UTOPOLO KENGE SANA MNAWEWESEKA BADO NA KIPIGO KWA ORLANDO PIRATES,UMEZUNGUKA WE KUMBE UNATAFUTA MECHI YA ORLANDO,VP MBONA UMESAHAU PENATI YA MCHONGO YA YANGA YA KUSAWAZISHA DHIDI YA VIJANA WA GEITANajaribu kuwaza hawa waamuzi wanao chezesha michuano iliyo chini ya CAF wana matatizo gani ? ni kwamba hawana uelewa, wanafanya makusudi au kuna sheria za mpira ambazo zipo Africa kwingine hazipo?
Mifano ya mechi zilizo leta utata zipo nyingi hapa nita ainisha chache
1. Mechi ya kufuzu world cup kati ya Ghana na South Africa penalty ya utata
2. Finali ya Champions league 2019 kati ya Wydad Casablanca na Esperance de Tunis ( mechi ilivunjika kwa utata waemaamuzi)
3. Mechi ya Tunisia na Mali kwenye mashindano ya AFCON 2022
4. Mechi ya Al Ahl na Raja Casablanca hii ya juzi ajabu ni kwamba referee alienda kuangalia kwenye VAR na inaonyesha wazi mpira uligusa goti sio mkono bado referee akaweka tuta
5. Mechi ya Simba na Orando sikujua kwanini referee hakuenda kujiridhisha kwenye VAR
6. Mechi ya Asec Memosa na USGN kuna penalty ilitowewa mpka unae tazama unaona aibu.
Hizo ni baadhi ya mifano they are too many to mention, swali ambalo najiuliza kwamba CAF ni taasisi dhaifu imeshindwa kuondoa huu uozo kwani hatuoni kama hausaidii lolote ndio maana team zetu zikienda level ya mashindano ambayo fair play ipo tuna kwama mfano klabu bingwa dunia na world cup
Nb. Sijataka kuongelea waamuzi wetu wa TFF hawa wamekisha shindikana