Tatizo sio Katiba ama CCM, tatizo ni Watanzania wenyewe

mbalaka

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
2,241
2,622
Last week nilikua natoka mkoa, ndani ya basi nililokuwa nimepanda mbele yetu kulikuwa na mabasi mengine mawili.

Gari zilikimbia kwa muda mrefu hatimahye tukaingia stendi moja hivi ndogo tu. wahudumu wakatuambia tuna dakika 5 za kuchimba dawa katika stend hiyo. Baada kumaliza kuchimba dawa tukaanza kutoka ndani ya hiyo stend, wakati tunakariba kwenye cheni ya ushuru wa stend, gari la mbele yetu likasimamishwa na traffic, tulio kuwa gari ya nyuma mwanzo hatukujua tatizo nini ila baadae ikabainika kwamba wakati gari zinatoka na kukaribia cheni ya ushuru kuna baadhi ya abiria waliokuwa wamechelewa kupanda gari ilipokua imepaki hali iliyopeleka kuja kupanda gari karibu na cheni ya ushuru.

Sasa kumbe kitendo hiki ndani ya hiyo stendi ni makosa. Traffics wakaaanza kufosi kuwaandikia wale madereva faini.

na wale madereva walijitetea kwamba:, hapa ni ndani ya stendi, sasa kwanini mtuandikie faini eti kwasababu tu abiria kachelewa toilet na kuja kupandia hapa karibu na cheni ya ushuru wakati cheni hii ipo ndani ya stendi?. maeleezo yote hayo hayakubadili kitu kwa wale trrafics, wale madereva kwa unyonge wakatoa leseni zao, faini ikaandikwa.

sasa kimbembe kilianza pale walipokuja kwenye gari letu. Trafik akamwambia konda wa gari letu:, mwambie dereva aje hapa (mbele ya gari).

konda akamwambia Dereva kwamba anaitwa:

Dereva: Mwambie aje yeye na sio.

Konda akamwambia Trafik, dereva amesema uende wewe.

Trafik akenda kwa dereva.

Traffic: Naomba leseni yako.

Dereva: Leseni yangu unaitaka ya nini?.

Traffic: Kuna kuna kitu nataka kukagua.

Dereva: Wewe unakagua leseni kama nani? Kama una mashaka na leseni yangu muite 'VEKO' aje anikague na sio wewe.

Ikabidi trafiki afunguke zaidi kimaelezo.

Trafik: Ndani ya stendi hii tuna utaratibu wa kutokuruhusu gari kubeba abiria karibu na cheni ya ushuru.

Dereva: Utaratibu wenu sio sheria rasmi, Sheria inaniruhusu kubeba abiria eneo lolote ndani ya stendi.

Trafik: Maneno yako hayatakusaidia, nipe leseni niandike faini, utachelewesha abiria bure.

Dereva: Leseni sitoi, na ili nitoe leseni inabidi unionyeshe mipaka ya stendi, stendi inaanzia wapi na kuishia wapi.

Trafik: Haya toa gari upeleke kituoni.

Dereva: Hapa gari sitoi, hadi umuite (sijui DOD alitamka jina moja hivi, ila ni jina la kitengo ndani ya jeshi la polisi) ama nichukue picha za eneo nilipopaki gari, ndo nitoe gari.

Trafiki akatoka eneo lile na kusogea pembeni kidogo akaanza kuongea kwenye simu, akawa ni kama vile anatoa maelezo juu ya tukio linaloendelea hapo. Baada ya sekunde 20 akarudi kwa dereva na kumpa simu aongea na huyo si DOD dereva akatoa maelezo yote. DOD akamwambia dereva: Kama ulikuwa umeshampa leseni yako, mwambie akurudishie utoe gari uende zako.

Dereva akatoa gari, tukaondoka bila kupigwa faini kama walivyopigwa wengine.

