Tatizo ni Baba Mkwe

Tatizo ni Baba Mkwe

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
Ifuatayo ni sehemu ya shairi liloandikwa na Idd Ninga likijulikana kama tatizo ni baba mkwe ,unaweza kutoa maoni na ushauri wako.

1>tatizo ni baba mkwe,mke amenibania.
Sipendwi na wangu wakwe,wote wamenichunia.
Wameamua nifyekwe,mbali kunifutilia.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
2>ndoa yenyewe ni fupi,tena yakimkataba.
Kosa langu lipo wapo wapi,miaka kumi si haba.
Mrefu siyo mfupi,haba na haba kibaba.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
3>ukweli inaniuma,ila siwezi kusema.
Nikisusa ni lawama,ningejitoa mapema.
Nimefeli hii ngoma,kweli sina cha kusema.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
4>mke huyu mke gani,hajafunzwa unyagoni.
Nimwoe nimweke ndani,maji yafike shingoni.
Bora niwache njiani,hata kama nahuzuni.
Kuposa nipose mimi,mke apewe mwingine.
5>bora ndoa niizime,harusi nihairishe.
Vyema mimi nikalime,koo nisihatarishe.
Matunda nikayachume,acha wanikaribishe.
Tatizo ni baba mkwe,kupenda posa nyingine.
Shairi=TATIZO NI BABA MKWE.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
 
Last edited by a moderator:
Shairi zuri wamalenga, limekaa vyema kwa ustadi mzuri pasi na shaka.
 
Sasa mkuu. Japo wewe ni wa Tengeru Arusha lakini nakusalimia kwa Kirangi ... joole, vasinga ni nkasu vare?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom