Tatizo la kula/kutafuna kucha

Kuna jamaa yangu alikuwa anakula kucha mpaka vidole vikawa kama vya sokwe mtu.
 
Mkuu kwa nilipofikia sasa cjui kama nitaweza tena kuacha.. Nimeshakua teja kabisaaa.. Naweza nikajikana asubuhi mpaka mchana ila ikifika jioni kama kawa... Aisee nataman sana kuacha.. Ila nikikosa kazi ya kufanya tu hata kama nipo ofisini au niliwa na kazi ngumu sana...
 
Ukiwa kazini zipake kitunguu saumu ukiwa nyumbani zipake mafuta taa jaribu hii usikate tamaa
 
Sorry una umri gani? na tatizo lina muda gani?
Binti yangu alikuwa na kuchagua nzuri sana, zimeharibika sababu ya kuziuma, nilishaongea hadi nimechoka. Je akifanikiwa kuacha kuzing'ata zitarudi kuwa nzuri?
 
Yaani mimi nimeona huu uzi nimefurahi sana,nakula kucha mpaka najisikia vibaya mimi mwenyewe!Kwetu tumezaliwa watatu na wote tunakula kucha ile mbaya na nakumbuka pia kumwona baba yangu akila kucha sasa huwa na waza tuliiga au tuliridhi kutoka kwake.Kuna saa huwa ni tamu mpaka nakimbia kukaa mahali peke yangu mtu asinione halafu nakula kwa raha zangu na enjoy sana.Nikiwa mja mzito nakula mpaka natoka damu.Jamani hii kitu nikiweza kuacha nitafurahi sana yaani mpaka kucha zimepinda na kuwa nyeusi.Mume wangu amepambana na mimi mpaka amesanyoosha mikono.Mshana jr asante sana kwa hili somo nitaanza sasa kuacha na nitawapa mrejesho kabla na baada!
 
Du! I see kuna rafiki yangu anatafuna kucha hadi namuonea huruma. Hata yeye anasema huwa hakumbuki chochote wakati anapozitafuna na ameishajizuia kuacha hiyo tabia bila mafanikio. Afanyeje?
 
mimi nimeathirika kweli kweli,mpaka leo,zikikuwa tu,uwa sina mpango wa kutafuta kiwembe,mwendo wa meno tu,kuna wakati nilikuwa nakula kucha,zikiwa fupi,nakula na ile ngozi ya ncha za kucha,kazi ilikuwa kwenye kula ugali wa moto,nilikuwa NAKOMA
 
Mimi tatizo langu ni kula kizibo cha kalam(pen)yaani siwezi kukaa na pen bila kuitafuna kizibo,kiasi kwamba ofisi nzima wanajua pen zangu.nimejizuia nimeshindwa.mradi hainidhuru nimeona niache hali kama ilivyo.
 
Mshana jr, vipi unatoa tiba mkuu, kuna dogo langu yani huwa nampiga mingumi ila hasikii, huyu ni mgonjwa type gani chronic ama?
Kupiga siyo dawa,dawa ni kumuelewesha kuwa kula kucha ni uchafu kila unapomuona anakula kucha.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…