Dah! Taarifa za msiba zimekuwa nyingi sana. Kwanza naamini Watanzania wanakufa sababu ya uzembe na kujitakia wenyewe. Mtu anakufa kwa nimonia watu mnajazana msibani kwenda kuzika bila tahadhari yoyote unategemea nini hapo? Umeenda kuzika mara 3 je Disemba utaenda tena.
Mkoa wa Kilimanjaro wilaya zinazoongoza kwa misiba mpaka sasa
Rombo
Moshi (v)
Hai
Sina watu wa kunijuzi kuhusu wilaya nyingine
Nina marafiki kadha wengi sana wameshasafiri kwa ajili ya msiba wengine wamsafiri zaidi ya mara 3( kulingana na hali yake kiuchumi) safari zote kwenda kuzika.
Kulingana na marafiki walionizunguka mikoa hii inaongoza kwa vifo
1. Kilimanjaro
2. Arusha
3. Mbeya
4. Dar es Salaam
Je, kwa mujibu wa marafiki, ndugu na jamaa zako ni mikoa mingapi unapata ripoti nyingi za misiba?
Tuchukue tahadhari, tuache mzaha