Tatizo ni ngozi nyeusi au uelewa mdogo? au ni elimu ndogo

Mi nafikiri ni vyote, Elimu na Uelewa mdogo...! Nitawaadisieni kisa kimoja halfu mtoe muone hali halisi ya uongozi tulionaoambao CCM imetupa.

Hivi unajua hela tulizozipata baada ya kuuza mashirika ya umma zilifanyia nini? Zile hela badala ya kuziwekeza katika miundombinu na kuboresha usimamizi wa mashirika hayo, Serikali ya Mkapa iliamua kutumia hela hizo kwa ajili ya kununulia silaha (magari ya kivita pamoja na mabomu, na vifaa vingine vya kijeshi)...!

Huu ni mfano kidogo tu, sasa kwa jambo kama hili unaweza ukaliiltaje? Ukosefu wa akili, elimu au ni wendawazimu? Hivi kweli unauza mashirika ya umma halafu unawekeza kwenye silaha?

Kwa hali iliyopo sasa na mfumo CCM inaoujenga ni kwamba, madaraka ni "ULAJI" na sio "UWAJIBUKAJI". Ndio maana watu wanapoteuliwa UWaziri huwa ni kupongezana na kusheherekea...! Kila kukicha ni skendo za ufisadi na unadhirifu wa mali za umma lakini sijawahi kuona kiongozi hata mmoja ame resign au hata kuchukuliwa hatua...! On the account kwamba Kikwete anaogopa akichukuliwa hatua inaweza ikamrudi hapo baadae wakati amestaafu wanaweza wakamfanyia hivo hivo....!

Hatuna vipimo au vigezo vya kuwapima viongozi wetu. Viongozi hawana ubunifu, mawazo yamekua mgando...! nafikiri kuna haja ya kuiondokana na CCM ili walau kutoa mwanya kwa wengine nao walete mawazo mapya na utendaji mpya.

sasa sijui alikuwa anataka kwenda kupigana na nani, vita vyenyewe sku hizi hakuna labda akapigane na wananchi wake
 
umetumwa na ccm? sijui hata unajua unachokiongea ndugu yangu...wewe hujaona jinsi ccm wanavyotugawanya kidini? angalia hata uchaguzi uliopita angalia cuf walipata kura ngapi sehemu za pwani na angalia walipata kura ngapi sehemu za kilimanjaro na arusha huko? kwa nini?
Ungemalizia pia kwanini chadema wamepata kura nyingi katika mikoa uliyoitaja swali lako lingekua zuri zaidi, But naomba nikufahamishe kila mtu anauelewa wake na anamchagua yule anayemuona anafaa na kama watu wanachagua viongozi kwa sababu ya dini zao ujue hawajielewi. Niliposema c.c.m ni chama chenye mchanganyiko zaidi wa watu wa dini tofauti hiyo ni kweli. Au kama kuna chama kingine chochote chenye uwiano mzuri wa watu wa dini tofauti (mfano kwenye nafasi za ubunge) zaidi ya C.c.m nifahamishe nipo tayari kujifunza.kwenye ukweli tusemeni kweli sio kutumia siasa kila kitu Dat is not Fair. Pia nina hamu sana yakufahamu ni vipi C.c.m imewagawa kidini? Siiungi mkono c.c.m pia siungi mkono uongo wala sidhani kama kuna chama cha dini Tanzania.kwa mtazamo wangu vyote ni vya wafanyabiashara wala hakuna haja ya kumwagana damu kwa ajili ya maslahi yao.
 
ccm ndio walioeneza dirty politics kuwa CUF ni chama cha waislam na hatimaye wakakiua na sasa kwa style ileile wakadai kuwa dr Slaa ni padri, na lengo lao ni kuusambaratisha upinzani tu ili maovu yao yasifichuke.nadhani umenipata kijana,ndio maana mimi nasema hivi ccm ni kama mubaraka na gadafi. This regime must end now. Wewe nchi kama Tanzania sio ya kuwa na umeme wa mashaka kiasi hiki watu wenyewe wanaoptaka huo umeme hawazidi 20% wtf is this? Tuendelee kuwachekea tu?..angalia ukiachana na rasilimali wanatukata kodi kila siku hela wanapeleka wapii wananunua bajaji kwa dola 5900 kila bajaji moja? Wanatudharau sana hawa 5900 na 6000 kuna tufauti gani?? They just playing with our mind hapa kuna hela inataka kuibwa hapa. Ok . Kama utanielewa nitashukuru na ninakaribisha critism pia
 
I'm very sad Mr Ivuga.But kilio chetu CHADEMA wamekisikia hivy watatufut machoz ye2 ifikap Mwaka 2015.Ni kwel hay ulioongea ila hii nchi imeshikwa na wachache na hap ndip 2naon hat uhuru 2liopat ni wa watu wachache na sio wa wote.But Chadema under Slaa anataka kuufanya Uhuru huu kuwa wa wote ifikap Mwaka 2015.
 
ccm ndio walioeneza dirty politics kuwa CUF ni chama cha waislam na hatimaye wakakiua na sasa kwa style ileile wakadai kuwa dr Slaa ni padri, na lengo lao ni kuusambaratisha upinzani tu ili maovu yao yasifichuke.nadhani umenipata kijana,ndio maana mimi nasema hivi ccm ni kama mubaraka na gadafi. This regime must end now. Wewe nchi kama Tanzania sio ya kuwa na umeme wa mashaka kiasi hiki watu wenyewe wanaoptaka huo umeme hawazidi 20% wtf is this? Tuendelee kuwachekea tu?..angalia ukiachana na rasilimali wanatukata kodi kila siku hela wanapeleka wapii wananunua bajaji kwa dola 5900 kila bajaji moja? Wanatudharau sana hawa 5900 na 6000 kuna tufauti gani?? They just playing with our mind hapa kuna hela inataka kuibwa hapa. Ok . Kama utanielewa nitashukuru na ninakaribisha critism pia
Nakushukuru sana kwa maelezo yanayoendana na upeo wako>Kuhusu umeme na hayo mabajaji ni ujinga ulio wazi hata Watoto wanajua.labda nikuulize tena ndugu yangu kuna hutuba yoyote ambayo Huyu rais wa CCM JK amesema msimchague slaa kwa sababu ni padri au msimchague lipumba kwa sababu ni muislamu?
Kama nikweli c.c.m imewafanya muamini kua CDM au CUF ni vyama vya kidini Tatizo lao au lenu?hebu nieleweshe pale watu wanaposema c.c.m au JK ni wadini wanamaanisha nini?inamaana unataka kusema wanaanchi wa Tanzania hawajielewi kiasi hicho?labda uniambie kwa mtazamo wako Je kuna chama cha kidini Tanzania?Kwa mtzamo wangu vyama vyote vipo kwa ajili ya maslahi binafsi.Nakuunga mkono kua C.C.M inatakiwa iondoke. But tusiishie hapo lazima tumalizie JE TUMUWEKE NANI? Lipumba au Slaa au Mrema au Mr.2?maana wote ninaowaona mbele yangu ni vituko vitupu
 
Tatizo ni uwezo mdogo wa viongozi wa serikali ya CCM, ni kweli.

But what's the alternative?

Waziri Sugu? Waziri Regia Mtema? Waziri Cheyo? Waziri Shibuda? Waziri Mrema? Waziri Zitto?

Na yule no-name, no-re'sume, aliyegombea u-VP kwenye tiketi ya Slaa, sijui nani yule, ndio awe VP.

Yani ndio tungejenga hizo treni za Tunis na kina Waziri Sugu? Tafadhali sana!
 
JK hajawahi kusema kuwa Slaa ni padri , ila JK ashawahi kusoma kuwa yeye sio John na watu wakampigia makofi mikoa ya kusini huko, na kwa nini umekimbilia moja kwa moja kumtaja mr 2? Naona unaleta mzaha hapa ndugu yangu na hakuna sehemu yoyote ambayo mimi nemempigia mr debe hapa , na kama huoni mtu wa kutuongoza ina maana basi wewe usharidhika na maisha wanayoishi watanzania. Na kama ullikuwa unafuatilia bunge lililopita naomba unipe mfano mmoja tu wa kiongozi/mbunge aliyetetea maslahi ya wananchi zaidi ya dr Slaa, hapa tuweke vyama pembeni kwanza naomba unipe uwezo wao binafsi
 
nakutukana but via inbox.
Kwa mtizamo wako waziri sofia simba , waziri mwinyi, makamba ,ngeleje, rostam aziz,lowasa wamekufanyia nini? Nipe mfano mmoja tu hai ngeleja kafanya nini kinachoonekana kwenye ile wizara? Kitu ambacho tungemuweka form 4 leaver asingeweza kukifanya.
 
Tatizo ni uwezo mdogo wa viongozi wa serikali ya CCM, ni kweli.

But what's the alternative?

Waziri Sugu? Waziri Regia Mtema? Waziri Cheyo? Waziri Shibuda? Waziri Mrema? Waziri Zitto?

Na yule no-name, no-re'sume, aliyegombea u-VP kwenye tiketi ya Slaa, sijui nani yule, ndio awe VP.

Yani ndio tungejenga hizo treni za Tunis na kina Waziri Sugu? Tafadhali sana!

wewe nawe...unadhani hizo treni zilijengwa na hao viongozi? Moja ya kazi za serikali ni kuwezesha maendeleo. Huyo no-name VP angeweza sana kujenga hali ya uwezeshaji. Huhitaji degree hata moja kujua hali halisi ya nchi na kutafuta njia za kuwezesha wananchi kuleta maendeleo. Inaonyesha kuwa wewe ni moja ya product za poor education system ya bongo! Yani unasema ni bora kuchagua mwizi kwa vile huyo mwingine hajulikani?
 
Wanandugu nimekuja hapa, nikiwa nina masikitiko makubwa kabisa , nchi yetu na wananchi wake(sisi) ..mpaka sasa hivi najiuliza kwa nini tunaikumbatia ccm? kina mods naomba msije mkaifuta thread yangu kwa sababu ni mawazo yangu na sijaribu kumtukana mtu ila najaribu tu kuweka mambo wazi na kupasua jipu.
Ukiangalia waarabu nchi zao huwezi kuzifananisha na nchi kama Tanzania,sisi nchi yetu ni maskini sana kuanzia mjini hadi vijijini , nishawahi kufika Tunis na Cairo ni miji mizuri sana na huwezi hata siku moja kuifananisha na mji wowote wa Tanzania , pale tunis kuna treni ndogo ndogo (behewa moja) zinatumia umeme kwa hiyo suala la usafiri kwao sio tatizo ukikompare na sisi watoto wa ngozi nyeusi.
Lakini jamaa kwa vile yale maendeleo hayaendani na rasilimali zao walizo nazo wakaamua kujitoa mhanga na damu zao zikamwagika ili mradi tu regime ile iondoke, hawa waarabu wanafanana kabisa na sisi , tunisia walikuwa na rais wao kwa muda mrefu Egypt alikuwepo Mubaraki na Libya yuko Gaddafi lakini hawa viongozi wote wameshachokwa , nikirudi hapa kwetu kuna hili dude ccm, this regime should end now.
Kwa sababu hawa jamaa wanatudanganya wanatudharau na wanatubeza na wanataka kutugawanya kiudini. mimi nina jiuliza kwa nini hatutaki kuwatoa hawa jamaa? au akili zetu ni fupi? kitu gani wameturidhisha nacho? watu wanapenda tu madaraka na hawapendi kuwajibika , hakuna anayetaka kuresign hata kama amefanya kosa linalomtaka yeye awajibike. so what to do? uwoga jamani utatuua na tutaendelea kubaki maskini hivi hivi!! maisha tunayoishi hayaendani hata kidogo na nishati ambazo tunazo au amabazo tunazalisha nchi kama Tanzania asilimia ya wananchi wake wanaotumia umeme haizidi 20%.. na ndani ya hao watu ishirini huwezi kuwapatia umeme wa uhakika. this aint joke anymore na hii inamaanisha kuwa wewe hiyo nafasi uliyopo haikufai na sio yako. I guess JK pale alipo kawekwa na hana sauti yoyote thats why hawezi kufanya maamuzi yoyote, na sisi watu kama hawa hawatufai katika karne hii.tuiondoe CCM

Usikae hata siku moja na kudharau rangi yako. Unaonyesha fikra duni sana na kutojiamini!
Jibu unalo alafu unazunguka mbuyu. The answer is EDUCATION. Watu hawajui alternative to shida. Wewe kama huna umeme utajuaje uzuri wa kuwa na umeme? Kama umezoea kubanana kwenye daladala, utajuaje uzuri wa kuwa na electric trains. Kama umezoea foleni, shida ya maji, nk, kweli utaweza kuchagua alternative? Hapo ndipo maswali yalipo...
 
JK hajawahi kusema kuwa Slaa ni padri , ila JK ashawahi kusoma kuwa yeye sio John na watu wakampigia makofi mikoa ya kusini huko, na kwa nini umekimbilia moja kwa moja kumtaja mr 2? Naona unaleta mzaha hapa ndugu yangu na hakuna sehemu yoyote ambayo mimi nemempigia mr debe hapa , na kama huoni mtu wa kutuongoza ina maana basi wewe usharidhika na maisha wanayoishi watanzania. Na kama ullikuwa unafuatilia bunge lililopita naomba unipe mfano mmoja tu wa kiongozi/mbunge aliyetetea maslahi ya wananchi zaidi ya dr Slaa, hapa tuweke vyama pembeni kwanza naomba unipe uwezo wao binafsi
Najua wewe ni mpenzi wa CDM,Ndio maana unasahau hata kuwakataza watu wanaoleta ukabila( yaani wanaotumia Ukwere) kama ndio unaoharibu nchi, hili naomba mrekebishane mkimtaja JK haina haja ya kuweka kabila lake.Mbona mkimtaja Slaa hamueki kabila lake?ok turudi kwenye mada yetu,kilichokufanya useme CCM wanasema msimchague Slaa kwasababu ni padre ninini?wakati unajua kua sio kweli. then Mbona umen'gaka sana uliposikia Mr.2 inamaana haumsuport waziri wako mtarajiwa?au kuna baadhi ya watu hauwakubali ndani ya chama chako?Ninaposema sioni wa kumchagua namaanisha Wagombea wote hawaonyeshi kua na nia ya kutuletea maaendeleo ndio maana wanahubiri Uchama kuliko Utaifa.Mara nimeibiwa kura mara nimechakachuliwa,hii hauoni kwamba ni uchu wa madaraka.Mfano zanzibar kila siku Maalim Seif alikua analalamika anaibiwa mbona baada ya kuahidiwa umakamu wa rais katulia?Tuachaneni na hoja za kitoto kama Hizo za udini sijui umefanyajefanyaje mara John mara musa sisi itatusaidia nini?(just wasting of Time),.turudi katika swali lako la Msingi na jibu lake ni kwamba sijaona mbunge hata mmoja aliyefanya jambo la kuwaletea maendeleo watu wake nilichokua nakiona kwa Slaa awali nilidhani anafanya kwa maslahi ya Taifa nikampenda lakini baadae nikagundua alikua anayafanya hayo kwa ajili ya kutaka Urais akanitoka kabisaaaa.hasa hiyo sera yake ya kuchakachuliwa na kutokumtambua rais,Huu ni upuuzi au wewe unaonaje?
 