Nikabaki najiuliza: Ni kwa vipi wale madereva wengine walishindwa kujisimamia kama huyu alivyofanya? Kabla sijapata jibu nikakumbuka kitu kimoja kuhusu yule dereva mbishi. Lafudhi yake ni ya nchi jirani kwa akina Odinga. Nadhani UTHUBUTU wa kuhoji na kujisimamia vinabebwa na asili ya mtu. Jamaa alikuwa na guts ya kuwabishia wale trafiki kwa ustaarabu tu.

Tukio hilo likanikumbusha hali yetu ya kisiasa, na nilichogundua ni kwamba mtaji wa CCM sio katiba ama mihimili mingine kuwa mibovu, Mtaji wa CCM ni kundi kubwa la watu wajinga waliopo ndani ya nchi hii.

Tanzania kuna watu wajinga aisee. Na huo ndio mtaji wa CCM kuliko kitu kingine.

CCM wamewekeza kwenye ujinga ili waendelee kutawala, na tujue Tanzania ndo nchi pekee inayoweza kuongozwa na mtu yoyote yule awe malaika ama shetani.

Wewe kiongozi itahitajika huruma zako na busara zako tu kuwaongoza watanzania katika Haki na USAWA, lakini ukisema uwaongeoza kwa mkono wa chuma, Hakuna mtanzania wa kukuonyooshea kidole japo kuna kundi dogo sana (la mtandaoni) ila kundi ili ni dhaifu mno. Kundi ili la wajinga lita endelea kuwa mtaji wa wanasiasa wachumia tumbo hata baada ya CCM kuondoka madarakani.

CCM inaweza anguka leo ama kesho, lakini kundi ili mwisho wake sio leo ama kesho. Guts aliyonayo jiwe sio kwasababu ya jeshi kuwa nyuma yake, bali kundi kubwa la wajinga liko nyuma yake. Kundi ambalo mtu anapewa tisheti na kusahau shida zake zote.

Hata kama tutakopi katiba nzima ya Marekani, hilo halita saidia. So, tatizo hapa sio katiba, tatizo ni sisi Watanzania wenyewe. Leo jiwe akiteuliwa kuwa rais wa Marekani, atabadilika na kuwa rais tofauti kabisa.

Tutahitaji katiba mpya na miimili isiyoweza kupokwa MAMLAKA yake na muimili mwingine (serikali) lakini bila Watanzania wenye akili timamu ilo HALIWEZEKANI kusimama, mwisho wa siku tunarudishwa kule kule.

Unapoona demokrasia ya marekani iko pale si kwamba kule kuna serikali IMARA NA MIIMILI imara tu, bali wananchi wa marekani ni imara zaidi kuliko miimili yote, ndo maana ukizingua pale jumba jeupe unatoka mapema tu. Sasa Tanzania ni nani mwenye UTHUBUTU huo?.

Gari moja tu la 'washawasha' likipita mtaani nia na dhamira nzima inapotea. Vijana ambao ni tegemezi wa kuleta mabadiliko wapo FB kwenye page za akina Gigy, Mond ana Harmo.

FUTURE YA TANZANIA SIIONI KABISA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo jiwe akiteuliwa kuwa Raisi wa marekani atabadilika na kuwa rais tofauti kabisa. Hahahahahhhhahahaha pamoja na kwamba ni mfano ila jiwe katu hawezi kuwa Raisi wa Marekani watamtoa ndani ya masaa 24.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mbalaka, Katika kundi la unaosema wajinga, wewe umo. Kwasababu:

1. Haki za binadamu zinastahili kwa binadamu wote, sio wenye elimu au nguvu tu!
2. Watawala na vyombo vyao (traffic police) ndiyo wanaowajibika kuheshimu sheria na haki za binadamu.
3. Haihitaji elimu au hekima kuminya democracy na kuiba kura, ni woga, ujinga na bunduki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeleta kitu kizuri kwenye platform lakini badala ya kutumia neno ujinga nadhani ungetumia neo UWOGA kama siyo UOGA mtanisahihisha kiswahili. Watanzania siyo kwamba hawajui haki zao wanajua sana ila tu ni waoga wa kutetea haki zao. Ndo maana wasimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa hawajatolewa hata na ngeu kidogo au kukata mashamba yao ya mahindi ili kuwapa funzo kwamba haki zetu zisichezewe. We are simply timid.
 
