Tatizo la umeme halitakuja liishe


Ni kweli.

Na hii ya kila mtendaji mkuu wa taasisi iliyo chini ya Setikali kuteuliwa na Rais, imesababisha kuzaliwa kwa machawa wengi, na kuwa na watendaji ambao akili na uwezo hakuna kabisa. Kuna baadhi unaongea nao masuala ya kitaalam mpaka unakata tamaa kabisa! Maana unamwona ni mtupu wa ajabu, hata huelewi amekuwaje hapo mtu asiyejua chochote kwa kiwango hicho.
 
Umemaliza kila kitu.
Nchi yetu kwa sehemu kubwa inaongozwa na watu wasio na uwezo kwa sababu tu wao ndo vimbelembele, wanoko na machawa.


Watu wenye uwezo na maono ya kweli katika nchi hii wanapigwa sana vita na kamwe hawapewi nafasi na hata wakipewa nafasi wanapingwa sana na siku ya mwisho kutolewa kwenye nafasi zao kwa majungu, chuki na wivu.

Nchi hii itapona siku tukiwa na watu sahihi kwenye maeneo sahihi na hili litawezekana pale tu utaalam utakapopewa nguvu juu ya siasa kupitita Katiba
 
* Ili kupata maendeleo vinahitajika:
1. Ardhi ✅
2. Watu ✅
3. Sasa safi ✖️
4. Uongozi Bora ✖️
  • Namba 3 ndio huzaa namba 4, vitu ambavyo ukiwa sirikalini na ukavipigia kelele ndg zako wanaweza omboleza mazishi yako haraka au uishi kama mzururaji.
  • Kwa jirani ili mtu apewe CEO wa shirika inafanyika vetting ya nguvu na mijadala nchi nzima; kwingine inapaswa kwanza uwe 'chawa', n.k. Je 'chawa' amewahi kuleta tija kwenye kaya yako?
 
Hoja iliyopo mezani ni tatizo la umeme linaloendelea kila siku nchini, na huku chanzo chake kikiwa ni kukosekana na watu wenye sifa sahihi za kuweza kupewa dhamana katika uongozi na utendaji. Sasa wewe Lucas unadandia tu treni kwa mbele, na kisha kuingiza uchawa wako ili kuonyesha mahaba yako kwa rais na serikali hata kama inaboronga.

Ukiona "constructive critism" imeelekezwa kwa serikali, basi wakati mwingine pita hata kimya kimya pasipo kutia neno, ili upate madini kutoka kwa wachangiaji wengine. Maisha ya uchawa ni sawa kabisa na biashara ya udangaji. Tambua tu kuwa unajiuza kwa bei rahisi mno.
 
Kilimo ambacho hakina tija?? Ambacho hakijawahi kumkomboa mkulima??

AFYA: Wingi wa majengo ambayo mnayaita vituo vya afya, visivyokua na wataalamu wa kutosha? Visivyokua na vifaa Tiba? Kila siku visivyokua na dawa, ikiwemo ujue Ni paracetamol, tofauti na hapo unashauriwa kanunue pharmacy.

ELIMU: Hapa nako Ni mitihani mitupu Mwenyezimungu awasamehe, mishahara kidogo kwa waalimu, Kila siku wanatuomba tuwakopeshe pesa, na kwa taarifa yako, waathirika wakubwa wa mikopo kausha damu Ni waalimu, tunawaona Kila siku wanavyodhalilika na madeni, hawana nyumba za kuishi, Bora wenzao polisi wanapewa pesa ya pango. Wao Kila siku Ni kilio, shida shida. Kwa mangi mwalimu Ana daftari la kukopea, kila mwisho wa Mwezi analipa Deni na kuanza Deni upya. Sizungumzui ubovu wa miundombinu, madarasa, meza na madawati, shule hazina ofisi za waalimu, Sera mbovu za ELIMU nk.

Kikubwa mlichobakiwa nacho Ni kusifiasifia tu na kusema anaupiga mwingi.

Nikukumbushe kuandika namba yako ya simu, Mana mikeka inatoka wewe huonekani
 
Nchi hii ina tatizo la Ujinga kwa wananchi wake katika kiwango cha kutisha sana.

