Tatizo la kukosa hamu ya kula kwa mtoto mdogo miaka 8

massawe7

Member
Oct 28, 2011
10
1
wakuu ukweli mtoto wangu mwenye umri wa miaka 8 ana tatizo kubwa la kuto kula na hii inatusumbua sana sisi wazazi wake wakuu naomba ushauri ama mwenye kujua tiba atujuze.nawasilisha
 
nenda umnunulie dawa ya kuongeza hamu ya kula.atakula hadi atakwambia niongezee
 
wakuu ukweli mtoto wangu mwenye umri wa miaka 8 ana tatizo kubwa la kuto kula na hii inatusumbua sana sisi wazazi wake wakuu naomba ushauri ama mwenye kujua tiba atujuze.nawasilisha

Pole sana sijaelewa tatizo hili analo kwa muda gani au tangu kuzaliwa.Hata hivyo mtoto kutokula vizuri au kukosa hamu ya kula maana huwezi kusema huwa hali kabisa maana asingekuwa hai,inaweza kuwa ni dalili ya kuwa na tatizo kiafya kama ugonjwa,pia mtoto anapokuwa na mawazo sana hamu ya kula yaweza potea.Hivyo ni vema kucheck hospital kama kuna tatizo la kiafya.

Hata hivyo unaweza jaribu tumia mbinu hizi kumfanya atamani kula/kula.
1.Mwambie acheze michezo kama kuruka,kukimbia nk. ina speed up digestion automatically atataka tu kula baaada ya mazoezi.
2.Usimpe chakula kilekile kila siku jaribu kumbadillishia vyakula au kumuuuliza anapenda apikiwe nini.
3.Mpe chakula kidogo kuliko kumpa kingi kwa wakati mmoja.
4.Kama anapenda kulamba vitu vitamu au kunywa kama juice tamu sana mpunguzie badala yake mpatie matunda kama machungwa.
5.Jaribu kuongea naye huenda ana mawazo fulani yanamsumbua maana watoto wengine husimangiwa vyakula japo sisemi wa kwako nao huamua kuacha kula,au wanapofokewa mara kwa mara au kuambiwa wao wanakula sana.
4.Mpangie ratiba fixed ya kula let say mara nne kwa siku utakuwa umemwandaa kisaikolojia kwa ajili ya kula saa hiyo ikifika.
5.Nisinge shauri kutumia vidonge vya kuongeza hamu ya kula kwani vile havimalizi tatizo na vinafanya kazi kwa saa fulani nguvu yake ikiisha tatizo lina baki palepale kumbuka dawa zote zina side effects zake si vizuri kumweka mtoto kuwa at risks ya matatizo mengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom