Tatizo la kizunguzungu yapata mwezi mmoja

RoadLofa

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
1,347
2,957
Wakuu Nina tatizo la kizunguzungu / dizness na kuona maluweluwe yapata mwezi mmoja sasa nimeenda dispensary naona miyeyusho tu daktari kanipima tu pressure basi kasema ipo sawa ila nikajiongeza mwenyewe nikamwambia acheck damu na maji akadai atanicheck mpaka jumatano- week ijayo

kama mnavyojua izi dispensary za bush ni miyeyusho yaani naumwa naambiwa kupimwa mpaka next week na sijaambiwa Kwa sababu gani nikajiondokea zangu,ila nimepanga kufunga safari kwenda hospital ya wilaya maana kizunguzungu muda wote yapata mwezi mmoja na zaidi na nachoka balaa bila sababu maalumu
 
KIZUNGUZUNGU NI DALILI MBAYA​

Tofauti na watu wengi
wanavyodhani, kizunguzungu huwa ni ishara ya tahadhari inayotolewa na mwili kuwa kuna kitu hakiko sawa, hivyo uchunguzi wa chanzo cha tatizo unapaswa kufanywa haraka.

Kwa mujibu wa utafiti wa kitabibu, kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha kizunguzungu, ikiwemo ukosefu wa usingizi (insomnia), kuumwa kichwa, kuchomwa na jua kwa muda mrefu, upungufu wa sukari mwilini na upungufu wa damu au maji.

Kwa kawaida,
tatizo la kizunguzungu unaweza kulidhibiti mwenyewe kwa kutumia tiba mbadala ya kutengeneza mwenyewe nyumbani na kama tatizo litakuwa sugu, basi unashauriwa kumuona daktari mapema zaidi kabla hali hajawa mbaya zaidi.

Kuna tiba nyingi
za nyumbani unazoweza kutumia kujitibu kizunguzungu, ya kwanza ni maji iwapo kizunguzungu kitatokana na kupungukiwa na maji mwilini, hivyo hatua ya kwanza ni kunywa kiasi cha lita moja au nusu ya maji yaliyochanganywa na asali au limau, maji haya yatatibu upungufu wa maji mwilini na kurejesha virutubisho vilivyopotea kutokana na joto kali.

Kizunguzungu kilichosababishwa na ukosefu wa usinginzi, kinahitaji kushugulikiwa na mtaalamu wa masuala ya usingizi au kutibiwa hospitali, ni vizuri kuwasiliana na daktari mara moja kuhusu tatizo hilo.

Watu wanaosumbuliwa
na shinikizo la juu la damu (high blood pressure) huwa hawasumbuliwi na kizunguzungu kwa muda mrefu. Kwa watu wenye tatizo la presha, huwa na dalili zingine kama vile kusikia uchovu, kichefuchefu, kupoteza fahamu na dalili nyingine. Iwapo dalili hizi zitaenda pamoja na kizunguzungu, mgonjwa anashauriwa kuonana na daktari kwa ushauri zaidi.

Kwa wale wanaopatwa
na kizunguzungu kutokana kuwa na wasiwasi, kizunguzungu huja pale wanapokuwa katika hali fulani ya mchanganyiko wa mawazo juu ya jambo fulani, wakiwa katika hali hiyo, dawa pekee ni kujipumzisha na kuacha kuwaza kwa muda. Wanaweza kujipumzisha kwa kufanya mazoezi ya kuvuta na kushusha pumzi.

Upungufu wa damu mwilini (Anaemia),
nao husababisha kizunguzungu wakati mwingine, hali hii hutokana na mwili kukosa hewa ya oksijeni ya kutosha. Kula vidonge vyenye madini ya chuma na ulaji wa mboga za kijani, maziwa, siagi na jibini husaidia kuondoa tatizo la kizunguzungu.

Si kawaida mtu kusikia kizunguzungu
kila mara, ukiwa katika hali hii ujue una tatizo ambalo unashauriwa kulifikisha kwa daktari kwa uchunguzi zaidi. Vile vile unashauriwa kufuatilia dalili nyingine unazoziona wakati unapopatwa na kizunguzungu.

