Amani kwenu,
Wadau nimepata mwanamke ninae taka kuoa kwa maana ya mke wa pili,tatizo kwa haraka haraka alilonalo amejichora tattoo kwenye paja tattoo hiyo ina jina la mwanaume wake aliemuacha na jina lenyewe lipo kwenye paja.
Yaani ni sehemu nyeti na mimi nimefika nataka kuchukua jumla lakini kila nikifiria nakosa amani na mwenye jina lake anaweza kuwa bado ana nguvu na kuweza kutaka kuona jina lake kama bado linadumu.
Nashauri kina dada wakati wa mapenzi yenu kumbukeni kuna kuachana sasa kizazaa kama hiki cha kuolewa na majina ya watu ni hatari.
Wadau nisaidieni ushauri mimi ndio nishaoza lakini nikifikiria jina nakosa amani.