Tatizo la mtoto kuvimba kitovu baada ya kukatwa vibaya

christmas

JF-Expert Member
Jul 21, 2011
2,703
1,277
Wakuu mwanangu ana miezi mitano tatizo ni kwamba kitovu chake kimevimba na nimejaribu kuuliza watu mbalimbali wanasema aliemkata hakumkata vizuri ndio mana. Wakuu naomba ushauri kwa yeyote anaefahamu dawa au hospitali ninayoweza kwenda na wakanisaidia. Shukrani
 
Pole sana mkuu christmas kwani nimehisi mwili kusisimuka sana , mpeleke hospital fasta mkuu. Hiyo ni hatari sana , usichezee kitovu hata siku moja hasa cha mtoto mchanga.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo ni kuwepo kwa hewa ndani yake
Tiba yake ni kumfungia sarafu yeyote itakayokifunika kitovu na uibandike na Plasta
kama keshakua na umri wa zaidi ya miaka 3 huwa kuna operation ndogo
 
Ukwaju ... najua unatoa ushuri kwa nia nzuri,. lakini hii ni imani POTOFU na ya hatari. Mara zote imesababisha madhara kwa mtoto badala ya kumsaidia. Ni jana tu nilikuwa namsaidi rafiki yangu ambaye mwanae ana tatizo hilo la kuvimba kitovu akamfunga sarafu (coin)... Coin ni metal na always ni chafu na inaweza ikasababisha itching (muwasho) eneo inapofungwa. Hii inapelekea kusababisha mchubuko na kwa kuwa ni chafu mchubuko unakuwa infected na kuwa donda kubwa...mtoto wa rafiki yangu kapatwa na hilo. ACHA KABISA KUSHAURI WATU HIVYO, INAATHIRI WATOTO. metals (coins/sarafu) zinaweza hata beba wadudu wa Tetanus ikawa msala!
 
Wakuu mwanangu ana miezi mitano tatizo ni kwamba kitovu chake kimevimba na nimejaribu kuuliza watu mbalimbali wanasema aliemkata hakumkata vizuri ndio mana. Wakuu naomba ushauri kwa yeyote anaefahamu dawa au hospitali ninayoweza kwenda na wakanisaidia. Shukrani

Kwa hakika mwanao ana tatizo linaitwa 'Umbilical Hernia', hili tatizo linasababishwa na defect (udhaifu) kwenye ukuta wa tumbo pale palipo kitovu, ukuta unakuwa haujafunga vizuri hivyo unaacha kakitundu (HAISABABISHWI NA KITOVU KUKATWA VIBAYA). Presha inapoongezeka tumboni (intra-abdominal pressure) basi kitovu kinavimba. Mara nyingi defect hii hujifunga yenyewe kadri mtoto akuavyo...lakini kama ni kubwa, inaweza isifunge na mtoto kubaki na kitovu kikubwa maisha yake yote. Mara nyigi tiba yake ni kwa operation (Umbilical Hernia repair) kufunga ile defect kwa kuioanisha vizuri misuli ya ukuta wa tumbo hapo kwenye kitovu. Lakini tiba hii ya operation si lazima, kwa sababu kitovu kuvimba hakina madhara yoyote. Mara chaache sana hutokea utumbo ukajifunga na kunasa ukipenya kwenye hiyo defect, hapo lazima operation ifanywe, lakini hili hutokea mara chache sana. Ushauri: USITHUBUTU KUMFUNGA MTOTO SARAFU/COIN. Peleka mtoto akaonwe na Paediatric Surgeon amchunguze na kuestimate ukubwa wa defect na kama inaweza leta hatari ya kuziba utumbo (intestinal obstruction) kisha atawashauri. Kama mtoto ni wa kike, basi anaweza hitaji tu kumfanyia operation for cosmetic purposes, kwa sababu itamsumbua ujanani kuvaa vitopu na hata kuwa confident akiwa na mpenzi wake faragha. Anaweza jisikia vibaya kuwa na kitovu kikubwa kiasi ikamuathiri kisaikolojia...watoto wa kiume mara nyingi hawamind.
 
Ilinitokea kwa Mtoto wangu last year nikashauriwa kumfunga sarafu ya shilingi 200, not other coin. But niliambiwa kusiwe na direct contact ya kitovu na coin. Nikafanya hivyo mtoto akapona na yuko poa hadi sasa. Aliyenipa ushauri ni very highly repected pediatrician.
 
Alipona sababu ya ukweli kwamba, watoto wengi wenye hilo tatizo hupona tu wenyewe kwa defect kujifunga...na sio kwamba coin ilimponyesha! Kisayansi..theres no association between tying a coin on umbilicus with closure of the defect! Hata Paediatrician gani akisema...may be alikuwa anawatibu nyie wazazi psychologically mtulie, but the fact is...coin haifungi hernia defect kwenye kitovu.
 
Okay mkuu siwezi kubisha zaidi kwa kuwa sina scientific evidence au data, just observations. By the way huenda huyo very highly respected pediatrician ni wewe mkuu Riwa then nikaanza kuleta maubishi unanichora tu...
 
Last edited by a moderator:
Ilinitokea kwa Mtoto wangu last year nikashauriwa kumfunga sarafu ya shilingi 200, not other coin. But niliambiwa kusiwe na direct contact ya kitovu na coin. Nikafanya hivyo mtoto akapona na yuko poa hadi sasa. Aliyenipa ushauri ni very highly repected pediatrician.
Hata wa kwangu alipona kwa kushauriwa na MaDr km Riwa na labda kwa kumshauri mtu yeyote atumie akili asiweke direct ile coin na mwili ni lazima aifunge vizuri na plasta ndio ambandike kwenye Kitovu
na sio kwamba coin ilimponyesha! Kisayansi..theres no association between tying a coin on umbilicus with closure of the defect! Hata Paediatrician gani akisema...may be alikuwa anawatibu nyie wazazi psychologically mtulie, but the fact is...coin haifungi hernia defect kwenye kitovu.
labda DR ruwa nikueleweshe kitovu hakitibiwi na Coin ya 200. nimesema mfano wake tu wa umbo hhata ukitumia kifungo kikubwa kinairudisha kitovu na sifichi ndio matibabu yanayotumika hapa Hospital ya mkoa
 
Last edited by a moderator:
Hata wa kwangu alipona kwa kushauriwa na MaDr km Riwa na labda kwa kumshauri mtu yeyote atumie akili asiweke direct ile coin na mwili ni lazima aifunge vizuri na plasta ndio ambandike kwenye Kitovu

labda DR ruwa nikueleweshe kitovu hakitibiwi na Coin ya 200. nimesema mfano wake tu wa umbo hhata ukitumia kifungo kikubwa kinairudisha kitovu na sifichi ndio matibabu yanayotumika hapa Hospital ya mkoa

Labda niseme tu kuwa...unapoapply pressure kwenye kitovu kilichovimba sababu ya hernia (umbilical hernia), yes kitarudi sababu utumbo ulioherniate utarudi back to abdominal cavity..lakini intra-abdominal pressure ikiongezeka, basi kitovu kitavimba tena tu..na ndio maana nasema kuapply pressure iwe kwa kufunga coin au kitu kingine, haitatibu umbulical hernia. Matibabu certain ni iwapo utafanyika upasuaji kuziba hiyo defect kwa kuvuta na kufunga misulu ta abdominal wall over the defected part. Nimefanya hizi operation nikifanya kazi Muhimbili idara ya upasuaji watoto chini ya walimu wangu marehemu Dr Sayi na Prof Carneiro. Coin haijawahi kusaidia, no evidence na hata kisayansi haimake sense.
 
Dr natoka nje ya mada kidogo mwanangu ana miezi minne' kende yake (pumbu) moja ni kubwa sana kuliko nyingine je hili ni tatizo?
 
