Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Nitaongea kwa ufupi sana!
Tatizo la kukomaa kwa umadhubuti mfumo wa Ufisadi na kukosekana Uwajibikaji ambao umeliletea Taifa letu hujuma na taswira chafu kuhusiana na Rushwa, Ujangili, Madawa ya Kulevya, ubadhilifu na matumizi mabaya fedha za umma, na hata kufumuka kwa deni la Taifa na kupungua au kukosekana kwa mahitaji muhimu kwa wananchi au kukosekana kwa mapato ya kodi kutokana na uzalishaji (misamaha ya kodi) si jambo la mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ndani ya serikali!
Jipu hili na uozo huu ni malezi imara na yenye lishe bora kutoka chama tawala CCM!
CCM haiwezi kujitenga na utovu wa nidhamu wa watendaji au Serikali yake!
Ni CCM ambayo kupitia vikao vyake iliridhia kuwapa uanachama hawa watu, ikaridhia kuwapa majukumu ya kuwa wawakilishi wake katika Serikali na hata kuwapa fedha ili wachaguliwe kuwa wawakilishi Bungeni na kisha kuunda Serikali kuu.
Mawaziri wote na watuhumiwa wote ni wanachama na viongozi wa CCM!
Matendo yao yasiyo na woga, yanaashiria wazi kuwa chama kinakubaliana na kuafiki kauli na matendo yao machafu, na kimetoa baraka!
Kama kweli CCM kama chama hakihusiki na kinataka kujitenga kutoka hii taswira ya udhaifu na kupenda hujuma, basi na iwavue na kuwafukuza uanachama watuhumiwa wote maana wanakitia doa chama!
Wala lisiwe suala la kusubiri eti kesi za mahakamani, au uchunguzi
Kuna miongozo na kanuni kebekebe za kuwezesha Maamuzi haya yafanyike bila shida wala wasiwasi!
Fukuza hawa watu, it is that simple!