Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
- Thread starter
- #21
Mi nafikiri ni vyote, Elimu na Uelewa mdogo...! Nitawaadisieni kisa kimoja halfu mtoe muone hali halisi ya uongozi tulionaoambao CCM imetupa.
Hivi unajua hela tulizozipata baada ya kuuza mashirika ya umma zilifanyia nini? Zile hela badala ya kuziwekeza katika miundombinu na kuboresha usimamizi wa mashirika hayo, Serikali ya Mkapa iliamua kutumia hela hizo kwa ajili ya kununulia silaha (magari ya kivita pamoja na mabomu, na vifaa vingine vya kijeshi)...!
Huu ni mfano kidogo tu, sasa kwa jambo kama hili unaweza ukaliiltaje? Ukosefu wa akili, elimu au ni wendawazimu? Hivi kweli unauza mashirika ya umma halafu unawekeza kwenye silaha?
Kwa hali iliyopo sasa na mfumo CCM inaoujenga ni kwamba, madaraka ni "ULAJI" na sio "UWAJIBUKAJI". Ndio maana watu wanapoteuliwa UWaziri huwa ni kupongezana na kusheherekea...! Kila kukicha ni skendo za ufisadi na unadhirifu wa mali za umma lakini sijawahi kuona kiongozi hata mmoja ame resign au hata kuchukuliwa hatua...! On the account kwamba Kikwete anaogopa akichukuliwa hatua inaweza ikamrudi hapo baadae wakati amestaafu wanaweza wakamfanyia hivo hivo....!
Hatuna vipimo au vigezo vya kuwapima viongozi wetu. Viongozi hawana ubunifu, mawazo yamekua mgando...! nafikiri kuna haja ya kuiondokana na CCM ili walau kutoa mwanya kwa wengine nao walete mawazo mapya na utendaji mpya.
sasa sijui alikuwa anataka kwenda kupigana na nani, vita vyenyewe sku hizi hakuna labda akapigane na wananchi wake