Tatizo gani linafanya simu kuchemka?

Tatizo gani linafanya simu kuchemka?

Check labda Cylinder head imepata ufaa, or rejector itakuwa kuna sehemu inavuja uzibe, au rejetor fan itakuwa haifanyi kazi or check fan belt inaweza iko lose
Kama kuchekeshwa tushachekeshwa na wnzako hizi sasa ni sifa dada
 
Pole sana hiyo ina mAh ngapi? Huenda ni battery ndogo jaribu kuhamia iPhone mkuu
 
Simu kuchemka inategemea na matumizi, unakuta inafanya kazi nying kwa mpigo huku hakuna feni inayoweza kuipoza ndio maana inakuwa inachemka, dats y pc zina feni kwa ajili ya kuzifanya zifanye kazi kwa mda mrefu bila kuchemka
 
Wakuu naomba mnisaidie simu yangu ina tatizo la kuchemka kila nifunguapo data ,nimejaribu kurestore simu zaidi ya mara tatu ili niondokane na hili tatizo la kuchemka kwa simu yangu lkn naona bado iko vile vile mpaka ss inachemka ,pia betri lake ni unremovable ,nimejitaidi kuondoa app zisizo za msingi katika simu yangu lkn bado ipo vile vile ,nimejaribu kuweka cool master inasaidie lkn bado ,ndo nimeona nije kwenu najua humu kuna wataalam watanisaidia .SIMU YANGU TECNO W4 WALA HAIJAWAHI ANGUKA CHINI NA SIJAWAHI KUICHAJI IKIWA NA MOTO MM HUWA NAIACHA INAISHIWA CHAJI NDO NAWEKA,ILA NISIPOFUNGUA DATA HAICHEMKI .
Pole ndugu! Naomba utumie hii code *#*#4636#*#* ingia kwenye Phone information, shuka chini hadi kwenye "Set Preferred Network Type" Chagua WCDMA preferred kama eneo ulilopo lina coverage nzuri ya 3G utapata speed nzuri bila kui-force simu kwa kutumia WCDMA Only.
Pili jaribu kutafuta betri mpya, punguza idadi ya Apps zilipo kwenye simu haswa Security apps kama Avast kwa sababu ya udhaifu wa specs za simu yako.
 
Pole kwa hilo janga, lakini Fanya kama ambavyo wengi wamejaribu kukuelekeza,
1) badili betri
2) punguza apps kama antvirus, cleaner, boost, games nk
3) SD card ya ujazo mkubwa na kuijaza mazagazaga
4) hizi simu zetu hiz..! Dah! Ni shida, DAR nyuzi joto 30.c UWEZO simu mdogo, imeundwa kwa bati na plastic, halafu ukavika cover la mpira, ukapakua apps kibao mapaka ambazo hukumbuki uliitumia lini Mara ya mwisho,, halafu unawasha data kitakachotokea hapo ni janga
 
Hilo ni tatizo la ac power android ambayo inazidiwa uwezo na apps so ipeleke kwenye ofisi za tecno popote Tanzania watakurekebishia bure coz simu za tecno zina warranty ya 1year
 
Wakuu naomba mnisaidie simu yangu ina tatizo la kuchemka kila nifunguapo data ,nimejaribu kurestore simu zaidi ya mara tatu ili niondokane na hili tatizo la kuchemka kwa simu yangu lkn naona bado iko vile vile mpaka ss inachemka ,pia betri lake ni unremovable ,nimejitaidi kuondoa app zisizo za msingi katika simu yangu lkn bado ipo vile vile ,nimejaribu kuweka cool master inasaidie lkn bado ,ndo nimeona nije kwenu najua humu kuna wataalam watanisaidia .SIMU YANGU TECNO W4 WALA HAIJAWAHI ANGUKA CHINI NA SIJAWAHI KUICHAJI IKIWA NA MOTO MM HUWA NAIACHA INAISHIWA CHAJI NDO NAWEKA,ILA NISIPOFUNGUA DATA HAICHEMKI .


Kupata joto kwa simu inaweza kuwa sio tatizo , cha muhimu jaribu kuchunguza kama hilo joto sio la kawaida. Tecno W4 ni moja kati ya simu nzuri za tecno zilizotoka mwaka jana. Hizo simu zimekuja na MashMallow. Sasa pengine sababu ya kupata joto inaweza kuwa hii: simu hiyo ukiReboot (ukizima na kuwasha) huwa Apps zilizokuwa zinaRun zinaendelea kuRun. Yaani kama ulikuwa umefungua Gallery, Email, calculator,Game, facebook halafu UkareBoot basi hizo Appd zote zinaeudi kama zilivyokuwepo hivyo RAM bado inakuwa na Mzigo mkubwa. Sasa jaribu kufunga Apps zote au zile Apps ambazo huzitumii kwa muda huo. Pia funga Apps zote kabla ya kuzima na kuwasha simu. Kufunga Apps zote BONYEZA LEFT BUTTON wakati upo Home, halafu bonyeza hiyo Alama ya BRUSH .
 
kama ume restore bado inapata joto solution nyingi unazofanya hazitasaidia sababu unaporestore simu inaanza upya unakuwa huna vitu vingi ilitakiwa isipate joto, hapo kuna mambo kama matatu

1. ni bloatware zinazokuja na Tecno
2. Simu yako ina malware (virusi)
3. Ni Tatizo la hardware.

cha kufanya
1. install app ya cpu z toka playstore halafu nenda upande wa thermal itakuonyesha joto la simu yako na eneo gani hilo joto linatokea.

LF5uCPtvowgKzQBqqodghxqGjXnqKkoNJtJW2fikqSM.jpg


2. angalia app gani ipo background mda wote na kutumia cpu/gpu hadi kusababisha simu ipate joto

nenda playstore search app inaitwa os monitor halafu simu ikipata joto ifungue itakwambia ni app gani inatumia sana cpu wakati huo.

pia jaribu njia hii
-nenda setting halafu security halafu device administrator hakikisha hakuna app usioijua. mara nyingi kunatakiwa kuwe na device manager tu.
 
Kama hamna majibu si mkae kimya waje wenye akili wampe majibu.
Ndg yangu haya ndiyo mawazo ya wengi humu, huwa nayadoma mpaka njiuliza hili taifa ndiyo maana hatusongi mbele kazi kukatishana tamaa tu, kwani tecno siyo simu? Na je! Jibu alilolihitaji ndio haya yanayotolewa! Mungu tusaidie kubadirisha mawazo mgando ya maadhi wa watanzania.
 
Back
Top Bottom