HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO
TANGAZO LA KAZI
Halmashauri ya wilaya ya Rombo kwa kushirikiana na chama cha wanaume rijali Tanzania (CHAWARITA) inatangaza nafasi elfu saba na miatano (7500) za Maafisa Rijali (AR) watakaofanya kazi katika zoezi la uboreshaji wa ndoa rombo na kuiepusha wilaya kutokana na kizazi cha wakenya.
Muda wa Mkataba wa kazi ni mpaka ambapo kina swai Massawe Mushi na kina Mlacha watakapoacha kupiga kilaji na kuurudia urijali wao.
Sifa za Mwombaji
1. Awe ni Mtanzania mwenye umri usiozidi miaka 45 mwenye uzoefu katika masuala ya ndoa michepuko au fani inayofanana na hiyo.
2. Mwombaji aambatanishe CV akielezea uzoefu wake katika mapenzi na picha mbili (Passport size)
3. Waombaji ambao si wachagga watapewa kipaumbele.
4. Mwombaji asiwe mlevi maana rombo idadi ya bar na nyumba ni sawa.
5. Mwombaji aambatinishe nakala za vyeti vya magonjwa ya zinaa ikiwemo UKIMWI kutoka katika hospitali inayotambiliwa na serikali.
Mwisho wa kupokea Maombi ni tarehe 22/05/2015 saa SITA na NUSU usiku. Maombi yatumwe au kuletwa kwa:-
MKURUGENZI WA WILAYA,
HALMASHAURI YA WILAYA YA ROMBO,
S. L. P 3040,
KILIMANJARO.
eeeeeeh....
Na umachinga wangu nahamia, rombo tuu
Natumia fursa kihivo,
Hii itachangia kushuka kwa thamani ya Tshs. Tunafanya import mpaka ya hii kitu
Nahamia Rombo kikazi...
Nonesense. Wanawake kibao tena walioko kwenye ndoa wana mahusiano nje ya ndoa na wanaume wengine wakati hao wanaume wao wa ndoa hawajui hata harufu ya pombe. Naona Gazeti la Mwananchi linaanza kuwa kama magazeti ya udaku sasa.
Maana hapo wamekutana.
Maana haya wanawake wa huko kwenye mapenzi sio kabisaaa tasteless .
Ndio maana wameenda Kenya kuchukua vimeo wenzao.
Inaonekana eneo la Kenya mpakani na Rombo wanaume wake hawajaathirika na pombe. Kenya hili tatizo ni kubwa kuliko hata Tanzania. Kumbuka wanawake wa central kenya walipoamua kuwachapa hawa wanaume.Pombe haramu haziuzwi baa. viroba vinauzwa hata kwenye maduka ya kawaida. Hata wilaya ya hai ninakotoka hali ni mbaya. wanaume hasa vijana wa 20-30s wamepotelea kwenye pombe. wanalala nazo na kuamka nazo. kazi hawafanyi wanachukua vijimali vya nyumbani hata chakula cha watoto wanaenda kuuza wapate hela ya pombe. wanawake wakikosea wakaweka hela hovyo zinaibwa ili pombe ikanunuliwe. Viroba vimesambaa na kupata umaarufu kupita kawaida. mzigo wa maisha umewaelemea wanawake. huko hai wanadai sababu ni kuanguka kwa zao la kahawa ambapo kumewafanya wanaume wakose shughuli za kiuchumi za kufanya!?! arusha nako hivyo hivyo....maisha magumu yanafanya wanaume wapunguzie mawazo kwenye viroba, matokeo yake nguvu ya kuzaa na kufanya kazi inapotea.
Nimejionea hali ilivyo Rombo kupitia report maalum Itv, Hali ni mbaya akina mama wanalalamika hawapati huduma, uzalishaji mali kwa wanaume ni mdogo sana kwa sababu ya ulevi wa pombe za kienyeji!rai yangu vyombo husika vichukue hatua kali za kisheria dhidi ya hawa watengenezaji. Lasivyo hili ni janga.
ILA NIWAPONGEZE HAWA WACHAGGA!mwonekano wa hayo mazingira haufananii na hao walevi! Najiuliza ni nan wanaojenga huko vizuri namna hyo ilihali wenyeji ni pombe tuu