Suluhisho la magonjwa ya viungo na mifupa

Mar 4, 2022
43
12
Leo tutazungumzia tatizo linalowapata watu wengi sana pale umri wao unapokuwa umezidi miaka 50 na hasa wale wenye miili mikubwa. Nina uhakika kuwa umewaona akina mama wenye umri mkubwa na miili mikubwa wanavyopata shida kutembea huku wakiinama toka upande mmoja hadi mwingine kila wakipiga hatua au shida wanayopata pale inapowabidi kupanda ngazi au kukuchuchumaa. Maneno kama “ugonjwa wa kuumwa joints, nina tatizo la joints, maumivu ya joints” na maumivu ya mifupa umeyasikia mara nyingi. Tatizo hasa hapa ni nini? Ungana nami katika mada hii uujue ugonjwa huu wa arthritis.



Ugonjwa Wa Arthritis Ni Nini?
Arthritis ni ugonjwa unaotokana na namna yo yote ya hitilafu katika maungio ya mifupa ya binadamu ambao husababisha maumivu na pengine kuvimba katika sehemu moja au zaidi ya maungio hayo. Neno arthritis halilengi ugonjwa mmoja bali jamii ya magonjwa ambayo kwa ujumla yapo zaidi ya 100. Tabia kuu ya magonjwa haya ni maumivu kwenye maungio ya mifupa (joints) ambayo ni endelevu na ambayo hutokea eneo hilo moja.



Chanzo Cha Arthritis Ni Nini?
Kusudi kuelewa chanzo cha ugonjwa huu, hebu kwanza tutazame muundo wa joint au sehemu mifupa miwili inapokutana. Fikiria goti ambapo mifupa miwili mmoja wa paja na mwingine wa mguu vinapokutana:

Ligaments: Ndicho kitu kinachoshikilia mifupa hii miwili pamoja. Hii ni kama utepe wa plastiki au mpira unaonyumbuka uliozunguka eneo hilo kwa nje, ukikunja goti inanyumbuka na ukinyoosha mguu inarudi.

Cartilage: Huu ni utando unafunika eneo ambalo mifupa hugusana ili kuzuia mifupa hii isisuguane moja kwa moja. Utando huu ambao kwa kiswahili tunauita gegedu huyawezesha maungio hayo kufanya kazi kiulaini pasipo kusababisha maumivu.

Capsule: Hiki ni kitu kinachofunika maungio haya kikizunguka pande zote. Ndani ya mfuko huu wa capsule kuna ukano (synovial fluid) ambao huzalishwa na synovial membrane. Ukano ni ute wa kulainisha sehemu hiyo ya maungio na synovial membrane ni utando ulio kwenye kuta za ndani za capsule.



Ugonjwa wa arthritis unasababishwa na hitilafu yo yote katika sehemu hizo za maungio ya mifupa. Inaweza kuwa gegedu inalika, upungufu wa ukano (synovial fluid), maambukizi ya vijidudu katika moja ya maeneo hayo au mchanganyiko wa matatizo.


Aina Za Ugonjwa Wa Joints-Arthritis
Kama nilivyoeleza hapo juu, kuna aina zaidi ya 100 za ugonjwa huu wa joints au arthritis. Katika mada yetu ya leo tutatazama aina kama nne hivi za ugonjwa huu, tukielezea chanzo cha kila aina.

Osteoarthritis: Hii ni aina ya arthritis inayosumbua watu wengi zaidi kuliko aina nyingine zote. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa. Osteoarthritis hutokea pale cartilage inapopoteza uwezo wake wa kubonyea na kuwa ngumu hivyo kuharibika haraka. Cartilage ni kiungo cha kuhimili migandamizo ya ghafla (shock absorber). Cartilage hii inapopoteza ubora wake, tendons na ligaments huvutika na kusababisha maumivu. Hali ya uharibifu huu wa cartilage ikiendelea, mwishowe mifupa huanza kusuguana moja kwa moja na ndipo mgonjwa atakapoanza kupata maumivu makali sana.

Athari za ugonjwa huanza taratibu na kuongezeka na muda. Kutaanza kutokea maumivu kwenye joint baada ya kufanya shuguli fulani au baada ya mapumziko ya muda mrefu. Joints zitakaza, hasa mapema asubuhi unapotaka kuanza shughuli zako za kawaida. Siku zinavyosogea ndivyo utakavyoona ni vigumu zaidi kukitumia kiungo chako. Mara nyingine utaona uvimbe kwenye joint. Osteoarthritis hushambulia zaidi nyonga, mikono, magoti na uti wa mgongo.

Rheumatoid arthritis: Ugonjwa huu hutokea pale mfumo wa kinga ya mwili kwa bahati mbaya kuanza kushambulia viungo vya mwili ikiwa ni pamoja na synovial membrane (synovium) na kusababisha uvimbe na maumivu. Hali hii isipodhibitiwa, huweza kusababisha ulemavu. Ugonjwa huu unaweza pia kushambulia macho, ngozi, mapafu, midomo, damu na mishipa ya damu. Huu ni ugonjwa ambao zaidi

Kwa ushauri na maoni zaidi wasiliana nasi
Magheahealthcare
+255 678 211 747. +255 694 211 747.
IMG-20220218-WA0034.jpg
 
Back
Top Bottom