Labda niseme tu kuwa...unapoapply pressure kwenye kitovu kilichovimba sababu ya hernia (umbilical hernia), yes kitarudi sababu utumbo ulioherniate utarudi back to abdominal cavity..lakini intra-abdominal pressure ikiongezeka, basi kitovu kitavimba tena tu..na ndio maana nasema kuapply pressure iwe kwa kufunga coin au kitu kingine, haitatibu umbulical hernia. Matibabu certain ni iwapo utafanyika upasuaji kuziba hiyo defect kwa kuvuta na kufunga misulu ta abdominal wall over the defected part. Nimefanya hizi operation nikifanya kazi Muhimbili idara ya upasuaji watoto chini ya walimu wangu marehemu Dr Sayi na Prof Carneiro. Coin haijawahi kusaidia, no evidence na hata kisayansi haimake sense.

Dr natoka nje ya mada kidogo' mwanangu ana miezi minne kende yake moja (pumbu) ni kubwa sana kuliko nyingine je hili ni tatizo?
 
Kwa hakika mwanao ana tatizo linaitwa 'Umbilical Hernia', hili tatizo linasababishwa na defect (udhaifu) kwenye ukuta wa tumbo pale palipo kitovu, ukuta unakuwa haujafunga vizuri hivyo unaacha kakitundu (HAISABABISHWI NA KITOVU KUKATWA VIBAYA). Presha inapoongezeka tumboni (intra-abdominal pressure) basi kitovu kinavimba. Mara nyingi defect hii hujifunga yenyewe kadri mtoto akuavyo...lakini kama ni kubwa, inaweza isifunge na mtoto kubaki na kitovu kikubwa maisha yake yote. Mara nyigi tiba yake ni kwa operation (Umbilical Hernia repair) kufunga ile defect kwa kuioanisha vizuri misuli ya ukuta wa tumbo hapo kwenye kitovu. Lakini tiba hii ya operation si lazima, kwa sababu kitovu kuvimba hakina madhara yoyote. Mara chaache sana hutokea utumbo ukajifunga na kunasa ukipenya kwenye hiyo defect, hapo lazima operation ifanywe, lakini hili hutokea mara chache sana. Ushauri: USITHUBUTU KUMFUNGA MTOTO SARAFU/COIN. Peleka mtoto akaonwe na Paediatric Surgeon amchunguze na kuestimate ukubwa wa defect na kama inaweza leta hatari ya kuziba utumbo (intestinal obstruction) kisha atawashauri. Kama mtoto ni wa kike, basi anaweza hitaji tu kumfanyia operation for cosmetic purposes, kwa sababu itamsumbua ujanani kuvaa vitopu na hata kuwa confident akiwa na mpenzi wake faragha. Anaweza jisikia vibaya kuwa na kitovu kikubwa kiasi ikamuathiri kisaikolojia...watoto wa kiume mara nyingi hawamind.

Nami nimejifunza mengi kwa maelezo yako, nilikuwaga sijui kwa nini watu wachache wanakuwa na vitovu vikubwa. Asante sana!
 
Dr natoka nje ya mada kidogo' mwanangu ana miezi minne kende yake moja (pumbu) ni kubwa sana kuliko nyingine je hili ni tatizo?
UKItaka Ubaya ... kwa mtoto wa miezi mi4 nachelea kusema kwamba ni tatizo. Sababu mara nyingi kende hutofautiana size, japo si sana. Kama zikitofautiana sana, sababu yaweza kuwa infection (kama mwanao ana dalili nyingine za infection kama swelling, pain, fever), au hydrocele (busha, kuna congenital hydrocele) ambayo si kende huvimba bali mfuko wa kende hujaa maji, na torsion/twisting ya kende wakati ikishuka during its development. Kama tofauti ni ndogo huna haja ya kuhofu, kama ni kubwa sna basi daktari amuone.
 
hizo dalili ulizozitaja hapo juu hana kabisa na mfuko wa kende haujajaa maji isipokuwa kende yenyewe ndo kubwa kuliko nyingine
 
Last edited by a moderator:
Salute to you Dr Riwa. kwetu hizi tunaziita hizi nyanga. Naona unakata nyanga tu.Elimu nzuri, nimejifunza kitu hapa
 
Last edited by a moderator:
Ilinitokea kwa Mtoto wangu last year nikashauriwa kumfunga sarafu ya shilingi 200, not other coin. But niliambiwa kusiwe na direct contact ya kitovu na coin. Nikafanya hivyo mtoto akapona na yuko poa hadi sasa. Aliyenipa ushauri ni very highly repected pediatrician.

