Tatizo la Ufisadi na Kutowajibika ni CCM

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Nitaongea kwa ufupi sana!

Tatizo la kukomaa kwa umadhubuti mfumo wa Ufisadi na kukosekana Uwajibikaji ambao umeliletea Taifa letu hujuma na taswira chafu kuhusiana na Rushwa, Ujangili, Madawa ya Kulevya, ubadhilifu na matumizi mabaya fedha za umma, na hata kufumuka kwa deni la Taifa na kupungua au kukosekana kwa mahitaji muhimu kwa wananchi au kukosekana kwa mapato ya kodi kutokana na uzalishaji (misamaha ya kodi) si jambo la mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu ndani ya serikali!

Jipu hili na uozo huu ni malezi imara na yenye lishe bora kutoka chama tawala CCM!

CCM haiwezi kujitenga na utovu wa nidhamu wa watendaji au Serikali yake!

Ni CCM ambayo kupitia vikao vyake iliridhia kuwapa uanachama hawa watu, ikaridhia kuwapa majukumu ya kuwa wawakilishi wake katika Serikali na hata kuwapa fedha ili wachaguliwe kuwa wawakilishi Bungeni na kisha kuunda Serikali kuu.

Mawaziri wote na watuhumiwa wote ni wanachama na viongozi wa CCM!

Matendo yao yasiyo na woga, yanaashiria wazi kuwa chama kinakubaliana na kuafiki kauli na matendo yao machafu, na kimetoa baraka!

Kama kweli CCM kama chama hakihusiki na kinataka kujitenga kutoka hii taswira ya udhaifu na kupenda hujuma, basi na iwavue na kuwafukuza uanachama watuhumiwa wote maana wanakitia doa chama!

Wala lisiwe suala la kusubiri eti kesi za mahakamani, au uchunguzi

Kuna miongozo na kanuni kebekebe za kuwezesha Maamuzi haya yafanyike bila shida wala wasiwasi!

Fukuza hawa watu, it is that simple!
 
Na hasa uongozi wa CCM
Haiwezekani waziri aliyejiuzulu kwa kashfa ya vijisenti, huyo huyo apewe fursa ya kuandika katiba ya wananchi kwa utashi wake. Iliposemwa watavuliwa mgamba, CCM haikuweza kwasababu kundi linalotengeneza mfumo wa ufisadi ndilo limeweka viongozi madarakani.

Nilisikitika kuona mwenyekiti wa CCM akishirikiana na ''wahalifu' kuandika katiba ya nchi.
Tutarajie nini endapo unamkabidhi fisi kazi ya ulinzi wa bucha yako ya nyama!

Katika kujitenga kumetokea utamaduni wa kujiuzulu. Hilo ndilo suluhisho la matatizo ambalo CCM imetuletea.
Kwamba wezi wapewe likizo ya kwenda kudumbua kwa raha mustarehe.

Ni CCM hao, kwamba kujiuzulu kwao ndio utendaji bora.
 
Ufisadi ni kama DINI/IMANI, una chimbuko hadi kwenye ngazi ya mizizi. Huwezi kushughulikia ufisadi kwa kuondoa viongozi wachache wanaotajwa kuhusika halafu ukaridhika kuwa umemaliza kazi... Wakiondoka hawa watakuwa replaced na walafi wengine na ulaji utaendelea kama kawaida! Jiulize yale mapendekezo ya kamati ya Richmond kwa nini hayajatekelezwa yote mpaka hii leo? Kwa nini Mwakyembe alisema bungeni kwamba kuna mengine hawajayasema kwa kulinda heshima ya chama na serikali? Wana-CCM hawa wanataka kupambana na ufisadi lakini wakati huo huo wanataka kuilinda system/status quo iliyopo madarakani...HAIWEZEKANI!
CCM iko kwenye DENIAL kwamba ina tatizo kubwa linalohitaji tiba nzito... ni sawasawa na mzazi mwenye mtoto mvuta unga/kibaka na ameshindikana lakini bado anamlinda asishughulikiwe na dola, amepofushwa na mapenzi yake kwa mwanawe kiasi cha kutoangalia jinsi alivyoharibika! CCM hii haiwezi kujitibu ugonjwa huu sugu wakati bado iko madarakani ikifaidika na mfumo uliopo... mabadiliko ya kweli yanawezekana ndani ya CCM ikiwa nje ya utawala.
 
Ufisadi ni matokeo ya kushindwa kwa mfumo wa Ubepari, na ni kutokana na kulazimisha kuusimika Ubepari katika Mazingira na Nyakati ambazo ni irrelevant to Ubepari!

Kipindi cha Uhujumu Uchumi wahalifu walitumia zaidi nguvu ya pesa na mamlaka kufanya wizi kwa umma,lakini leo hii fisadi anatumia sheria kufanya maovu yake! Ni sheria zilizotungwa na kusimamiwa na wao wenyewe mafisadi, system imeruhusu mimi kapuku nitasema nini?

Ni kweli Mkuu wangu Mwalimu, Ufisadi umekuwa imani, ni kasumba vichwani mwa zaidi ya z5% ya watz wote! Leo ukipata kazi TRA/boT, then ukae miezi 6 bila ya kununua gari, kujenga mahekalu ya ajabu, kutanua kwenye ma-casino wala kuongeza hata mke wa pili, watakucheka kila kona, wakidai 'UNACHEZEA BAHATI' Ndivyo tulivyo wabongo, si kazi ndogo kufuta upuuzi huu vichwani mwetu!

MAENDELEO NI HESABU, TUKAE CHINI KWANZA TUJIULIZE VIZURI!
Hiki kizazi hakiwezi hata kujiuliza kilikosea wapi maana hakijawahi kupatia.
Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:

Hao wezi kama wangekuwa wameibia serikali ya Marekani, Japan, Canada au UK wangesalimika? Ukweli wa mambo hili suala zima ni mapungufu ya miundo ya taasisi za kijamii.
 
Hao wezi kama wangekuwa wameibia serikali ya Marekani, Japan, Canada au UK wangesalimika? Ukweli wa mambo hili suala zima ni mapungufu ya miundo ya taasisi za kijamii.

Kamwe wasingesalimika! Na ndio maana nimesema kuwa haya ni matokeo ya irrelevance ya capitalism katika Tz na Afrika kwa ujumla, na ndio maana Una-fail.

Hayo mapungufu ya Taasisi zetu za kijamii, ukiyatazama kwa undani utagundua sisi tulikuwa bado sana kukurupukia huu mfumo, TUNACHOFANYA NI KUTUMIKA TU NA MABEBERU! Sisi tumelazimishwa kuingia ngoma tusiyojua midundo yake, imebaki kurukaruka tu ngomani kama wachawi tusijue taratibu za midundo, TUMEKUWA KITUKO NA TUNATIA AIBU, WANATUCHEKA KWA HESHIMA YA KUWAVIMBISHA MATUMBO YAO! Ni Upumbavu tu!

Takataka ni kitu chochote kilichokaa mahali pasipostahili, Ubepari kwa Afrika ni takataka!

Kuna ukweli wa kuwa tulikurupuka. Lakini hata wale viongozi wa mwanzo wa kiAfrika waliotaka kuongoza nchi zao kwa kuanzisha miundo mipya kama african socialism nao walishindwa.

Binadamu wakikaa pamoja kwa muda mrefu wanaanzisha utamaduni. Ni miaka zaidi ya 50 toka ya uhuru. Muda huu umeshaanza kujenga jamii na utamaduni. Masuala ya ufisadi na kutoheshimu vyombo vya kijamii yameanza kuwa ni utamaduni wa watanzania.
 
Kushindwa kwa mfumo kunaweza kuwa kwa sababu nyingi, aidha ni incompetence ya viongozi au irrelevance ya mfumo wenyewe, n.k
Irrelevant system hata ikipata competent wasimamizi, utaanguka tu, lakini competent men wakipata relevant system daima utasimama!

Hakika Mkuu wangu, ufisadi umeshakoma kuwa sehemu utamaduni wetu, ni hatari. Je, unajua kilichosimika utamaduni huu kwenye fikra zetu? Ni kutosadifika kwa mfumo, ambako kuna-intertain negative nature ya binadamu, UBINAFSI/MIMI KWANZA.
Anaita sasa!
 
Bado CCM imeleta uozo kugombea nafasi za uongozi wa nchi na serikali. Chadema na Ukawa wamempokea "mlokole"
 
Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom