kuwa Tshs.5,000. Nikamuomba pia anitumie huo ujumbe wa simu kama ilivyo kawaida lakini cha kushangaza mpaka leo ujumbe huo haujanifikia. Inavyooneka hawa madereva wananacheza na mfumo mzima wa taxify ili kumuibia mteja. Kwa nini msiwe kama Uber wanavyowasimamia madereva wao kwa ukaribu. Ukiwa Dar es Salaam utasafiri na Uber toka Sinza mpaka Railway Station kwa Tshs.7,000 tu hapa ujanja wa madereva wa taxify ingekuwa Tshs.15,000. Nawaomba muwe karibu sana na madereva wenu watawafanya mtoke barabarani.