Daudi1
JF-Expert Member
- Dec 14, 2013
- 8,805
- 8,716
Habari ndugu zanguni, nawasalimuni wote kila mmoja kwa imani yake
Niende moja kwa moja kwwnye hoja ya leo, kumekuwa na malalamiko mengi juu ya mahusiano mpaka inafikia mahali inaonekana mahusiano hayana maana tena, wengine wamefanya mahusiano kuwa biashara, wengine imekuwa uwanja wa vita kuonyesha uwezo na ujanja maana halisi ya mahusiano haieleweki hasa kwa kizazi cha sasa.
Mwingine ukimwambia suala la mahusiano fikra zinazoingia kwake ni ngono hicho ndo anachokifahamu, mwingine atawaza kupewa zawadi/hela na mambo kadha wa kadha. Tatizo ni upendo wa kwanza kupungua, ule upendo wa kumpenda mpenzi wako kama unavyojipenda haupo tena, saizi upo upendo wa nipe nikupe.
Tatizo hili ni kubwa sana kwa sisi vijana wa sasaivi hasa kwa wanandoa, tumeshindwa kupendana katika uhalisia wake "tumetanguliza sentensi ya nitapata nini" yaani leo unamtongoza binti anakuambia utaniweza? Sasa nisikuweze kwa lipi wewe tembo? Mwingine anakuuliza nikikukubalia utanipa nini?? Aaaggrrr yaani wanajiweka kimtego mtego, tatizo upendo tumetanguliza vitu tumechukulia kama fursa fulani.
Upendo wa kweli hauangalii vitu, ukimpenda mtu sawa sawa,
1. Hautaangalia madhaifu aliyonayo bali utamvumilia
2. Hautamhesabia makosa kwamba jana ulinifanyia hivi, leo tena..
3. Utakuwa mwepesi wa kumsamehe kwa kuwa unampenda
4. Hautapenda awe katika msongo wa mawazo kwani ndiye furaha yako hivyo utamsaidia
5. Hautamtangaza vibaya kwa marafki hata kama kuna mahali hakutendei haki au hakuridhishi
6. Utaridhika na hali aliyonayo, iwe kiuchumi, kimaumbile au kwa namna alivyo
7. Utamthamini na kumheshimu kama wewe unavyopenda kufanyiwa.
Na upendo wa mtu kwa mwenzi wake unapungua kutokana na yafuatayo:
1. Dharau kwa mwanamke au mwanaume, yaani kuona kama bila wewe yeye hana maisha, au kuona kama wewe ndo umemfanya vile alivyo
2. Kutomsikiliza hasa wanawake wanapenda sana kusikilizwa hata kama jambo la kipuuzi msikilize tuu usipofanya hivyo ataona unampuuza hana maana kwako
3. Kukosa utii hasa kwa wanawake wamekosa utii kwa waume zao,hakuna mwanaume asiyependa mwanamke amtii, na wanawake wengi wanaona kumtii mwanaume ni utumwa hilo ni tatizo.
4. Kusema madhaifu ya mwenzi wako kwa mashost au masela, labda nikuambie kitu cha uhakika si kila mtu anapenda mahusiano yako na mwenzako hivyo ukianza kusimulia ya ndani unampa point ya kukuumiza tumeona na kushuhudia wengi wakipoteza mahusiano yao.
Mwisho kabisa rudisha upendo ule wa mwanzo kwa mpenzi wako na mahusiano yako yatakuwa salama, achana na habari za kuomba omba ushauri juu ya mahusiano yako inapotokea mmetofautiana tafuta suluhu mwenyewe, muwe na siku njema