Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Ufisadi ni matokeo ya kushindwa kwa mfumo wa Ubepari, na ni kutokana na kulazimisha kuusimika Ubepari katika Mazingira na Nyakati ambazo ni irrelevant to Ubepari!
Kipindi cha Uhujumu Uchumi wahalifu walitumia zaidi nguvu ya pesa na mamlaka kufanya wizi kwa umma,lakini leo hii fisadi anatumia sheria kufanya maovu yake! Ni sheria zilizotungwa na kusimamiwa na wao wenyewe mafisadi, system imeruhusu mimi kapuku nitasema nini?
Ni kweli Mkuu wangu Mwalimu, Ufisadi umekuwa imani, ni kasumba vichwani mwa zaidi ya z5% ya watz wote! Leo ukipata kazi TRA/boT, then ukae miezi 6 bila ya kununua gari, kujenga mahekalu ya ajabu, kutanua kwenye ma-casino wala kuongeza hata mke wa pili, watakucheka kila kona, wakidai 'UNACHEZEA BAHATI' Ndivyo tulivyo wabongo, si kazi ndogo kufuta upuuzi huu vichwani mwetu!
MAENDELEO NI HESABU, TUKAE CHINI KWANZA TUJIULIZE VIZURI!
Hiki kizazi hakiwezi hata kujiuliza kilikosea wapi maana hakijawahi kupatia.
Anaita sasa!
Hao wezi kama wangekuwa wameibia serikali ya Marekani, Japan, Canada au UK wangesalimika? Ukweli wa mambo hili suala zima ni mapungufu ya miundo ya taasisi za kijamii.
Kamwe wasingesalimika! Na ndio maana nimesema kuwa haya ni matokeo ya irrelevance ya capitalism katika Tz na Afrika kwa ujumla, na ndio maana Una-fail.
Hayo mapungufu ya Taasisi zetu za kijamii, ukiyatazama kwa undani utagundua sisi tulikuwa bado sana kukurupukia huu mfumo, TUNACHOFANYA NI KUTUMIKA TU NA MABEBERU! Sisi tumelazimishwa kuingia ngoma tusiyojua midundo yake, imebaki kurukaruka tu ngomani kama wachawi tusijue taratibu za midundo, TUMEKUWA KITUKO NA TUNATIA AIBU, WANATUCHEKA KWA HESHIMA YA KUWAVIMBISHA MATUMBO YAO! Ni Upumbavu tu!
Takataka ni kitu chochote kilichokaa mahali pasipostahili, Ubepari kwa Afrika ni takataka!
Anaita sasa!
Kuna ukweli wa kuwa tulikurupuka. Lakini hata wale viongozi wa mwanzo wa kiAfrika waliotaka kuongoza nchi zao kwa kuanzisha miundo mipya kama african socialism nao walishindwa.
Binadamu wakikaa pamoja kwa muda mrefu wanaanzisha utamaduni. Ni miaka zaidi ya 50 toka ya uhuru. Muda huu umeshaanza kujenga jamii na utamaduni. Masuala ya ufisadi na kutoheshimu vyombo vya kijamii yameanza kuwa ni utamaduni wa watanzania.