Tatizo ni ngozi nyeusi au uelewa mdogo? au ni elimu ndogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo ni ngozi nyeusi au uelewa mdogo? au ni elimu ndogo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Mar 5, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  Wanandugu nimekuja hapa, nikiwa nina masikitiko makubwa kabisa , nchi yetu na wananchi wake(sisi) ..mpaka sasa hivi najiuliza kwa nini tunaikumbatia ccm? kina mods naomba msije mkaifuta thread yangu kwa sababu ni mawazo yangu na sijaribu kumtukana mtu ila najaribu tu kuweka mambo wazi na kupasua jipu.
  Ukiangalia waarabu nchi zao huwezi kuzifananisha na nchi kama Tanzania,sisi nchi yetu ni maskini sana kuanzia mjini hadi vijijini , nishawahi kufika Tunis na Cairo ni miji mizuri sana na huwezi hata siku moja kuifananisha na mji wowote wa Tanzania , pale tunis kuna treni ndogo ndogo (behewa moja) zinatumia umeme kwa hiyo suala la usafiri kwao sio tatizo ukikompare na sisi watoto wa ngozi nyeusi.
  Lakini jamaa kwa vile yale maendeleo hayaendani na rasilimali zao walizo nazo wakaamua kujitoa mhanga na damu zao zikamwagika ili mradi tu regime ile iondoke, hawa waarabu wanafanana kabisa na sisi , tunisia walikuwa na rais wao kwa muda mrefu Egypt alikuwepo Mubaraki na Libya yuko Gaddafi lakini hawa viongozi wote wameshachokwa , nikirudi hapa kwetu kuna hili dude ccm, this regime should end now.
  Kwa sababu hawa jamaa wanatudanganya wanatudharau na wanatubeza na wanataka kutugawanya kiudini. mimi nina jiuliza kwa nini hatutaki kuwatoa hawa jamaa? au akili zetu ni fupi? kitu gani wameturidhisha nacho? watu wanapenda tu madaraka na hawapendi kuwajibika , hakuna anayetaka kuresign hata kama amefanya kosa linalomtaka yeye awajibike. so what to do? uwoga jamani utatuua na tutaendelea kubaki maskini hivi hivi!! maisha tunayoishi hayaendani hata kidogo na nishati ambazo tunazo au amabazo tunazalisha nchi kama Tanzania asilimia ya wananchi wake wanaotumia umeme haizidi 20%.. na ndani ya hao watu ishirini huwezi kuwapatia umeme wa uhakika. this aint joke anymore na hii inamaanisha kuwa wewe hiyo nafasi uliyopo haikufai na sio yako. I guess JK pale alipo kawekwa na hana sauti yoyote thats why hawezi kufanya maamuzi yoyote, na sisi watu kama hawa hawatufai katika karne hii.tuiondoe CCM
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu, naunga mkono hoja....
   
 3. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  naunga mkono hoja
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ila chichiem jamaaani aaaaaghhhhhhhhh
   
 5. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu Ivuga CCM wamehodhi kila kitu na hakuna uwezokano wa kuwatoa kwa sanduku la kura. Bila vita au nguvu ya umma hawata toka hawa watu. Wanatudharau na kurithishana uongozi wao na watoto wao. Lazima kitu cha ziada kifanyike kuwaondoa hawa wakoloni weusi. Namwomba Mungu anipe uhai niishi na niione siku watakapoondilewa madarakani hawa manyang'au CCM!
   
 6. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kunasiku nilimuuliza kada mmoja wa CCM, nini mafanikio ya CCM tangu imeanzishwa na kuwepo kwake madarakani hadi leo. Akanijibu, ni kuwepo kwake hadi sasa na bado kipo madarakani. Hivyo si rahisi kukubali kuachia madaraka ya kuongoza nchi kwa DEMOKRASIA tunayotamka mdomoni. Angalia walivyoliua BUNGE, sasa wenzao wamehamishia hoja zao nje ya BUNGE, wao wanasema ni wahaini. Kwahiyo JFPM Ivuga, tunakazi kubwa ya kuivunja hii NGAO YA MAFISADI.
   
 7. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Tatizo ni watanzania kuongea too much politik! Tumia muda wako ufanye kazi kwa bidii kijana.
   
 8. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,045
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Tatizo watanzania ni wabinafsi...kila mtu anajali raha zake hawakumbuki wengine..kwa kifupi watz wanapenda bia,wanawake na anasa zingine za kijinga ndo maana tunashindwa kufanya maamuzi magumu katika wakati mgumu.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  mkuu method, siwezi kukupinga hata kidogo, hapa hata wote tukihamia chama cha upinzani/vyama vya upinzani ccm hatutaitoa kwa kupitia sanduku la kura, naona tunapoteza mda tu na hela za kampeni,
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  sasa binti mkongwe hata nikifanya kazi kwa bidii zzote na hawa watu wanakata kodi kwenye mshahara wangu na wanaipeleka wapi? Kwa nini washindwe kuondoa hizi foleni na umeme wa uhakika?
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  hali naona imezidi kabisa, tunadharauliwa sana na wakubwa wetu.
   
 12. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  TATIZO NI UELEWA MDOGO, ELIMU NDOGO.
  Kila inapotajwa ngozi nyeusi kuwa kikwazo cha maendeleo huwa inaniuma sana kwani hii haiwezi kuwa sababu. Sababu ni uelewa mdogo na elimu ndogo.
  Uelewa mdogo kwa sababu Watanzania walio wengi ama hawamjui au hawataki kumjua adui yao. Baada ya miaka 50 ya utawala wa TANU/CCM, kila siku tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Mfano mdogo tu, miaka 50 bado hatuna ufumbuzi wa suala la umeme. Imani yangu hata CCM ikikaa madarakani miaka 50 mengine, tatizo hili hawatalitatua kwa sababu ya kukosa sera, mipango na vipaumbele vya maendeleo. Badala ya kutatua tatizo la kitaifa, CCM ilinunua ndege ya raisi na rada huku viongozi wa CCM wakiziba masikio vilio na maoni ya wananchi, na kufoka kwa kiburi kuwa "tutanunua hata kama itabidi Watanzania kula dongo".

  Elimu ndogo kwa sababu baada ya yote hayo, Watanzania tumeendelea kuichagua CCM katika uchaguzi mkuu uliopita. Kama tunalaumu uchakachuaji, tuelewe kuwa ni Watanzania wenyewe tuliliruhusu hili, kwa kukubali kwetu kuingia katika ushindani tukielewa kuwa "uwanja wa mchezo haukuwa na usawa" - Mwenyekiti wa vyama vya siasa, mkurugenzi mkuu wa uchaguzi, wasimamizi wakuu wa uchaguzi wilayani na mikoani, wote walichaguliwa na raisi tunayeshindana naye. Hapa unategemea nini? Ina maana gani baadaye kulalamika? Tungelikuwa na elimu ya kutosha, tusingekubali kwa mara nyengine tena kushiriki uchaguzi mkuu katika mazingira haya.

  Kama yote hayo hayatoshi, bado kilio changu ni kugawanyika kwa vyama vya upinzani. Nilishasema kabla na sitochoka kulisema hili, ikiwa vyama vya siasa vya upinzani zaidi ya kumi vyote vina dhamiri moja ya kuwatetea na kuwanasua Watanzania, kwa nini haviungani. Badala yake ni kushutumiana, udini, u-kanda, uitikadi. Mara huyu ni CCM B, huyu ni CCM C, huyu ni mkatoliki, huyu ni muislamu. Badala ya kuangalia maslahi ya Tanzania, kwanza tunataka kujua nani anatoka dini gani au mkoa gani. Hatuaminani, hatupendani. Kila mmoja anataka awe mkubwa yeye. Kama huu si ubinafsi ni nini?

  Tatizo si ngozi nyeusi bali roho nyeusi.
   
 13. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tunakujuwa wewe ni kipenzi cha January Makamba na CCM yao, nawe u-CCM damu.
   
 14. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni wale wote wanaoiona nchi ni yao peke yao.
   
 15. m

  maskin Member

  #15
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 76
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  mkuu najua inauma sana mtu anaposema kuwa rangi nyeusi ndo tatizo,lakini imagine africa tuna nchi 53 na zaidi,ukiangalia zile zenye watu weusi hasa toa waarabu ni matatizo na umaskini ,ukiangalia kuna nchi kama zimbabwe iliongozwa na mweupe ikapiga maendeleo kaja mtu mweusi kaivuruga na hataki hata kuwaachie wenzie waongeza mpaka afie hapo,africa kusini ilikuwa na mweupe sasa hivi kapewa mweusi mi naamini kabisa wape muda tu utaona uvundo watakao fanya hapo,sasa mimi sipendi kuhusisha rangi na hilo,ila ndo matusi tunayopewa na weupe ambao {tumewapa rasilimali zetu zote kimangungo} wakituangalia wanatuona kama hatuko smart, kwa sababu ya mazingaombwe tunayofanya,

  kuhusu kuunganisha vyama nalo mimi sio zuri sana kwa sababu mwishowe tutaungana na chama tawala utashangaa kuna chama kimoja tanzania wacha vyama vyenye kuwaelimisha wanachi vile vitakavyoshindwa basi vitajifia mbali kitu ambacho nacho sipendi ni ruzuku kwa vyama vya siasa nadhani imefika mahali sasa vyama vijitegemee vyenyewe na wanachama wachangie tu watu wanaanzisha vyama kama miradi tu.

  Mkuu haya ni mawazo yangu tu
   
 16. L

  Leornado JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ignorance is blissful.

  Mkuu mtoa mada, wewe angalu umepata exposure unaweza kucompare ni kiasi gani sisi bado ni maskini na hatudai haki zetu.

  Kumbuka asilimia 80 ya watanzania wanaishi vijijini hivyo hawajui nini maana ya maendeleo maana hawajawahi kuyaona.

  Kwao hadi leo hii maendeleo ni kujengewa kisima cha maji na CCM, kupewa trekta la kijiji, kujengewa kijidispensari.

  Hiyo mambo ya treni au miji mikubwa na mizuri kama Cairo chini ya serikali ya CCM ni ndoto.

  Kwa watanzania wengi umaskini wameuzoea na waoga kudai haki zao kwa viongozi.
   
 17. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu, ninakualiana na mawazo yako isipokuwa hilo la kuungana na chama tawala, angalau mimi niliposema kuungana nakusudia vyama vya upinzani tu. Jengine ninalokuunga mkono ni hili la watu kuanzisha vyama kama mitaji yao au NGO zao binafsi na sio kwa maslahi ya umma. Hilo la ruzuku pia lisingelipaswa kuwepo, kwa kuwa ni hela ya wavuja jasho bora ingekwenda kwa maendeleo na sio kulipia matumbo ya wachache.

  Mimi sijakata tamaa bado na Tanzania. Mabadiliko yatatokea lakini ni pole pole sana, kwa njia ya "Mageuzi" na wala sio kwa njia ya "Mapinduzi".
   
 18. Ibnu Ayoub

  Ibnu Ayoub Member

  #18
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tumuweke nani?, Kama kweli c.c.m ni wadini basi hawajui Dini, maana katika uislam ukiamua kuchukua uongozi kuwaongoza watu wa jamii mchanganyiko halafu unawapendelea Baadhi ujue hauna sifa ya kuingia peponi. naamini kwenye imani nyingine zote itakua ni hivyo. Binafsi sikijui chama chenye watu wengi wa dini Tofauti zaidi ya c.c.m. Nakubaliana na hoja zote lakini udini sijauona. we need change dat true but hawa wapinzani wote wananipa mashaka kama kweli wapo kwa maslahi ya Taifa kwanini wasiungane au wapo kimaslahi binafsi zaidi? waache umimi. am proud of my blackness na weusi sio Tatizo
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,467
  Trophy Points: 280
  umetumwa na ccm? sijui hata unajua unachokiongea ndugu yangu...wewe hujaona jinsi ccm wanavyotugawanya kidini? angalia hata uchaguzi uliopita angalia cuf walipata kura ngapi sehemu za pwani na angalia walipata kura ngapi sehemu za kilimanjaro na arusha huko? kwa nini?
   
 20. Mhafidhina

  Mhafidhina JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mi nafikiri ni vyote, Elimu na Uelewa mdogo...! Nitawaadisieni kisa kimoja halfu mtoe muone hali halisi ya uongozi tulionaoambao CCM imetupa.

  Hivi unajua hela tulizozipata baada ya kuuza mashirika ya umma zilifanyia nini? Zile hela badala ya kuziwekeza katika miundombinu na kuboresha usimamizi wa mashirika hayo, Serikali ya Mkapa iliamua kutumia hela hizo kwa ajili ya kununulia silaha (magari ya kivita pamoja na mabomu, na vifaa vingine vya kijeshi)...!

  Huu ni mfano kidogo tu, sasa kwa jambo kama hili unaweza ukaliiltaje? Ukosefu wa akili, elimu au ni wendawazimu? Hivi kweli unauza mashirika ya umma halafu unawekeza kwenye silaha?

  Kwa hali iliyopo sasa na mfumo CCM inaoujenga ni kwamba, madaraka ni "ULAJI" na sio "UWAJIBUKAJI". Ndio maana watu wanapoteuliwa UWaziri huwa ni kupongezana na kusheherekea...! Kila kukicha ni skendo za ufisadi na unadhirifu wa mali za umma lakini sijawahi kuona kiongozi hata mmoja ame resign au hata kuchukuliwa hatua...! On the account kwamba Kikwete anaogopa akichukuliwa hatua inaweza ikamrudi hapo baadae wakati amestaafu wanaweza wakamfanyia hivo hivo....!

  Hatuna vipimo au vigezo vya kuwapima viongozi wetu. Viongozi hawana ubunifu, mawazo yamekua mgando...! nafikiri kuna haja ya kuiondokana na CCM ili walau kutoa mwanya kwa wengine nao walete mawazo mapya na utendaji mpya.
   
Loading...