FUTURE HUNTER
JF-Expert Member
- Apr 30, 2018
- 2,026
- 2,608
Wanajukwaa poleni na majukumu.
Mimi niende moja kwa moja kwenye mada yangu hapo juu.Tangu nianze kukua na kuijua siasa imekuwa bahati nzuri nimekuta vyama vingi ndio vipo hot kweli kweli hivyo nimeona chaguzi kadhaa namna hali inavyokuwa haswa baada ya kupiga kura.
Kumekuwa na wimbi kubwa sana la vyama vya upinzani kulalamika kudhurumiwa matokeo yao halisi(haswa wabunge na madiwani) katika majimbo mbali mbali.
Mfano nakumbuka mwaka 2015 sehemu nyingi sana akishinda mpinzani ilikuwa ni kwa utata sana mpaka atangazwe mshindi tofauti na pale anaposhinda mtu wa chama dola.
Njoo kwa haya tuliyoyaona k/ndoni ya box la kura kutoka nje ya kituo na kurudishwa baadae,kunyimwa barua za wasimamizi, au kukataa kupokea fomu za wagombea toka upinzani.
Lakini juu ya hili mara nyingi vyama vya upinzani huhimiza raia kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura kipindi cha chaguzi lakini wakishapiga kura naona kabisa vyama havina namna ya kuzilinda kura hizi ili haki itendeke.Wananchi wanabaki wanalishwa matumaini feki tu.(Nakumbuka huyu edo 2015 alisema pigeni kura kwa wingi kuhusu kuiba ondoeni shaka) lakini mwisho wa siku bado vyama vinaangukia pua.
Kwa kuhitimisha,Je imekosekana njia sahihi kutoka vyama pinzani kulinda kura za wanyonge baada ya kutumbukizwa sandukuni?.Wenzetu nchi zingine wanafanyaje kuepuka hili?.
Maana naona kabisa kama haina haja ya kupiga kura maana inaonekana hata ikipigwa haiwezi amua nani mshindi isipokuwa chama kaisali.
Karibuni Kwa michango.
Sent using Jamii Forums mobile app