Na bahati mbaya kupitia huo ujinga wa wananchi ndo tunapata Viongozi wajinga wasiojali kesho ya Taifa bali kesho ya mifuko yao na familia zao.

Amini maneno yangu. Ukiwachukua CEO's wote wa mashirika ya Umma, Mawaziri na Makatibu wakuu wote pamoja na Viongozi wote wakuu wa nchi hii ukiwauliza unaionaje Tanzania in the next 50 or 100 years unaweza pewa majibu ya ajabu hadi ukajuta kuzaliwa mwafrika na Mtanzania.

Kwa kifupi nchi hii u hovyo ndo umetawala kila mahali na tunaenda kwa kudra za MwenyeziMungu tu.

Itahitaji kuwa na watu based on merit wanaolindwa kikatiba inayoogopwa na kuheshimiwa na Wanasiasa na Wananchi wote ili nchi yetu iweze kupiga hatua sahihi za kimaendeleo na sio ngonjera tulizonazo sasa
 
Kuna mitambo fulani naona imeharibika inabidi inunuliwe mpya ifungwe 😄
Au kuna system imezingua kwa hiyo inahitajika bilion 10 kuboresha system mpya 😄

Kwa kwa kwa

Ova
Umeme umekatika Nchi Nzima au Sehemu kubwa ya Nchi !
Bilioni 10 ni pesa ndogo hiyo !
Wengine huwa wanaiita hela ya mboga tu !!
 
Changamoto zipo na hata hizo unazosema hazipo ni kwa sababu tu saivi mikoa mingi hasa ya kusini mvua zinanyesha hivyo mabwawa ya umeme kujaa.

Umeshawahi kujiuliza tukipata ukame wa mwaka au miaka 2 hali yetu ya umeme itakuwaje? Tuna vyanzo vya uhakika vya umeme vya kutupa umeme kipindi nchi imepata majanga kama ukame kwa muda mrefu?

Kama hujaelewa hii ndo hoja ya mtoa mada. Nchi hii inatakiwa kuwapa nafasi watu wanaowaza na kufikiria namna hii.

Wewe hujiulizi kwa nini Kenya hapo wameanza kujenga umeme wa Nyuklia?

Hizi ndo akili zinazotakiwa katika maeneo yote ya uongozi katika nchi yetu. Watu wanaowaza mbele sio watu wanaopewa nafasi za juu kwa sababu tu chawa, anajipendekeza, anajua kukaripia watu, mnoko au anasali sana au anaswali sana. Huu ni ujinga na ili tupate maendeleo ya kweli lazima tutoke huko na watu wapate nafasi based on merit.
 

Kuweka naibu waziri mkuu kutuongezea gharama bure. Hii post ifutwe!
 
Katiba mpya bora ni muhimu sana !
 
Kuweka naibu waziri mkuu kutuongezea gharama bure. Hii post ifutwe!
Juzi eti analalamika yupo kwenye ziara alafu mkuu wa Taasisi ametuma mwakilishi.

Tuna viongozi wanaofikiri kuwa kwenye ziara yake anatakiwa kuambatana na wakuu wa Taasisi alafu hao wakuu wa Taasisi kazi zao za msingi waziache ili wakatembee tu na Waziri.

Huyu ndo anapewa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu alafu nchi mnawaza kabisa mtapata maendeleo ya uhakika.

Hii nchi ukiwa na akili piga zako kimya tu maana inatia hasira, huruma na kinyaa.
 
Katiba mpya bora ni muhimu sana !
Na hapa ndo mwanzo wa mabadiliko ya kweli . Ila mbaya zaidi Wanasiasa wameshaju hilo kuwa kabuli lao katika siasa zao za kujinufaisha na uzandiki ni Katiba Mpya inayoipa nguvu mifumo kuliko wao na matamko yao.

As long as nchi hii wanasiasa ndo kila kitu sahauni iyo Katiba mpya na kamwe msiitegemee kwa sababu mmewapa nguvu wenyewe wanasiasa kuliko wataalam kupitia mifumo imara inayowa control wanasiasa.
 
Hapa naandika reply simu yangu inachaji 12% na umeme hakuna tangu jana usiku
Huku kwetu na ratiba ya mgao huwa inatoka kabisa ya wiki wiki. Hata walipotangaza mgao kuisha, huku haujawaji kuisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…