Hata wa kwangu alipona kwa kushauriwa na MaDr km Riwa na labda kwa kumshauri mtu yeyote atumie akili asiweke direct ile coin na mwili ni lazima aifunge vizuri na plasta ndio ambandike kwenye Kitovu

labda DR ruwa nikueleweshe kitovu hakitibiwi na Coin ya 200. nimesema mfano wake tu wa umbo hhata ukitumia kifungo kikubwa kinairudisha kitovu na sifichi ndio matibabu yanayotumika hapa Hospital ya mkoa

Kwa maelezo niliyowahi kusikia na niliyosoma hapa, naamini coin ingesaidia ku-balance pressure ya nje ya kitovu dhidi ya pressure ya ndani wakati ukuta wa tumbo (pale palipo kitovu) ukiendelea kufunga. Hata hivyo, ushauri wa Riwa ni wa kuzingatiwa sana kwani kwa hakika madhara yanaweza kuwa makubwa.

Kuhusu kuzungushia plasta kwenye coin, daktari mmoja wa watoto bado alikataa utaratibu huu japo coin imezungushiwa plasta. Hata hivyo, alitoa njia mbadala akipendekeza kumvisha mtoto kaptula au bukta yenye mkanda mpana utakaofunika kitovu.

Ndugu christmas ni vyema ukampeleka mtoto akaonwe na daktari kama ilivyopendekezwa hapa. Binafsi nimehisi huenda ulichokieleza sicho tunachodhani ndicho, kwani kitovu kuvimba na kitovu kutuna inaweza kuwa vitu viwili tofauti. Na je, kitovu kimeshapona kabisa kwamba hakuna dalili ya kidonda?
 
Mie pia nilizaliwa na kitovu kikubwa hali hii ilimchanganya sana mzee ikafika hatua alitaka nifanyiwe upasuaji lakini kwa ushauri mzuri wadaktari kuwa ipo siku kitaisha wazaziwangu walizingatia leo hii hata nikivua shati huwezi amini kama nilikuwa nakitovu kikubwa,hii hali ilininyimaga raha enzi za utotoilikuwa vigumu sana kuvua shati mbele ya wenzangu,kama tulikuwa tunenda kucheza soccer ilinilazimu kuwakipa endapo timu yetu ilitakiwa kuvua mashati..Nakushauri pia vumilia hiyo hali inaisha na hutakuja kuamini kama mtoto alikuwa na kitovu kikubwa
 
Kwa maelezo niliyowahi kusikia na niliyosoma hapa, naamini coin ingesaidia ku-balance pressure ya nje ya kitovu dhidi ya pressure ya ndani wakati ukuta wa tumbo (pale palipo kitovu) ukiendelea kufunga. Hata hivyo, ushauri wa Riwa ni wa kuzingatiwa sana kwani kwa hakika madhara yanaweza kuwa makubwa.

Kuhusu kuzungushia plasta kwenye coin, daktari mmoja wa watoto bado alikataa utaratibu huu japo coin imezungushiwa plasta. Hata hivyo, alitoa njia mbadala akipendekeza kumvisha mtoto kaptula au bukta yenye mkanda mpana utakaofunika kitovu.

Ndugu christmas ni vyema ukampeleka mtoto akaonwe na daktari kama ilivyopendekezwa hapa. Binafsi nimehisi huenda ulichokieleza sicho tunachodhani ndicho, kwani kitovu kuvimba na kitovu kutuna inaweza kuwa vitu viwili tofauti. Na je, kitovu kimeshapona kabisa kwamba hakuna dalili ya kidonda?
mkuu Lazydog kitovu kimetuna na kuhusu kuwapo na kidonda hapana kwani pamekauka na kufunga kabisa
 
Back
Top Bottom