Tatizo la Galaxy s5 kukwama kwama, naomba msaada

Howt Lady

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
1,519
470
Habarini wapendwa.

Natumia Samsung Galaxy s5 original yenye warranty ya two year's niliinunulia pale posta makao makuu ya Samsung J M Mall

Sasa tangu jana simu inastuck mara kwa mara.. mfano nikifungua Gallery au INSTAGRAM AU WHATSAPP YAAN APP YOYOTE ILE inajifungua taratibu mno tofaut na mwanzo then inaweka black screen.

Halafu inaandika GALLERY HAS STOPPED DO U WANT TO WAIT OR TO REPORT? Then ukibonyeza wait itakaa mpaka dakika mbili ndo ifunguke au iweke black screen then ijizime kabisa

Na mda mwingine haijizimi lakn inastuck na kuwa black screen hapo ata ufanyeje haikupi notification yoyote kama imejizima au la nikaicha badae nikapata wazo la kuifungua kutoa battery na kuliweka tena ndo ikawaka

sasa kila napogusa app yoyote ile tangu jana inakua ivo ivo je nifanyeje? nini tatizo jaman? Au niirudishe pale pale?? Na je nikiirudisha watanipa nyengine au?

Nipeni mawazo tafadhali.
 
Jaman msiwe kimya nipeni mawazo tafadhali maana nimekwazika sana na sijawahi kuidondosha wala kuingia maji simu bado mpyaaa kabisa na naipenda.
 
Jaman msiwe kimya nipeni mawazo tafadhali maana nimekwazika sana na sijawahi kuidondosha wala kuingia maji simu bado mpyaaa kabisa na naipenda

Ebu jaribu kurestore kwa kufanya hard rest..ila kila application itapotea na sms etc
 
Yap warudishie,

Kama lilianza taratibu huwenda ni wewe mwenyewe tu umeeka vitu vingi ila kama limeanza ghafla tu itakuwa ni hardware ndani possibly memory zimeanza kufa.
 
yap warudishie, kama lilianza taratibu huwenda ni wewe mwenyewe tu umeeka vitu vingi ila kama limeanza ghafla tu itakuwa ni hardware ndani possibly memory zimeanza kufa.

Nami natumia s4 mkuu inatatizo ili na kweli ina vitu vingi mno kwaiyo solution ni kuvifuta au? ?
 
yap warudishie, kama lilianza taratibu huwenda ni wewe mwenyewe tu umeeka vitu vingi ila kama limeanza ghafla tu itakuwa ni hardware ndani possibly memory zimeanza kufa.

Ahsante mkuu kwa MAWAZO yako mazur maana nilikua nataka KUKUPM ila nashukuru umechangia nashindwa kuelewa memory zimeanza kufa mapema ivo? simu bado mpya kabisa na kuhusu vitu vingi nikweli ina vitu vingi lakn na uwezo wa simu ni mkubwa

Kwaiyo kesho naweza kuwarejeshea au nisubiri mpaka j3? Na hapo uliposema kwenye hardware je ni nn yaweza kua ni tatizo? Samahan kwa usumbufu.
 
yaan wamaanisha nifute kila kitu au? Samahan nifafanulie kidogo

Ndio hii njia hufuta kila kitu...na jinsi ya kufanya ni; Zima simu fanya hivi wakati wa kuwasha: Bonyeza home botton,volume down key na power bottun kwa pamoja...shikilia kwa mda kidogo hadi itokee menu ya kurestore...

ikiwa itatokea tumia button za volume ku highlight options..sasa hapo highlight option ya "wipe everythin" then kuselect bonyeza power button.

Hapo itafuta vitu vyote na itawaka kama mpya!
 
MALISA92,

Sijui ntaweza mkuu ngoja nifanye ivo alafu ntakupatia jibu.

Ahsante sana kwa mawazo yako mazuri
 
Last edited by a moderator:
nami natumia s4 mkuu inatatizo ili na kweli ina vitu vingi mno kwaiyo solution ni kuvifuta au?
Yap ukiwa na apps nyingi simu inakuwa slow sababu apps nyingi za simu huwezi kuzifunga. bonyeza home button kwa kuishikilia halafu bonyeza kiduara cheupe kwa pembeni utaingia kwenye task manager then utaona ram unayotumia na ambayo ipo free, app zilizo open nk.

Pia ku update kwenda latest software kutasaidia kuifanya simu yako ifanye vizuri zaidi. Kitkat Samsung walifree ram kubwa.
 
ahsante mkuu kwa MAWAZO yako mazur maana nilikua nataka KUKUPM ila nashukuru umechangia nashindwa kuelewa memory zimeanza kufa mapema ivo? simu bado mpya kabisa na kuhusu vitu vingi nikweli ina vitu vingi lakn na uwezo wa simu ni mkubwa

Kwaiyo kesho naweza kuwarejeshea au nisubiri mpaka j3? Na hapo uliposema kwenye hardware je ni nn yaweza kua ni tatizo? Samahan kwa usumbuf

Tatizo linaweza kuwa jengine mimi naguess tu. ukienda ofisi zao ndio watakupa jibu sahihi maana wao wanakuwa na tools zenye uhakika.

Simu ikiwa slow ghafla na app hazirespond au kustack kwa muda mara nyingi ni tatizo la memory aka internal memory yako ambapo hizo apps zimehifadhiwa.

Ila kama ilikuwa inaanza taratibu kila siku simu inazidi kuwa slow huenda tu ikawa ni software issue ukireset ikakubali.
 
yap warudishie, kama lilianza taratibu huwenda ni wewe mwenyewe tu umeeka vitu vingi ila kama limeanza ghafla tu itakuwa ni hardware ndani possibly memory zimeanza kufa.
Eti hiyo ndo flagship ya mwaka jana ya samsung. Samsung ni majanga. Watu wanatumia flagship za apple za mwaka 2012 na hawajapata matatizo hadi leo
 
Eti hiyo ndo flagship ya mwaka jana ya samsung. Samsung ni majanga.

Watu wanatumia flagship za apple za mwaka 2012 na hawajapata matatizo hadi leo

Hakuna simu ambayo hazina matatizo, ukumbuke hizi simu zinatengenezwa hadi unit milion 50 na zinatengenezwa na technology ya wanadamu hivyo tegemea maelfu kama sio malaki ya simu kuwa na vifaa ambavyo ni defective.

Ingekuwa zinatengenezwa na malaika hapo sawa.

Even iphone zipo defective kibao nenda forums za apple/site zao utaona malalamiko.

Cha muhimu ni warranty ikizingua wakuekee sawa au wakupe nyengine bila kukupotezea data zako.
 
Ndugu yangu fanya kama ulivyoelekezwa na mkuu Chief-Mkwawa namuaminia sana kwenye hili jukwaa la technology kama huez kufanya ivyo basi iache iyo simu kama ilivyo wala usiipeleke kwa fundi irudishe pale pale Samsung Mobile posta hapo Makao makuu ulipoinunulia fika pale nadhani j3 ndio itakua siku nzuri japo kila siku wanafungua.

Ukishafika waeleze tatizo la ilo simu wataikagua then watairekebisha au watakupatia simu nyingine kama iyo Mpya usiwaze wala usiwe na shaka hawana shida kikubwa usiipeleke kwa fundi yoyote yule.

Nb: ikiwezekana beba na risiti pamoja na box la simu ingawa sio lazma.
 
MALISA92,

Ahsante sana mkuu nimefanikisha na inafanya kazi kama kawaida nimefuta yote ambayo hayakua na umuhimu na haistuck tena

Ubarikiwe mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom