Wakuu habari zenu. Naomba niende kwenye lengo mahususi bila kupoteza muda.
Ninapata changamoto kwenye simu yangu tangu niiwekee memory card majuzi juzi baada ya storage yake mama kuzidiwa. Nimehamisha nyimbo mp3 zote zilizokuwa kwenye memory ya simu na kuzipeleka kwenye memory card niliyoweka. Zinaonekana vizuri ila kimbembe kinakuja kwenye kuzicheza sasa. Kila media player niliyonayo haizichezi. Tatizo litakuwa wapi?