Tatizo la ulevi Rombo: Wanawake wakodi wanaume kutoka Kenya kufanya nao ngono

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasinim amejipalia makaa kwa kukanusha taarifa za wanaume wa jimbo hilo kupoteza nguvu za kufanya tendo la ndoa kutokana na ulevi. Pia kauli ya kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atumie nafasi yake kuhalalisha biashara ya pombe haramu ya gongo kwa madai kuwa inawaingizia kipato watu wa hali ya chini imelaaniwa. Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama, baadhi ya wasomi na wananchi, wamesema Selasini hajui ukweli wa tatizo hilo bali amekurupuka kulikanusha wakati liko wazi.

Baadhi ya viongozi wa dini wa Kanisa Katoliki jimboni humo, wamekiri wanawake kutopatiwa haki yao ya msingi kwa muda mrefu, huku idadi ya watoto ikipungua.

Juzi, Gama alifanya ziara katika Kijiji cha Kikelelwa kilichoathiriwa zaidi na tatizo hilo.

Katika ziara hiyo, wakazi wa eneo hilo walimlaumu mbunge wao kwa kuingiza siasa katika janga linalotafuna maisha ya watu wake.

“Wananchi wanakubali pombe hizo zinaharibu nguvu za kiume na wanawake wamekiri kuwa wanakaa miezi tisa bila kupewa huduma ya ndoa halafu kiongozi anasimama anasema ni uongo,” alisema Gama na kuwataka wananchi kutompa kura kiongozi anayetaka gongo ihalalishwe wakati tayari imeleta madhara makubwa katika familia nyingi jimboni humo.
 
jamani nyie mnaaowalaani hao kina mama kuchukua wakenya badala ya watz inabidi muelewe kwanza jiografia ya rombo ipoje..kimsingi rombo imepakana sana na ky wananchi wanaingiliana sana hasa kwny biashara kilimo nk.ukiwa rombo waweza kwenda kenya kwa kutembea kwa miguu tuu.hivyo watu ambao ni majirani kwa warombo ni ky...
 
bora wangekodi wasukuma huwa wanajua kupenda kuliko kuchukua wakenya wanaodundwa na wake zao
 
Habari ya kiongozi wa serikali kukiri kuwa wanaume wa Rombo hawawezi kuwatosheleza wake zao hadi kukodi ndume za Kenya inaonesha picha iko hivyo kwa Watanzania.Habari kama hiyo ikisomwa na watu wa nje hawawezi kuangalia wana Rombo tu!Watatuunganisha watanzania wote kuwa ni watu goi goi!Habari hii itawafurahisha sana wababe Kenya kwa kuwa tayari wanatudharau sana kwa mengi.Laiti kama maneno hayo yangesemwa na kiongozi wa Kenya,Uganda ama Rwanda,sidhani kama angeendelea kuwepo kwenye nafasi yake!Maana akisema DC ni serikali imesema!Ni aibu sana kwetu wanaume Watanzania!Kwani maisha yetu hayatofautiani sana sehemu nyingi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasinim amejipalia makaa kwa kukanusha taarifa za wanaume wa jimbo hilo kupoteza nguvu za kufanya tendo la ndoa kutokana na ulevi. Pia kauli ya kumtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atumie nafasi yake kuhalalisha biashara ya pombe haramu ya gongo kwa madai kuwa inawaingizia kipato watu wa hali ya chini imelaaniwa. Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Leonidas Gama, baadhi ya wasomi na wananchi, wamesema Selasini hajui ukweli wa tatizo hilo bali amekurupuka kulikanusha wakati liko wazi.

Baadhi ya viongozi wa dini wa Kanisa Katoliki jimboni humo, wamekiri wanawake kutopatiwa haki yao ya msingi kwa muda mrefu, huku idadi ya watoto ikipungua.

Juzi, Gama alifanya ziara katika Kijiji cha Kikelelwa kilichoathiriwa zaidi na tatizo hilo.

Katika ziara hiyo, wakazi wa eneo hilo walimlaumu mbunge wao kwa kuingiza siasa katika janga linalotafuna maisha ya watu wake.

“Wananchi wanakubali pombe hizo zinaharibu nguvu za kiume na wanawake wamekiri kuwa wanakaa miezi tisa bila kupewa huduma ya ndoa halafu kiongozi anasimama anasema ni uongo,” alisema Gama na kuwataka wananchi kutompa kura kiongozi anayetaka gongo ihalalishwe wakati tayari imeleta madhara makubwa katika familia nyingi jimboni humo.

kuwachukua watu wa wilaya nzima na kuwaweka ktk kapu moja siyo sahihi hata kidogo! kwanza ni utafiti gani wa kina uliofanyika? Rombo ina wanawake wannggapi na ni wangappi waliohojiwa? kama pombe zimeleta athari kiasi hicho katka wilaya hiyo hao viongozi akiwemo huyo mkuu wa wilaya ni hatua gani walizochukua kuondoa tatizo la utengenezaji na unywaji wa kupindukia wa pombe?
 
Siyo rombo pekee walevi wako nchi nzima. Sema huko nano wamepitiliza. Kama unaweza kupiga tungi hadi kusaha kama kuna mahitaji mengine yanakusubiri basi ni hatari sana.
 
Na kuna mgombea alisema angeshinda angehalalisha gongo. Mnalalamika nini? Leweni msaidiwe .Hata Mbunge wenu Selasini alijaribu kutetea uongo wakinamama wakamjia juu imebidi aufyate.
 
jaribu kusema ROMBO mara kumi kwa kurudia rudia haraka haraka ndio utaona yanayosemwa kwa kuhusu wanaume wa rombo si ya kweli na kwamba ni rijali haswa.
 
Wanawake wa rombo kuagiza wanaume kutoka kenya ili wafanye mapenzi ilhali kuna mamilioni ya wanaume rombo imetutia aibu wanaume wote hata tusio wachaga.hivi pombe inamfanya mwanaume ashindwe tendo la ndoa.AIBU WACHAGA.
 
Back
Top Bottom