Farolito
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 15,032
- 35,206
Habari,
Nimekuwa na tabia ya kukumbuka vitu na matukio yaliyopita kuliko kawaida,au kukumbuka vitu ambayo naweza kusema sio vya muhimu sana.
Mfano kuna watu nimesoma nao levels za chini tangu shule za msingi kuna wengine hua nakutana nao nawakumbuka vizuri ila wao ni kama hawanikumbuki labda niwaambie mimi ni fulani ndio akili inamrudia.
Kuna washkaji Kibao hua nawaona mjini najua kabisa huyu ni fulani na ananiangalia lakini hanitambui ila nikimwambia mimi ni fulani tuliokuwa wote shule fulani ndio anapata picha, kuna mmoja alishanikuta duka fulani akanisalimia kabisa ila hakunijua na mimi kwakuwa sikua na muda nikaona nimwache tu, akapiga story na majamaa wa pale akasepa.
Haiishii hapo yaani kuna maneno fulani ya utani tu niliwahi kuambiwa huko utotoni lakini hadi leo nayakumbuka na sio ya mtu mmoja ni watu tofauti, hata matukio mengi tu nayakumbuka ila ukiwasimulia tuliokuwa nao atasema mbona siikumbuki au nakumbuka kuna kitu kama hicho ila details hakumbuki kabisa.
Haiishii hapo hata harufu za vitu ziwe nzuri au mbaya kama niliwahi kukutana nazo sikunyingi hua zinakaa kichwani kiasi nikiisikia tu inayofanana nayo inanirudisha kwenye ile ya mwanzo, mfano niliwahi kuwa na demu miaka kama 15 iliyopita alikuwa anatumia pafyumu fulani inaitwa Chastity ile harufu ilibaki kichwani kiasi hadi lleo hata nikiwa sehemu mfano kanisani au popote nikihisi mtu kapulizia hua nakumbuka vizuri sana, hata harufu mbaya hivyo hivyo zinanikaa hadi leo.
Hii inakuwa nzuri lakini kuna wakati inaniletea shida ya kushindwa kusahau hasa kama niliambiwa maneno ya kukwaza kwenye argument kiasi wewe ulisahahu ila mimi hua nakumbuka hata ukimkumbusha mtu kwamba uliwahi kuniambia hivi atakwambia si kweli au mbona mi sikumbuki kama niliwahi kusema hivyo,sasa hii si nzuri hasa kama sitaamua kupuuzia.
Kuna t-shirt ya bro wangu alinunuliwa tukiwa na miaka kati ya 7-10 ilikuwa na imendikwa maneno Perth, Melbourne, Sydney, Adelaide, Brisbane, Darwin, Hobart Canberra,baadae ndio nilikua kujua ni majimbo ya Australia huko hasa baada ya kufuatilia.
Nikiwa sekondari nilikuwa na t-shirt iliandikwa "I'm the boss and I don't take shit from anyone"
Mwaka 2012 nilikuwa na t-shirt nyeusi imechorwa sura za mademu wawili mmoja sura yake ilifunikwa na mask nyekundu ya love mwingine haikufunikwa chini imeandikwa "But once again I lost my innocence somewhere along the way, Is it a lose or a gain? Still hard to say.
Kuna jamaa niliwahi kupishana nae miaka mingi imepita t-shirt yake nyuma iliandikwa" Do not go where the path may lead instead go where there's no path and leave a trail"
Hata humu JF kama nikitaka kutafuta uzi fulani hua natafuta kupitia member fulani alicomment nini then naingiza yale maneno kwenye search ndio napata uzi husika au naandika kupitia maneno yangu mwenyewe niliyocomment katika uzi ule ndio na search.
Kuna uzi humu JF nilianzisha wa kuwakumbusha watu fulani ambao kwenye majukwaa mbalimbali hutoa ahadi kwamba "Kuna siku nitaleta uzi kuhusu jambo fulani" Hawa wote nilikua nawakumbuka walitoa ahadi kuhusu kitu gani na kwenye uzi gani ila bahati mbaya hata baada ya kuanzisha uzi ule na kuwaita hawakuwahi kuleta hizo nyuzi zao, sasa sijui ilikua fix au vipi😀
Kwenye maisha ya kawaida inanisaidia sana kukumbuka watu, matukio, hadithi nk,kukumbuka nyimbo mbalimbali mfano hata nisipokuwa na kitabu cha nyimbo kanisani hua nakwama kuimba nyimbo chache sana tena ambazo sio maarufu.
Wakati nikiwa Sekondari nilikuwa napenda sana Rnb na wakati ule tulikua tunandika lyrics so yale maneno hadi leo ukipiga wimbo nayakumbuka mwanzo mwisho, nyimbo nyingi tu mfano.
✅Show me the Meaning-Backstreet Boys
✅More than that-Backstreet
✅Soledad-Westlife
✅La Isla Bonita-Madonna
✅Sacrifice-Elton John
✅Ain't it funny-JLo
✅Nothing at all-Santana
✅Forever more-Puff Johnson
✅I still believe-Mariah Carey
nk
Kuna zile simu za Nokia za zamani(Nokia 1112) ilikua na muito fulani sauti ya kike inaimba "Do you hear me when I say, I waiting, can you answer my call.... ni vitu hua nakumbuka halafu havitoki kichwani kirahisi.
Hata humu JF hua nafuatilia watu wanacomment nini na ndio hua zinanisaidia nikitaka kutafuta uzi na zinanisaidia kuwajua vizuri hata kama sichangii humo nasoma tu
Je kuna mtu inamkuta hali hii? Unafanyaje kusahau hasa yale yasiyo muhimu au ya kukwaza
Ahsante.