Tatizo liko wapi hapa kwetu

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
5,262
12,835
SIASA ZA MSIKITI UINGEREZA
Nimeishi Uingereza kwenye mji mmoja unaitwa Cardiff ambao ni mji mdogo ulioko Wales na kwa kawaida kwa Waingereza watu wa Wales wanadharaulika wanaonekana washamba.

Neil Kinnock alipata kugombea kutaka kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza na yeye ni Mwelshi.

Siku moja kaingia mwalimu wetu mmoja yeye ni kutoka England anaitwa Brown Thomas akamsema kwa ubaya sana Kinnock, ‘’Ati na huyu nae anataka kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza. Nani atampigia kura Mwelish?’’

Kwa sababu hii na dharau hii mimi nilipokwenda kupiga kura nilimpigia Neil Kinnock wa Labour Party lakini hakushinda aliyeshinda alikuwa John Major wa Conservative.

Najua msomaji wangu unashangaa vipi huyu mtu kutoka Kariakoo apige kura Uingereza?

Naam nimepiga kura. Uingereza sheria yao ni kuwa ukiwa ni mlipaji kodi haijaslishi kama ni mwananchi au mgeni unaweza kupiga kura.

Mbunge wangu mgombea alinifata nyumbani kwangu Column Road kwa adabu zote kuomba kura yangu.

Msikiti wa mtaani kwangu ni jengo ambalo hapo zamani lilikuwa kanisa lakini kwa kuwa watu walikuwa hawaendi kuabudu Wakristo wa sehemu ile wakaamua kuliweka gazetini kutangaza kuuza kanisa lao.

Hapo wakatokea Waislam wakalinunua kanisa lile na kuligeuza kuwa msikiti.

Hivi ndivyo ilivyotokea kwa msikiti huu Darul Isra kuwa katikati ya makazi ambayo wengi wa wakazi ni Wakristo.

Kwa muda wote nilioishi eneo lile sikupata kuhisi uadui wowote kutoka kwa hawa Waingereza kuwa walikuwa na chuki na msikiti ule.

Tatizo lilikuwa moja tu.

Barabara ya kuingia msikitini ilikuwa inakataza kuegesha magari kwa sababu ya ufinyu wa barabara.

Siku ya Ijumaa wanafunzi wengi wanakuja msikitini kwa ajili ya sala ya Ijumaa na baadhi yao ni vijana wanafunzi kutoka ncbi za Kiarabu ni wanafunzi lakini wana magari mazuri tu na lazima waje na magari yao na watayaegesha hapa mtaani na trafiki watakuja na kuweka tiketi.

Hawajali fedha wanazo wanalipa faini.

Ikatokea baada ya kurudi Tanzania nilirudi tena Cardiff nikitokea London na nikaenda Darul Isra msikitini kwangu kwa zaamani.

Safari hii nikapewa habari nyingine ya kufurahisha kuwa msikiti ule umenunua kanisa lingine na kuna mpango wa kulikarabati kuligeuza msikiti lakini kwa wakati ule lile kanisa wakilitumia kama bohari ya kuwekea vitu.

Nimekwenda Tilbury Port huu ni mji nje ya London na ni bandari.

Siku za nyuma bandari hii ilikuwa na biashara kubwa lakini wakati wa Magret Thatcher uchumi ulibadilika na bandari hii ikapoteza umuhimu wake.

Wengi wa wakazi wa mji ule mdogo walikuwa wafanyakazi wa bandari na baada ya bandari kukosa biashara na kazi kuwa haba wafanyakazi wengi walipoteza ajira kwa hiyo wakahama mji.

Niliingia Tilbury mchana kwa treni.

Nilipata mshtuko mkubwa sana.

Mji mzima hakuna mtu anaeonekana barabarani wala gari kupita.

Maduka ya mtaa mzima mkubwa wenyewe wanaita ‘’High Street,’’ yamefungwa lakini matangazo yapo yakitangaza biashara tofauti.

Unatembea barabarani unasikia sauti ya kiatu chako kinapogonga lami ya barabara.

Tilbury ni ‘’ghost town,’’ mji uliohamwa na katika maisha yangu yote sijapatapo kuona kitu kama hiki.

Inabidi wenyeji waliobakia wakuelekeze mahali ambapo unaweza kwenda kula chakula sehemu inaitwa Stella Maris, hii ni mfano wa huku kwetu wa Mission to Seaman sehemu ambayo zimewekwa maalum kwa kuwahudumia mabaharia kwa malazi na chakula.

Eid Kubwa imenikuta katika mji huu na hakuna msikiti lakini nimefahamishwa kuwa Waislam wapo ingawa hawana msikiti.

Wenyeji wakanieleza kuwa katikati ya mji kuna shule ya msingi ambayo hapo ndiyo Sala ya Eid huswaliwa ndani ya darasa.

Hapo ndipo niliposwali Sala ya Eid na wengi wa Waislam walikuwa Wahindi.

Miaka mingi ikapita siku moja nikajikuta niko Maryland, Washington DC Amerika na Ijumaa imefika.

Mwenyeji wangu Dr. Harith Ghassany akanichukua twende kusali.

Haikunipitikia kuwa sehemu ile hakuna msikiti na hivyo ndivyo ilivyokuwa.

Hapakuwa na msikiti.

Dr. Ghassany alinichukua John Hopkins University na tuliswali ndani ya moja ya madarasa ya chuo hicho.

Tanzania nchi ambayo Waislam ni umma mkubwa kuna chuki dhidi ya Uislam kupelekea kuvunjwa misikiti...

Swali la kujiuliza ni nchi yetu nani kaifikisha hapa?
Nini chanzo cha uadui huu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWA KWELI. DINI SIYO CHUKI. SISITUNACHUKIANA KWA SABABU UJINGA NA UELEWA WETU MDOGO KATIKA MAMBO YA IMANI NA ELIMU YA DUNIANI. DINI NI UPENDO KAMA UBINADAMU ULIVYO UPENDO NA MUNGU ALIVYO PENDO.
 
Back
Top Bottom