Tatizo la vyeti feki kama sio siasa basi

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,176
2,000
Inaelekea kusahaulika midomoni na vichwani mwa wengi. Ni majuma, miezi sasa inakatika tangu vyeti vikaribie kututoa roho. Tulitoka jasho kuviwasilisha kwa waajili na wao kusimamia zoezi la uhakiki.

Kwa kweli uhakiki ulienda vizuri, ingawa kuna usemi unatanabahisha kwamba kesi ya nyani ukimpekea fisi unategemea nini. Maafisa utumishi walisimamia ukahiki lakini wapo baadhi walicheza mchezo. Hivi kwa nini majina ya watu yafanane na wote wanafanya kituo kimoja? Hivi kwa nini watumishi wawili watumie cheti kimoja.. na afisa huyu alikuwa anafanyakazi hapo..achilia mbali ufeki wa cheti..hapa tunazungumzia utata unaonekana kutilia shaka..

Ni sawa baraza wamehakiki na kugundua magamba mengine si yao..Hao maafisa watapeta hivihivi? Hawa jamaa walikuwa kama miungu watu. Tena walizoea sana kutukana watumishi manesi na walimu huwaogopa sana HROs..Inawezekana walikuwa wakali ili mtumishi asione wizi na utapeli wa aina mbalimbali...Niongeapo hapa wapo wanaolia kwa kukosa mishahara tu kwa sababu wpuuzi majing HRO wameratibu ujinga

Kuna nyuzi zimeenea JF kuulizia majawabu ya rufaa, ama uhakiki uliofanywa chini ya utumishi na baraza...lakini maafisa utumishi walio ratibu vitendo viovu na kusababisha usumbufu wasiachwe. Hata kama wamestaafu wamehama nk.

Baraza wamekuwa makini sana..walikataa kumuhudumia mtumishi aliyetaka rufaa bila barua ya utumishi, na utumishi walitaka barua ya mwajili. hii imekaa vizuri sana.. Hapa mwizi utamkamata tu.

Hongerni sana. Utumishi na Baraza la mitihani lakini fanyeni haraka na ama kwa uhakika kutoa mrejesho

Asanteni...wale wa kumwaga mapovu karibuni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom