Tatizo la Mwanza ni mkurugenzi Kabwe na si CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tatizo la Mwanza ni mkurugenzi Kabwe na si CHADEMA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kisendi, Jul 8, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Meya wa Mwanza, Kutoka chadema ameanisha kuwa Mkurugenzi Kabwe anazidi kutumia na wanasiasa ili kuidhofisha Chadema. Hii ni baada ya kutokea vurugu za Mza kati ya Polisi na Machinga. Madiwani wa chadema wakiongozwa na meya wa jiji kutoka chadema walikaa chini na kukubaliana kuwa wamachinga wasifukuzwe kwanza kwenye maeneo mpaka itakapo bainika sehemu nzuri na yenye msongamano wa watu ili wamachinga waweze kuhamishwa. Lakini Mkurugenzi yeye kama yeye bila kufuata makubaliano ya madiwani aliomba waondolewe. Je serikali au CCM mimi binafsi naona kama wanakosa think tanker. Hapo CCM ijue inazid kujishusha.


  NIPASHE source
   
 2. A

  Anyambilile Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0  Ni kweli hapo kuna jambo limefichwa, baada ya lile tukio TBC waliongea na Naibu Waziri Mambo ya ndani, alichokuwa anaeleza ni kama Chadema Ndiyo wameamua kuwatoa wale wafanya biashara,

  "Serikali iliyoopo ni ya Chadema kwa hiyo hao ndiyo walio fanya maamuzi hayo" Hii ni Aibu.
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Uzuri ni kuwa wananchi wa kawaida hapa Mwanza wameisha lielewa hilo na njama za kuihusisha Chadema na vurugu hizo kama alivyosema Kagasheki haziwezi kufaulu zaidi ya kujishusha wao wenyewe CCM
   
 4. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hili suala linatakiwa lisichukuliwe wala kutumika kisiasa .. wahusika na hasa wanaosababisha hali hii kwa nni wasitolewe???
   
 5. msafiri.razaro

  msafiri.razaro JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 616
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Huyu KABWE yeye ni nani hasa mpaka afanye mambo kinyume cha wana Mwanza?. Tumechoka sasa kuwa na maamuzi ya mtu mmoja yakasababisha ndugu zetu kufa au kuumizwa. Imefika wakati sasa wananchi tuchukue maamuzi kwani kama vibaka wanachomwa moto kwa nini watu kama hawa? ambao ni zaidi ya vibaka tunawaachia wakiendelea kubaka demokrasia ya nchi yetu. Imefikia wakati sasa wafundishwa kuwaheshimu matakwa na umma kuliko matakwa na vibaraka wao.

  People's Power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...