Tatizo la waamuzi Africa limekosa tiba au ni udhaifu wa CAF

Chuki dhidi ya simba ni kubwa sana kwa Tanzania ni kubwa sana bora tutolewe tu watu wapate amani maana vita kila kona mpaka unahisi watu kama kuna deni vile wanaidai simba .
Uiona offside ya leo? toa povu lako sasa
 
Najaribu kuwaza hawa waamuzi wanao chezesha michuano iliyo chini ya CAF wana matatizo gani ? ni kwamba hawana uelewa, wanafanya makusudi au kuna sheria za mpira ambazo zipo Africa kwingine hazipo?
Mifano ya mechi zilizo leta utata zipo nyingi hapa nita ainisha chache
1. Mechi ya kufuzu world cup kati ya Ghana na South Africa penalty ya utata
2. Finali ya Champions league 2019 kati ya Wydad Casablanca na Esperance de Tunis ( mechi ilivunjika kwa utata waemaamuzi)
3. Mechi ya Tunisia na Mali kwenye mashindano ya AFCON 2022
4. Mechi ya Al Ahl na Raja Casablanca hii ya juzi ajabu ni kwamba referee alienda kuangalia kwenye VAR na inaonyesha wazi mpira uligusa goti sio mkono bado referee akaweka tuta
5. Mechi ya Simba na Orando sikujua kwanini referee hakuenda kujiridhisha kwenye VAR
6. Mechi ya Asec Memosa na USGN kuna penalty ilitowewa mpka unae tazama unaona aibu.
Hizo ni baadhi ya mifano they are too many to mention, swali ambalo najiuliza kwamba CAF ni taasisi dhaifu imeshindwa kuondoa huu uozo kwani hatuoni kama hausaidii lolote ndio maana team zetu zikienda level ya mashindano ambayo fair play ipo tuna kwama mfano klabu bingwa dunia na world cup
Nb. Sijataka kuongelea waamuzi wetu wa TFF hawa wamekisha shindikana
Acha kulia wewe; yule refa wa leo kutoka Seychells alimiliki mpira ule vizuri sana. Kuna wakati wachezaji wenyewe ndio wanataka kuharibu mchezo; kwa mfano pamoja na mchezo mzuri alioonyesha kwa kuzuia mikwaju mingi ikiwemo na penalt moja, kuna wakati Manula alivuruga mchezo kwa kujilaza sana chini kupoteza muda mara kwa mara, na ilipofika dakika za majeruhi akafanya hivyo tena kwa karibu dakika tatu hali iliyosbabisha apewe kadi.
 
akili yako imejaa upuuzi.

ulijifichia kwenye kimvuli cha mchicha br ......na ndo maana since day one nlikuumbua na Leo umedhihirisha rasmi.

ww n "mee" br
Hayo baki nayo mwenyewe ila najua una maumivu makali sana
 
Acha kulia wewe; yule refa wa leo kutoka Seychells alimiliki mpira ule vizuri sana. Kuna wakati wachezaji wenyewe ndio wanataka kuharibu mchezo; kwa mfano pamoja na mchezo mzuri alioonyesha kwa kuzuia mikwaju mingi ikiwemo na penalt moja, kuna wakati Manula alivuruga mchezo kwa kujilaza sana chini kupoteza muda mara kwa mara, na ilipofika dakika za majeruhi akafanya hivyo tena kwa karibu dakika tatu hali iliyosbabisha apewe kadi.
.
 
Tusemeni ukweli tuu, Afcon ya mwaka huu ilikua hovyo, waarabu wameonewa sana,,,fitina kama fitina 😁 kwanzia kwa egypt, Algeria, Comoro n.k
 
Back
Top Bottom