Msaada: Tatizo la binti wa mwaka 1 na miezi 8 kutokwa damu kila mwezi

edward93

JF-Expert Member
Jun 27, 2015
561
1,334
Habari za muda huu wakuu!

Lengo la uzi huu ni kuomba ushauri kwa wadau humu juu ya suala la mtoto ambaye yupo kwenye familia yetu, ni binti wa mwaka mmoja na miezi nane ana tatizo la kutokwa na damu (spot yani kidogo sana) sehemu za siri kila mwezi utokea mara moja au mara mbili na tangu azaliwe imetokea krbu kwa miez minne au mitano sasa!

Jitihada zimefanyika za kumpleka hospitali kadhaa (Rabinsia, Doctor plaza na Muhimbili) na amefanyiwa vipimo vingi sana na vyote vimetoa majibu kuwa hana tatizo lolote!

Na madaktari wanasema hilo hutokea mtoto akiwa na tatizo la hormones imbalance ila uambatana na dalili nyingne nyingi ambazo kwa mtoto huyu hawajaziona kabisa so wanaamini sio tatizo hilo na wameshauri tuendelee kumu-observe!

Najua humu kuna wadau mbalimbali tunaomba msaada wa ushauri au kama kuna mtu amewahi kupata changamoto ya aina hii.

Natanguliza shukrani.
 
Back
Top Bottom