Tatizo si Katibu Mkuu Makamba

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,283
976
Tatizo la CCM ni mawazo ya kizee na matendo ya kibepari. Kabla ya kubadili uongozi, kwanza wabadili fikra zao juu ya taifa la sasa la tz.. Wasiendelee kuamini kwamba mtanzania wa sasa ndio yule yule wa zamani, wa "ndio mzee" kwa kila kitu.. Watu wanataka kuhoji kwa kila kitu na si kupelekeshwa.
 
mkuu ... mbona mawazo yako ni tofauti na ID yako....
 
mkuu ... mbona mawazo yako ni tofauti na ID yako....

Mwacheni, akili yake imevua gamba.

Ametoa mfano halisi wa walichotakiwa ccm kufanya, yaani walitakiwa wavue gamba akili zao
 
Tatizo la CCM ni mawazo ya kizee na matendo ya kibepari. Kabla ya kubadili uongozi, kwanza wabadili fikra zao juu ya taifa la sasa la tz.. Wasiendelee kuamini kwamba mtanzania wa sasa ndio yule yule wa zamani, wa "ndio mzee" kwa kila kitu.. Watu wanataka kuhoji kwa kila kitu na si kupelekeshwa.
It is true Makamba and his secretariat is not a problem at all. Tatizo ni ufisadi, sera mbovu za privatatization, kukalibisha wawekazaji matapeli kuchukua ardhi ya wananchi kwa nguvu, mikataba mibovu na wizi wa madini unaofanyika usiku na mchana etc.
 
Hit the point; TATIZO LA CCM NI KUKUMBATIA UFISADI period!

Hilo laweza kuwa moja lingine ni "dhuruma". Dhuruma ni pamoja na;

1.Kitendo cha mpiga kura kumpigia kura "A" alafu ukampitisha "B" ndiyo awe kiongozi wake.
2.Kitendo cha kuzuia mwananchi asitoe maoni yake kuhusiana na muswaada wa mchakato wa katiba mpya
 
Kwi kwi kwi!! CCM bana they always solve the wrong problem!
If chenge,lowassa,rostam hawatafukuzwa na kushitakiwa there is no way ccm inaweza kuvutia vijana(tomorrow's voters)
 
Me nlijua atakuwa ameleta u mbumbumbu hapa kumbe sivyo.... Nimeyapenda mawazo yako
 
Wanachama wa chama cha kijani walikuwa wanapiga kelele kuhusiana na Makamba huku wakisahau kuwa beyond that kuna watu ambao bila wao kutolewa hakuna chohcote kile ambacho kitakachobadilika haya tumeona Sekretarieti ya CCM imejiuzulu lakini hilo halitoshi maana wao badala ya kubadili FIKRA na MATENDO yao wao wanabadili matairi wakati injini ndio mbovu
 
ccm ilitakuwa kuvua gamba la ufisadi

Naona gamba limegoma kuvurika

Ni kweli mkuu. CCM wanatakiwa waonyeshe kwa vitendo kuwa sasa ufisadi basi. Maliasili zetu yakiwamo madini, mbuga za wanyama, bandari zitumike vizuri kwa manufaa ya watanzania wote. Huduma za jamii ziboreshwe ikiwamo elimu, afya, maji, umeme n.k. Wahujumu uchumi kama Lowasa, RA, Chenge, Karamagi na wenzao washughulikiwe. Hapo sasa tutaona kweli wamebadilika.
 
Tatizo hasa lilianza na JK mwenyewe na wanamtandao wake wa kuusaka Urais tangu ile 1995. Mengine haya ni matokeo tu ya huo mchakato wa urais wa JK. Ni vigumu mno kwa JK huyuhuyu kukisafisha chama hiki. Kwa vile Kamati Kuu ilijiuzuru na yeye alipaswa kujiuzuru angalau uenyekiti wa CCM( T).
 
Tatizo sio CHENGE,ROSTAM,LOWASA AU MAKAMBA,tatizo ni mfumo,toka kufutwa kwa Azimio la Arusha,nakuletwa azimio la Zanzaibar hawakuweka miiko ya uongozi,kama ilivyokuwa ya azimio la Arusha,nakumbuka Baba wa Taifa alieleza sana hili,kwahiyo atatukiwahangamiza hao wanaoitwa mafisaidi bado watazaliwa wengine tu,tena kwa kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya..........kwahiyo bado CCM haijatibu maradhi yake,ni mpaka hapo katiba mpya itakapopatikana.....
 
Tatizo la CCM ni mawazo ya kizee na matendo ya kibepari. Kabla ya kubadili uongozi, kwanza wabadili fikra zao juu ya taifa la sasa la tz.. Wasiendelee kuamini kwamba mtanzania wa sasa ndio yule yule wa zamani, wa "ndio mzee" kwa kila kitu.. Watu wanataka kuhoji kwa kila kitu na si kupelekeshwa.
Huo ndiyo ukweli, bila kubadili fikra wataendelea kujivua magamba kama nyoka wakati wa jua kali lakini bado itatokea ngozi nyingine ya aina ileile. Kama ccm wanataka kweli kuwa chama cha mfano isiishie makamba tu, kuna wengi zaidi ya makamba bado ndani ya chama na mawazo yao bado ni ya miaka ya enzi za TANU na ASP, bila gamba hilo kuondolewa itakuwa bure kwani itakuwa sawa na kukata mti matawi ukiamini yataota mengine ya tofauti
 
Tatizo la CCM ni mawazo ya kizee na matendo ya kibepari. Kabla ya kubadili uongozi, kwanza wabadili fikra zao juu ya taifa la sasa la tz.. Wasiendelee kuamini kwamba mtanzania wa sasa ndio yule yule wa zamani, wa "ndio mzee" kwa kila kitu.. Watu wanataka kuhoji kwa kila kitu na si kupelekeshwa.

Si kweli, MAKAMBA ni tatizo, isipokuwa makamba si tatizo pekee, ni kweli fikra lazima ibadilike lakini officials kama makamba, nkuchika, JK ni lazima, katika ile process ya kujivua gamba, waachie ngazi.

Hili la CCM kubadili fikra haliakiwi litangulie linatakiwa liende sambamba na lile la kuwang'oa watu kama makamba, kosa.
 
Nakubaliana na mawazo ya wenzangu kama ingekuwa injini ya gari basi ingeshushwa chini na kuweka nyingine .
 
Makamba alikuwa sehemu kubwa ya tatizo kwani utendaji wake haukuwa na ufanisi zaidi. Lakini Mkulu naye sijui anajifichia wapi kwani walengwa wakubwa wa tatizo naona anawapapasa tu. Watanzania wanataka kusikia na kuona kitu kimetendeka kwa akina Chenge, EL, RA na washirika wake. Naona kimya ikiashiria kuwa bado kitu hakijafanyika hapo.
 
Back
Top Bottom