Kwa ujumla, kusikia kizunguzungu
mara moja moja baada ya muda mrefu, sio dalili mbaya, hasa kama kizunguzungu chako unakipata baada ya kufanya jambo fulani, kama vile kukaa sana juani au kwenye joto kali ambalo husababisha mwili kukaukiwa na maji, matokea yake huwa ni kusikia kizunguzungu.

Katika hali kama hii,
siku zote kimbilia kunywa maji yaliyochanganywa kidogo na limau pamoja na asali ambayo hurejesha maji na virutubisho vilivyopotea mwilini kutokana na joto kali.

Mwisho,
ni jambo zuri mtu kujenga tabia ya kuchunguza mwenendo wa mwili na kuchukua hatua za haraka za kudhibiti dalili zisizo za kawaida mwilini ili kujiepusha na maradhi hatari yanayoweza kuwa yanajijenga mwilini.
Ukitaka Tiba yake nione mimi kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole.
 
Wakuu Nina tatizo la kizunguzungu / dizness na kuona maluweluwe yapata mwezi mmoja sasa nimeenda dispensary naona miyeyusho tu daktari kanipima tu pressure basi kasema ipo sawa ila nikajiongeza mwenyewe nikamwambia acheck damu na maji akadai atanicheck mpaka jumatano- week ijayo

kama mnavyojua izi dispensary za bush ni miyeyusho yaani naumwa naambiwa kupimwa mpaka next week na sijaambiwa Kwa sababu gani nikajiondokea zangu,ila nimepanga kufunga safari kwenda hospital ya wilaya maana kizunguzungu muda wote yapata mwezi mmoja na zaidi na nachoka balaa bila sababu maalumu
Kizunguzungu ni dalili ya mwili kutokuwa sawa.

Ili kuelewa hili, ni muhimu kufahamu ni nini hasa mtu anajisikia:

1: Kukosa nguvu na kutaka kuanguka.

2: Kuona vitu (mazingira) vinazunguka/kumzunguka mtu.

Historia nzuri ya hayo(1&2) hapo juu hutakiwa kuchukuliwa vyema ikihusisha nini kinaanzisha, kuzidisha au kuleta nafuu na kupata vipimo vya kwanza vya mwili/vital signs.

Ukaguzi wa mwili/physical examination, husaidia kuongeza ushahidi au kupunguza aina ya matatizo yanayodhaniwa.

Wakati unamwona mgonjwa wa kizunguzungu vifuatavyo ni baadhi ya bisababishi fikiliwa kulinhana na mgonjwa wako:
[ ] Kushuka presha
[ ] Kupanda presha
[ ] Stress
[ ] Wasiwasi
[ ] Sukari kushuka
[ ] Sukari kupanda
[ ] Joto kali
[ ] Damu kushuka/chini ya kiwango kinachotakiwa
[ ] Tatizo la mishipa ya fahamu au ubongo
[ ] Tatizo la masikio
[ ] Tatizo la sinusi
[ ] Tatizo la macho
[ ] Tatizo la moyo
[ ] Baadhi ya dawa
[ ] Matumizi ya pombe

NB: Ni vyema kupita kwenye hatua hizi kwa kushikiana vyema na mtaalamu wa afya. Pia ni vyema kuchukua tahadhali unapopata kizunguzungu unapokuwa unaendelea na maisha kwa kupata sehemu salama na kupumzika badala ya kulazimisha kwenda mbali, ambapo unaweza kuanguka na kuumia vibaya. Pia kuwa makini wakati wa kusimama kwa kwenda kwa hatua/chunguza kabla ya kusimama kama uko sawa ili kuepusha kuanguka.
 
Wakuu Nina tatizo la kizunguzungu / dizness na kuona maluweluwe yapata mwezi mmoja sasa nimeenda dispensary naona miyeyusho tu daktari kanipima tu pressure basi kasema ipo sawa ila nikajiongeza mwenyewe nikamwambia acheck damu na maji akadai atanicheck mpaka jumatano- week ijayo

kama mnavyojua izi dispensary za bush ni miyeyusho yaani naumwa naambiwa kupimwa mpaka next week na sijaambiwa Kwa sababu gani nikajiondokea zangu,ila nimepanga kufunga safari kwenda hospital ya wilaya maana kizunguzungu muda wote yapata mwezi mmoja na zaidi na nachoka balaa bila sababu maalumu
Ukipata muda pima pia H-Pyroli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom