KERO Tatizo Malipo Tiketi SGR Kupitia M-Pesa

KERO Tatizo Malipo Tiketi SGR Kupitia M-Pesa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mnamo tarehe 24 July 2026, mimi na mfanyakazi mwenzangu tulifanya malipo ya tiketi za SGR kupitia M-Pesa kwa kutumia control number tulizopewa.

Fedha ziliondolewa kwenye akaunti zetu, lakini malipo hayakuwasilishwa kwa SGR.

Tulipowasiliana na SGR, walituambia control number zilikuwa bado hazijaonesha malipo lakini tulipowasiliana na Vodacom, walitueleza kuwa kulikuwa na hitilafu kwenye mfumo wa malipo ya Serikali na kutushauri tusubiri hadi saa 72.

Kwa bahati mbaya, kabla tatizo halijatatuliwa, control number zilikwisha muda wake na nafasi tulizokuwa tumepanga kusafiria zikanunuliwa na abiria wengine.

Baadaye Vodacom walitujulisha kuwa malipo yalikuwa yamekamilika, lakini SGR walieleza kuwa control number zilikuwa tayari zimeisha muda wake na haziwezi kutumika tena. Hatimaye tulilazimika kununua tiketi nyingine kwa kutumia njia tofauti za malipo.

Lengo la ujumbe huu si kudai fedha zetu pekee, bali kuomba taasisi husika ziboreshe mfumo ili changamoto kama hii isiwakute wateja wengine.

Ingekuwa vyema kuwe na utaratibu wa kurejesha fedha pale hitilafu za mfumo zinapotokea, au kuruhusu fedha hizo kutumika kulipia safari nyingine badala ya mteja kupata hasara kutokana na tatizo ambalo halikusababishwa naye.
 
Back
Top Bottom