Tatizo la mitaji kwa wajasiriamali Wa kilimo na mifugo

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
MITAJI, MITAJI, MITAJI

WAJASIRIA MALI HABARI?
Moja ya changamoto kubwa inayo kabili wajasiriamali wengi ni mitaji na kama mnavyo jua Benki sio lafiki wa wakulima, yaani ni rafiki kwenye kukuhifadhi pesa zako tu.

NJIA RAHISI NI KUANZISHA SACCOS
Saccos zinaweza kabisa kuwasaidia wakulima na uzuri wa hizi saccosi zinaweza anzishwa kulingana na intrest za watu.
- Wafugaji wanakuwa na Saccos zao
- Wakulima wa mboga na matunda
- Wakulima wa mazao ya muda mrefu

Why hivyo?

Ili hata mkikutana mnaongea lugha moja, yaani mkikutana ligha ni moja.

Hakuna namna ya kutatua mitaji bila kuanzisha saccos.

KENNYA
Wao wako mbali sana kwa sababu ya SACCOS wanaziita SACCO, yaani kuna SACCO mpaka raha na unakuta SACCO ya wafuga kuku wana hado mitambo ya kuprocess kuku zao.

SACCO za wazalisha maziwa wana hadi Mitambo ya kuprocess maziwa.
Wana mitambo ya kutengeneza chakula cha mifugo yao.

SACCO za wakulima wa mboga wana hadi Min supermarket.

Hii ya SACCO kuwa na Supermarket yao ili kukwepa madalali ndo ilinivutia kuliko zote ndo Idea iliyo kuwa bora miongoni mwa SACCO nyingi kule.

SACCO za Daladala kama umefika kule utaona Daladala zao zimeandikwa SACCO yaani kuna SACCOS nyingi Kenya kuliko nchi yoyote ile.

BONGO SASA

Ubinafisi sana, kuona mtu anaweza mwenyewe
Kuwaza kuibiwa
Kuwaza kudhurumiwa
Kuwaza kutapeliwa
Kuwaza mabaya muda wote
Kuwaza kuibiwa

Kwa staili hizi tusahau kutoka tutakuwa tunakuja humu whatsap kuliwazana tu.

INGEKUWA WATU WOTE WANAWAZA KUHUJUMIWA, KUIBIWA, KUTAPELIWA nadhani hata wenye mabasi wangekuwa wanaendesha wenyewe.

Nini kinafanya Mfanyabiashara anamkabidhi dereva Gari la milioni 200 pamoja na mzigo wa Milioni 90 kwamba peleka Mwanza au peleka Kongo. ni kwa sababu anawaza postive anaamini mzigo utafikka salama na likitokea la kutokea ni ajari na kujifunza.

BENKI ZETU

Kwa capita tulizo nazo za kuunga uunga ni vigumu sana kukopesheka benki na hata kama ikitokea basi hayo mashariti na liba zake ni balaaa tupu.

Wanao kopesheka kwa sasa ni wakulima wakubwa sana, Ukisikia benki ya kilimo jua wanakopa wakina Mtibwa sugar, Kagera sugar, Wazungu wanao lima maua na kadhalika au wakina Interchick.

Hao wanaaminika kwa asilimia 100 na kurudisha sio ishu. ni kivipi Mtibwa Sugar ashindwe kurudisha mkopo?

WAKULIMA WADOGO
.Tutaaminikaje ilihari unakuta hata shamba ni la kukodi? leo utalima mwakani hutakuwepo tena.

JIUNGENI ANZISHENI SACCO hakuna namna ya kutoka bila hivyo, Tukiendela na Negative thinking tutasubili sana.


TIME IS VERY LIMITED JAMANI

By Chasha Farming
 
Bravo! Kwangu hii ni mada kutoka kichwani mwa great thinker,anajua tatizo,an,anaeleza athari za tatizo hilo anapendekeza suluhisho.

Kwa watendaji tuungane,kwa walalamikaji hawatafanya chochote Zaidi ya kulalamika.
 
Kweli Kenya wako mbali sana, nilishangaa Nairobi, mombasa kila dala dala imeandikwa,,,,,,,,,,, sacco nikawa sielewi, kumbe watu wame jiongeza ili wafanikiwe kiuchumi.
 
Mimi nimepambana nimejenga banda la kuku nataka kufuga kuku wa nyama natafuta mtaji wa mil 1sijui nitapata wapi
 
wazo zuri sana naunga hoja 100% mimi ni mkulima wa vitunguu nalima Idodoma niko tayari kushirikiana ktk hili
 
fb kuna id inasomeka ofisi ya makamu wa raisi ati wanadai wanakupatia mikopo kwaajili ya kufuga na kulima ukingia inbox wanakupa email ad ya stephen mulokozi kwamba ndo msimamizi wa mradi ambayo kwa bahati mbaya haipatikani nimeshindwa kuelewa ni ya ukweli ama unaa na utapeli
 
Nimeshapiga hesabu hiyo pesa inatosha kama mtaji wa kuku 300 nahudumia na chechi inabaki na faida napata si chini ya laki 8 kwa wiki 8
Kifaranga cha broiler kimoja ni 2000/=×300=600000/=chakula mpaka unawauza??mfuko si chini ya 65 by average..miscellaneous ??? Kamtaji hako ka 1m na faida ya lak 8 .,kila mmoja angefuga mana ni super profit hyooo
 
Kifaranga cha broiler kimoja ni 2000/=×300=600000/=chakula mpaka unawauza??mfuko si chini ya 65 by average..miscellaneous ??? Kamtaji hako ka 1m na faida ya lak 8 .,kila mmoja angefuga mana ni super profit hyooo
Huku nilipo kifaranga ni 1200 chakula wanakula mifuko miwili ya starter ambayo kila mmoja ni 72000,mifuko miwili ya grower ambayo kila mmoja ni tsh 71000 na wanakula mifuko saba au sita ya finisher ambayo ina cost kama laki 3 mpaka 4 kwa hiyo ukijumlisha na madawa hiyo pesa inatosha sana
 
fb kuna id inasomeka ofisi ya makamu wa raisi ati wanadai wanakupatia mikopo kwaajili ya kufuga na kulima ukingia inbox wanakupa email ad ya stephen mulokozi kwamba ndo msimamizi wa mradi ambayo kwa bahati mbaya haipatikani nimeshindwa kuelewa ni ya ukweli ama unaa na utapeli
hao huwa ni matapeli tu hakunaga
 
Back
Top Bottom