Samahani ivuga naomba ulifute Hilo neno Rangi NYEUSi maana linakuonyesha kama wewe unasuport Racism maana hata hao watu weupe wana uozo kibao. sio waarabu wala wazungu.Tunachotakiwa kufanya ni kutafuta way out sio mineno miiiiiiiiiingi halafu point ni 10%.
 
Wanandugu nimekuja hapa, nikiwa nina masikitiko makubwa kabisa , nchi yetu na wananchi wake(sisi) ..mpaka sasa hivi najiuliza kwa nini tunaikumbatia ccm? kina mods naomba msije mkaifuta thread yangu kwa sababu ni mawazo yangu na sijaribu kumtukana mtu ila najaribu tu kuweka mambo wazi na kupasua jipu.
Ukiangalia waarabu nchi zao huwezi kuzifananisha na nchi kama Tanzania,sisi nchi yetu ni maskini sana kuanzia mjini hadi vijijini , nishawahi kufika Tunis na Cairo ni miji mizuri sana na huwezi hata siku moja kuifananisha na mji wowote wa Tanzania , pale tunis kuna treni ndogo ndogo (behewa moja) zinatumia umeme kwa hiyo suala la usafiri kwao sio tatizo ukikompare na sisi watoto wa ngozi nyeusi.
Lakini jamaa kwa vile yale maendeleo hayaendani na rasilimali zao walizo nazo wakaamua kujitoa mhanga na damu zao zikamwagika ili mradi tu regime ile iondoke, hawa waarabu wanafanana kabisa na sisi , tunisia walikuwa na rais wao kwa muda mrefu Egypt alikuwepo Mubaraki na Libya yuko Gaddafi lakini hawa viongozi wote wameshachokwa , nikirudi hapa kwetu kuna hili dude ccm, this regime should end now.
Kwa sababu hawa jamaa wanatudanganya wanatudharau na wanatubeza na wanataka kutugawanya kiudini. mimi nina jiuliza kwa nini hatutaki kuwatoa hawa jamaa? au akili zetu ni fupi? kitu gani wameturidhisha nacho? watu wanapenda tu madaraka na hawapendi kuwajibika , hakuna anayetaka kuresign hata kama amefanya kosa linalomtaka yeye awajibike. so what to do? uwoga jamani utatuua na tutaendelea kubaki maskini hivi hivi!! maisha tunayoishi hayaendani hata kidogo na nishati ambazo tunazo au amabazo tunazalisha nchi kama Tanzania asilimia ya wananchi wake wanaotumia umeme haizidi 20%.. na ndani ya hao watu ishirini huwezi kuwapatia umeme wa uhakika. this aint joke anymore na hii inamaanisha kuwa wewe hiyo nafasi uliyopo haikufai na sio yako. I guess JK pale alipo kawekwa na hana sauti yoyote thats why hawezi kufanya maamuzi yoyote, na sisi watu kama hawa hawatufai katika karne hii.tuiondoe CCM

Ni kweli kabisa sisi na Waarabu hatuko sawa ktk maendeleo ya kiuchumi na kijamii ila tunatofauti ktk maendeleo ya Kisiasa ndio maana Nchi yetu inamfumo wa Kidemokrasia ya vyama vingi ambavyo Mabwana zetu wa Magharibi walitulazimisha kuufuata na hata bajeti za kugarimikia Uchaguzi huwa wanatupa hao Mabwana zetu!

Lakini kwa kuwa ni Wanafiki wanao linda maslahi yao ya kiuchumi hawakujali kama nchi za Kiarabu zinaendeshwa kiimla au kidikteta wao walijali mafuta na kulinda maslahi ya Israel!!!

Sasa ndugu yangu unapotushauri tufanye kama walivyofanya Waarabu kwa kuingoa Serikali ya CCM iliyoingia madarakani kwa kupitia Kura! nashindwa kukuweka ktk kundi gani sijui!!! huo sio uhaini? au uasi?

Au bado hamjamtambua Rais Kikwete ndie alieshinda uchaguzi wa 2010? sasa kama hamjamtambua mnaenda Bungeni kutafuta nini?
 
Back
Top Bottom