Tatizo sote twataka tupambane na tubaki tunaishi

Northern empire

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
358
459
Hakika si siri tena nchi imakuwa ngumu saana kwa vyama pinzani na wananchi kiasi ambacho dhulma zinafanywa waziwazi.. Ipo mifano mingi kama kuziuwa kwa haki ya kufanya Mikutano, haki ya kutoa maoni, haki ya kupata tume huru, watumishi kudhulumiwa stahiki zao na mengine mengi..

Kwa watu wasiojua historia za kisiasa niwaeleze kuwa ni vigum zaidi ya ngamia kupenya kwenye tundu la sindano eti matamko, na kufanya siasa za mitandaoni zitaleta matamko chanya kwenye mustalbal wa siasa zetu.
Njia iliyopo kwa sasa ni moja tuu na ndio inakwepwa na sisi watanzania pamoja na wanasiasa ambayo ni kuandamana..

Ila ushawahi kujiuliza kwanini njia hii inaogopwa na wanasiasa na watanzania? Sababu ni moja tuu TUNATAKA KUPAMBANA NA TUENDELEE KUISHI. Hii ndio Sababu kubwa.

Hakika kila atakae amua kuandamana lazima atapambana na misukosuko na wakati mwingine kuuwawa. Nchi nyingi zilizofanya harakati za kuondoa unyanyasaji na ukandamizaji wengi wao waliopambana waliuwawa na kufungwa Japo walifanikiwa kuziokoa nchi zao walionufaika ni vizazi vyao

Hata ukija Katika dini mbalimbali mafanikio ya kuendelea kwa dini hizo umetokana na baadhi ya watu kujitoa hata kuhatarisha maisha Yao na wengine kufa kabisa lakini leo tunabaki kuwasifu kwa kujitolea kwao..

Swali ambalo unapaswa ujiulize jee upo tayari kupoteza maisha yako, mali zako na familia yako ili wengine wabaki wanaishi? Jibu unalo
Hakika hakuna sehemu ambayo ukiruhusu itengenezwe itakuwa na athari kubwa kama ubongo. Na nafasi hiyo imeachiwa mapandikizi ambayo yanafanya juhudi kushughulika na bongo za wa Tanzania na hii ni hatari kwani maneno Yao yamepelekea watanzania kuishia kulakamika tuu ila maamuzi sahihi kuchukuliwa. Watanzania wengi wanataka wakienda kwenye maandamano warudi kwao salama saalimiina wawahi juisi na pikau.. Huo ni utani embu tufuatilie hata nchi zilizopitia huko..

Narudia tena kwasasa hakuna haki yeyote atakayopewa mtu ila mpaka tuzidai kwa maandamano na kukubali kuwa kuishi au kutokuishi ni mapenzi ya Mungu..
Je upo tayari kukubali kutafuta haki kwa njia ambayo itakuwa na madhara kwetuu?
 
Tatizo ni ukosefu wa elimu mwamuko (awareness) na Umasikini uliokithiri kwasababu hizo usitegemee kitu kama hicho kutokea hapa nchini.
 
Hatujafikia huko kama Taifa sioni kama kuna sababu ya msingi ya mtu kupigana KUFA ... tukifikia huko hakutakua na haja ya kuhamasisha it’s human nature to survive
 
Hatujafikia huko kama Taifa sioni kama kuna sababu ya msingi ya mtu kupigana KUFA ... tukifikia huko hakutakua na haja ya kuhamasisha it’s human nature to survive
We ndio hujafika ila wengi washafika ila wanaogopa.. Hivi Kati ya Kenya na Tanzania wapi walau Kuna uhuru? Na kwanini wao wakenya wanachukuwa maamuzi Je wao ndio washafika alafu sisi hatujafikia?
 
We ndio hujafika ila wengi washafika ila wanaogopa.. Hivi Kati ya Kenya na Tanzania wapi walau Kuna uhuru? Na kwanini wao wakenya wanachukuwa maamuzi Je wao ndio washafika alafu sisi hatujafikia?
Sema UHURU unaoutaka kwanza ilinijue upo au haupo...
 
Back
Top Bottom