Hawa Bolt (Old Taxify) ni majambazi wa mchana kweupe!

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
66,696
172,650
Juzi nimefanya trip toka mjini mpaka kitaa kutumia app yao ya Bolt. Safari ilikuwa ya approximately 12km ambapo kwa initial price ilinipa 7000-9000 nikajua ikizidi basi walau elfu 10 sio mbaya.Kilichotokea nafika jamaa ana end trip bei iliotokezea ni 16,000. Sikuelewea hasa ni kipi kimefanya ile bei iwe kubwa namna ile ila moja kwa moja naichukulia kama dhuluma tu. Ni wizii uliokithiri kwa kweli na hauvumiliki na sijui ni mimi tu ndio yamenikuta au kuna wenzangu nao wametokewa na hio situation ya overpricing!?

App ya Uber kwa umbali huo huo huwa inacharge 11000 ikizidi sana ni 12000! Very reasonable increment. Toka bei ya awali ya 9000-10000. Mwanzoni Taxify ilikuwa nzuri kwa bei nafuu ila sasa toka iitwe Bolt ni kigango cha ujambazi kwa kwenda mbele, halii hii haivumiliki watoa leseni wa hizi kampuni pigaji waziangalie upya.

Waliowahi kukutana na hii kadhia jitokezeni tupaze sauti
 
Hao madereva wanaweka location kwenye battery saving mode. Kwahiyo mwisho wa safari ile route inakuwa haipo accurate, ina estimate tu distance ambapo mara nyingi inazidi.

Ishawahi nitokea, nimetoka sehemu mpaka kwangu inaonesha gharama 9,000 ila nimefika ananionesha 24,000 na ramani haieleweki imechorekaje. Nikaichukua simu yake nikaangalia location nikakuta kaweka battery saving mode, nikampa 10,000 nikaondoka bila kumsemesha.

Mwingine wakati anaendesha mi naangalia app ya uber kuangalia jinsi inavyoenda. Nikaanza ona madudu yasiyoeleweka. Nikachukua simu yake nikaondoka battery saving mode kwenye location. Mamb9 yakarudi sawa.

Wakazie hao jamaa.
 
Pole sana hao Taxify au bolt ni wezi hao madereva ni wezi kabisa huwa lazima price iwe double. ila usiwe na shida walime email hela yako itarudi.

Jumapili wakati wa mvua kali mimi niliamua kuifuta hiyo application kwenye simu yangu.Sikai na wezi wa mchana potelea mbali kama nikikosa Uber nitatembea kwa boda boda
 
Hili limenikuta jana, natoka sehemu A kwenda B estimated price ilikuwa 4000-5000 nikaona nitamudu.... hatukukutana na foleni sehemu pekee tulosimama ni sheli na mzunguko kidogo kutafuta U-TURN ila mwisho wa trip bili inakuja 16000 nilichoka na hapo kwa mfuko nina elfu kumi tu.
Sikuwa na nia ya kufanya dhuluma ila nilimkazia yule dereva huku roho inaniuma, ilibidi akubali kupokea hiyo elfu tugawane hasara japo alilialia sana kuwa ataenda kukatwa kuwa amepokea nauli kamili mi sikuwa na namna..... cha ajabu baada ya muda receipt kwa email wakatuma kuwa nimelipa 10000 sijui itakuwa aliongea nao yeye au ana access hiyo.
My take: Hawa viumbe kuna namna wanafanya kupandisha hizo bei halafu wanasingizia eti ni system, kama dereva aliweza kuwaeleza kilichotokea hadi wakaandika risiti sawa na kiasi nilicholipa basi iko namna hata ukikomalia kulipa bei ya awali (estimated) wataweza kuelewa..... tusikubali kuibiwa kwa kuwahurumia wezi.
 
Juzi nimefanya trip toka mjini mpaka kitaa kutumia app yao ya Bolt. Safari ilikuwa ya approximately 12km ambapo kwa initial price ilinipa 7000-9000 nikajua ikizidi basi walau elfu 10 sio mbaya.Kilichotokea nafika jamaa ana end trip bei iliotokezea ni 16,000. Sikuelewea hasa ni kipi kimefanya ile bei iwe kubwa namna ile ila moja kwa moja naichukulia kama dhuluma tu. Ni wizii uliokithiri kwa kweli na hauvumiliki na sijui ni mimi tu ndio yamenikuta au kuna wenzangu nao wametokewa na hio situation ya overpricing!?

App ya Uber kwa umbali huo huo huwa inacharge 11000 ikizidi sana ni 12000! Very reasonable increment. Toka bei ya awali ya 9000-10000. Mwanzoni Taxify ilikuwa nzuri kwa bei nafuu ila sasa toka iitwe Bolt ni kigango cha ujambazi kwa kwenda mbele, halii hii haivumiliki watoa leseni wa hizi kampuni pigaji waziangalie upya.

Waliowahi kukutana na hii kadhia jitokezeni tupaze sauti
Pole sana mkuu, japo kubadilisha Uber siyo suluhisho maana madereva ni wale wale wanakuwa wamejisajili app hata 3
Kote wanapiga pesa.
 
Uaminifu ni hakuna kila mtu anawaza mbinu ya upigaji, mwanzoni mambo yalikuwa fresh tu sasa fungate imeisha.... sitakaa nipigwe tena nitaandaa “chenji kamili” ili tuone kisheria imekaaje.
 
Tatizo watu wanakosa uaminifu na kufanya hiz system kuonekana hatufai na za wizi tu, maana wanatafuta kila njia ku over price
 
Kwa ujumla hao jamaa ni vibaka wala si tatizo la madereva nitatizo la kampuni biashala imewashinda kabisa system zao mbovu nawalichokifanya wameondoa bonas zote kwa madereva nabil yote kuiludisha kwa mteja iyobei inayokuja wakat unaomba trip sio ya kweli ,mfano kwa sasa dereva akianza trip let say atembee ata mita 10 akifunga trip tayar 3000 imeenda,kibaya zaid ata madereva wenyewe wanalalamika maana unakuta kuna wateja ambao hawalip kwa cash utumia kadi matokeo yake zile pesa kampun hawawalip madereva ,yaan ni vibaka waliopitiliza sema kwa Mwanza awajapata mpinzani sku Uber wakija Mwanza wateja wote na madereva watawakimbia.
 
Juzi nimefanya trip toka mjini mpaka kitaa kutumia app yao ya Bolt. Safari ilikuwa ya approximately 12km ambapo kwa initial price ilinipa 7000-9000 nikajua ikizidi basi walau elfu 10 sio mbaya.Kilichotokea nafika jamaa ana end trip bei iliotokezea ni 16,000. Sikuelewea hasa ni kipi kimefanya ile bei iwe kubwa namna ile ila moja kwa moja naichukulia kama dhuluma tu. Ni wizii uliokithiri kwa kweli na hauvumiliki na sijui ni mimi tu ndio yamenikuta au kuna wenzangu nao wametokewa na hio situation ya overpricing!?

App ya Uber kwa umbali huo huo huwa inacharge 11000 ikizidi sana ni 12000! Very reasonable increment. Toka bei ya awali ya 9000-10000. Mwanzoni Taxify ilikuwa nzuri kwa bei nafuu ila sasa toka iitwe Bolt ni kigango cha ujambazi kwa kwenda mbele, halii hii haivumiliki watoa leseni wa hizi kampuni pigaji waziangalie upya.

Waliowahi kukutana na hii kadhia jitokezeni tupaze sauti

kwa post yako hii tayari nimeshafuta hizo app kwa simu yangu ya shemeji yako pia

mkuu nashukuru sana kwa kutuhabarisha.mimi nikisha tonywa kwamba "utapigwa".huwa najihami sana.maana tumeshapigwa sana nchi hii.

bora ujue kwamba gharama halisi ni hii kabla ya kuanza safari hata kama ni kubwa kuliko mambo ya viini macho.ndiyo yale mambo ya kuuziwa sabuni badala ya simu pale ubungo ya enzi zile
 
Mwezi wa kwanza nilitoka Ubungo hadi mtongani Kwa 7000,nadhani kipindi hicho upigji bado, kama nitapanda nacheki bei kabisa harafu nitamwambia nimeruquest bei hii, ikizidi hiyo yako
 
Daaah juzi nimefika stop over kuelekea kimara mwisho nikaona 3000
Nikarequest
Kufika kimara deni likaja 16000

Nikafuta na app yao hapo hapo

Taxify Mungu anawaona

Bora nirudie bajaji tu
 
Hao madereva wanaweka location kwenye battery saving mode. Kwahiyo mwisho wa safari ile route inakuwa haipo accurate, ina estimate tu distance ambapo mara nyingi inazidi.

Ishawahi nitokea, nimetoka sehemu mpaka kwangu inaonesha gharama 9,000 ila nimefika ananionesha 24,000 na ramani haieleweki imechorekaje. Nikaichukua simu yake nikaangalia location nikakuta kaweka battery saving mode, nikampa 10,000 nikaondoka bila kumsemesha.

Mwingine wakati anaendesha mi naangalia app ya uber kuangalia jinsi inavyoenda. Nikaanza ona madudu yasiyoeleweka. Nikachukua simu yake nikaondoka battery saving mode kwenye location. Mamb9 yakarudi sawa.

Wakazie hao jamaa.
Basi kuna Shida kwenye app, ni swala taxify ku upgrade app yap. kama dereva anaweza akafanya ujanja wa kucheze na GPS, ilitakiwa app ikatae kufanya kazi kama location imezimwa
 
Mimi nimeapa kutotumia usafiri wa taxify. Siyo Kampuni yenye weledi na wanawaonea wateja wao. Hawana muda mrefu watakuja kufunga biashara zao kama wakiendelea kuwaonea wateja wao kwa kuwalipisha gharama zisizoendana na huduma wanayotoa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom