Tatu Bora Mawaziri 2020-2025

Tatu Bora Mawaziri 2020-2025

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Mimi binafsi nimefuatilia nimeamua kuja na Tatu Bora yangu ya Mawaziri Bora kwa mwaka 2020-2025. Hawa jamaa uwa ni wafanya kazi sana na hawana makando kando linapokuja swala la kazi, na hawanaga kulamba miguu mtu.

Waziri Huseein Bashe

thumb_1374_800x420_0_0_auto.jpg


Amehudumu kama Waziri wa Kilimo tangu alipoteuliwa kama Waziri kwa mara ya Kwanza kama kumbukumbu zangu hazijakaa vibaya. Huyu kwa ufupi ni mtaalamu wa mauzo na amebobea katika nyanja hii, na ndio maana anafanya vizuri sana katika sekta ya kilimo hususani kuuza mazao nje na ndani ya nchi. Moja ya tukio nilalolikumbuka ni namna alivyowatunishia Wamalawi na Waafrika Kusini baada ya kukataa mazao yanayotoka Tanzania, kilichofuata ni alifungia mazao ya Wamalawi na Waafrika Kusini yasiingie Nchini. Wasahili wanasema Dawa ya moto ni moto, ukiachilia mbali kuwa na msimamo mikali, huyu mwamba anaonekana ni wazi kazi hii ya uwaziri wa kilimo anaiweza vizuri na hii ni kutokana na takwimu na taarifa anazozitoa wakati anatatua mambo ya wizara yake, anazungumza kama mtu ambaye anajua nini anafanya. Na Wizara ya Kilimo haijawai kuyumbishwa kizembe tangu huyu mwamba aingie labda myumbe nyie wakulima.

Waziri Jumaa Awesu

bio_1607688996-aweso.jpg


Amehudumu kama Waziri wa maji tangu 2017 mpaka hivi leo 2025 kwa mujibu wa taarifa za kwenye website ya Bunge. Ni zaidi ya miaka 7 ameketi kwenye wizara moja, huyu Mwamba mwenye wake wawili amethibitisha kweli ni mkali wa hii wizara. Mkali huyu ambaye ni Mkemia kitaaluma mara nyingi utamkuta anafika Site endapo kuna changamoto na mara nyingine utamkuta anaingia mpaka huko ndani ndani au mitaani endapo kuna shida inayohitaji maamuzi ya haraka. Huyu mwamba kawapelekea moto sana wachina waliojaribu kudhoofisha miradi ya maji. Jamaa uwa ana respond haraka kama kuna changamoto ya maji katika eneo fulani, na kwa namna moja au nyingine maji yamefanikiwa kufika mitaa au vijiji ambavyo uenda umeme mpaka leo ni historia.

Dorothy Gwajima

d3af519f7cac14fbd8eaab19f7d60130.jpeg


Huyu mama ni kati ya mawaziri ambao ni wacheshi na mara nyingi anapenda kujichanganya na wananchi hususani mitandaoni hili kujua namna gani atawasaidia wananchi wake. Huyu mama amehudumu kama Naibu katibu mkuu Tamisemi anayeshughulikia mambo ya Afya. Mama huyu badae aliteuliwa na Magufuli kuwa waziri wa Afya nchini, na badae Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na wenye ulemavu ilipogawanyika, akateuliwa na Rais Samia kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamiii, Jinsia, Wazee na wenye ulemavu ambapo anahudumu mpaka leo... kitaaluma huyu mama ni Daktari na amewahi kuwa Maganga Mkuu Hospital ya Bagamoyo, akawa Mganga Mkuu wa Wilaya Iramba, badae akawa mganga mkuu wa mkoa wa singida na hapo ndipo akaanza kuwa kwenye vitengo na kamati za wizara mbalimbali ikiwemo ya Tamisemi na wizara ya afya mpaka kuwa Waziri kamili. Dorothy Gwajima anafahamika kwa ucheshi wake wa Kujibu maoni mitandaoni, pia amekuwa akichukua hatua mara moja endapo anaona kuna uvunjifu wa sheria nchini hususani zinazohusu wizara yake. Mfano yule binti wa Chuo kimoja Dar es Salaam ambaye alizalilishwa kwa kupigwa na kuvuliwa nguo baada ya kutembea na mwijaku, Waziri aliamuru polisi wawakamate wahusika wote na kuchukuliwa hatua. Pia yapo mambo mengi ikiwemo video chafu huko TikTok na mitandaoni, sakata la ushoga. Amekuwa mstari wa mbele tena alichukua hatua kwenye public kabisa.


Hitimisho: Uenda kuna wizara nyingi ambao mawaziri wake wanafanya kazi nzuri, ila hii ndio tatu bora yangu ya Mawaziri Bora kwa mwaka 2020-2025. Wizara nyingine kama Wizara ya mambo ya ndani kila siku Waziri wake haonekani kuwa msaada wa wananchi zaidi ya kutaka wananchi ndio wachukuliwe hatua, hiyo wizara uwa ni ngumu kiasi kwamba kila waziri anayepelekwa kwenye hiyo wizara lazima awe na bifu na Raia... watu wanatekwa hakuna press ya wizara kuhusu utekaji, polisi wanakula rushwa hasa hawa Traffic lakini kimya... yani ni wizara ngumu sana hii, na ni kwa sababu inaenda kwenye masilahi ya watu moja kwa moja.
 
Kuna mawaziri baadhi ni wazuri lakini wizara walizowekwa zinafanya waonekane sio wazuri kabisa, mchengerwa, bashungwa,
 
Kwa namba 1 na 2 nakupa 100 kwa 100. Let them keep it up. Kwa kweli wamezitendea haki Wizara zao. But kwa upande wangu namba 3 nimgempa Dotto wa kwa Biteko. Alipokuwa Madini alifanya kazi kubwa sana. Hata Nishati tunaona misimamo na utendaji wake, ahasa pale alipowambia watendaji wa TANESCO kwamba watanzania tunachotaka ni umeme wa uhakika na siyo michakato.

to me:
1. Bashe
2. Aweso
3. Dotto
 
Kuna mawaziri baadhi ni wazuri lakini wizara walizowekwa zinafanya waonekane sio wazuri kabisa, mchengerwa, bashungwa,
Mchengerwa huyu huyu aliyeuharibu uchanguzi wa Serikali za Mitaa 2024? Bashungwa pia mwondoe kabisa, hata 10 bora hawezi kuingia. Ni aliyepooza sana na hana hata kauli ya mamlaka.
 
Gwajima wakati wa COVID alitupiga viksi kwamba tujifukize. Mwamba alipovuta tu akasema kupige chanjo.
Kujifukiza kumeokoa ndugu zangu wanne na mimi nikiwemo.
Chanjo nimechanja sababu ya kuingia nchi za watu tu, lakini kama ningeweza kupata certificate ya chanjo bila kuchanja (kama hapa bongo), nisingechanja asilani.
 
Back
Top Bottom