Last week nilikua natoka mkoa, ndani ya basi nililokuwa nimepanda mbele yetu kulikuwa na mabasi mengine mawili.

Gari zilikimbia kwa muda mrefu hatimahye tukaingia stendi moja hivi ndogo tu. wahudumu wakatuambia tuna dakika 5 za kuchimba dawa katika stend hiyo. Baada kumaliza kuchimba dawa tukaanza kutoka ndani ya hiyo stend, wakati tunakariba kwenye cheni ya ushuru wa stend, gari la mbele yetu likasimamishwa na traffic, tulio kuwa gari ya nyuma mwanzo hatukujua tatizo nini ila baadae ikabainika kwamba wakati gari zinatoka na kukaribia cheni ya ushuru kuna baadhi ya abiria waliokuwa wamechelewa kupanda gari ilipokua imepaki hali iliyopeleka kuja kupanda gari karibu na cheni ya ushuru.

Sasa kumbe kitendo hiki ndani ya hiyo stendi ni makosa. Traffics wakaaanza kufosi kuwaandikia wale madereva faini.

na wale madereva walijitetea kwamba:, hapa ni ndani ya stendi, sasa kwanini mtuandikie faini eti kwasababu tu abiria kachelewa toilet na kuja kupandia hapa karibu na cheni ya ushuru wakati cheni hii ipo ndani ya stendi?. maeleezo yote hayo hayakubadili kitu kwa wale trrafics, wale madereva kwa unyonge wakatoa leseni zao, faini ikaandikwa.

sasa kimbembe kilianza pale walipokuja kwenye gari letu. Trafik akamwambia konda wa gari letu:, mwambie dereva aje hapa (mbele ya gari).

konda akamwambia Dereva kwamba anaitwa:

Dereva: Mwambie aje yeye na sio.

Konda akamwambia Trafik, dereva amesema uende wewe.

Trafik akenda kwa dereva.

Traffic: Naomba leseni yako.

Dereva: Leseni yangu unaitaka ya nini?.

Traffic: Kuna kuna kitu nataka kukagua.

Dereva: Wewe unakagua leseni kama nani? Kama una mashaka na leseni yangu muite 'VEKO' aje anikague na sio wewe.

Ikabidi trafiki afunguke zaidi kimaelezo.

Trafik: Ndani ya stendi hii tuna utaratibu wa kutokuruhusu gari kubeba abiria karibu na cheni ya ushuru.

Dereva: Utaratibu wenu sio sheria rasmi, Sheria inaniruhusu kubeba abiria eneo lolote ndani ya stendi.

Trafik: Maneno yako hayatakusaidia, nipe leseni niandike faini, utachelewesha abiria bure.

Dereva: Leseni sitoi, na ili nitoe leseni inabidi unionyeshe mipaka ya stendi, stendi inaanzia wapi na kuishia wapi.

Trafik: Haya toa gari upeleke kituoni.

Dereva: Hapa gari sitoi, hadi umuite (sijui DOD alitamka jina moja hivi, ila ni jina la kitengo ndani ya jeshi la polisi) ama nichukue picha za eneo nilipopaki gari, ndo nitoe gari.

Trafiki akatoka eneo lile na kusogea pembeni kidogo akaanza kuongea kwenye simu, akawa ni kama vile anatoa maelezo juu ya tukio linaloendelea hapo. Baada ya sekunde 20 akarudi kwa dereva na kumpa simu aongea na huyo si DOD dereva akatoa maelezo yote. DOD akamwambia dereva: Kama ulikuwa umeshampa leseni yako, mwambie akurudishie utoe gari uende zako.

Dereva akatoa gari, tukaondoka bila kupigwa faini kama walivyopigwa wengine.

Nikabaki najiuliza: Ni kwa vipi wale madereva wengine walishindwa kujisimamia kama huyu alivyofanya? Kabla sijapata jibu nikakumbuka kitu kimoja kuhusu yule dereva mbishi. Lafudhi yake ni ya nchi jirani kwa akina Odinga. Nadhani UTHUBUTU wa kuhoji na kujisimamia vinabebwa na asili ya mtu. Jamaa alikuwa na guts ya kuwabishia wale trafiki kwa ustaarabu tu.

Tukio hilo likanikumbusha hali yetu ya kisiasa, na nilichogundua ni kwamba mtaji wa CCM sio katiba ama mihimili mingine kuwa mibovu, Mtaji wa CCM ni kundi kubwa la watu wajinga waliopo ndani ya nchi hii.

Tanzania kuna watu wajinga aisee. Na huo ndio mtaji wa CCM kuliko kitu kingine.

CCM wamewekeza kwenye ujinga ili waendelee kutawala, na tujue Tanzania ndo nchi pekee inayoweza kuongozwa na mtu yoyote yule awe malaika ama shetani.

Wewe kiongozi itahitajika huruma zako na busara zako tu kuwaongoza watanzania katika Haki na USAWA, lakini ukisema uwaongeoza kwa mkono wa chuma, Hakuna mtanzania wa kukuonyooshea kidole japo kuna kundi dogo sana (la mtandaoni) ila kundi ili ni dhaifu mno. Kundi ili la wajinga lita endelea kuwa mtaji wa wanasiasa wachumia tumbo hata baada ya CCM kuondoka madarakani.

CCM inaweza anguka leo ama kesho, lakini kundi ili mwisho wake sio leo ama kesho. Guts aliyonayo jiwe sio kwasababu ya jeshi kuwa nyuma yake, bali kundi kubwa la wajinga liko nyuma yake. Kundi ambalo mtu anapewa tisheti na kusahau shida zake zote.

Hata kama tutakopi katiba nzima ya Marekani, hilo halita saidia. So, tatizo hapa sio katiba, tatizo ni sisi Watanzania wenyewe. Leo jiwe akiteuliwa kuwa rais wa Marekani, atabadilika na kuwa rais tofauti kabisa.

Tutahitaji katiba mpya na miimili isiyoweza kupokwa MAMLAKA yake na muimili mwingine (serikali) lakini bila Watanzania wenye akili timamu ilo HALIWEZEKANI kusimama, mwisho wa siku tunarudishwa kule kule.

Unapoona demokrasia ya marekani iko pale si kwamba kule kuna serikali IMARA NA MIIMILI imara tu, bali wananchi wa marekani ni imara zaidi kuliko miimili yote, ndo maana ukizingua pale jumba jeupe unatoka mapema tu. Sasa Tanzania ni nani mwenye UTHUBUTU huo?.

Gari moja tu la 'washawasha' likipita mtaani nia na dhamira nzima inapotea. Vijana ambao ni tegemezi wa kuleta mabadiliko wapo FB kwenye page za akina Gigy, Mond ana Harmo

FUTURE YA TANZANIA SIIONI KABISA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, Naunga mkono hoja, Watanzania ni watu dhaifu sana, waoga, sana, wapole mpaka wanakuwa Wajinga, Watawala wakion
gozwa na CCM wanalijua hilo..

Kama CCM wangelitumia huu upole wa Watanzania kwa manufaa ya Taifa, nchi ingelipiga hatua sana.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake..
 
Da. Hongera mtoa hoja. Umeandika kitu halisi kuhusu watanzania. Huwa najiuliza tumemwagiwa nini vichwani?

Yaani kama kuombeana kupo na kuna maana, yafaa tuombewe. Lakini ni nani atatuombea.

Wapi tuanzie?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom