Habari wakuu samahani na poleni na mihangaiko ya kila siku, naomba ushauri.
Nilipata placement utumishi Mwezi wa tisa baada ya kureport kwenye taasisi husika wakaniambia nitapigiwa simu ila mapokezi katika taasisi hiyo ayakuwa mazuri maana walikataa ata kuchukua barua kutoka utumishi nikaambiwa nitapigiwa simu.
Mpaka leo kimya lakini wenzangu walio enda taasisi zingine wameshaanza kazi.
Mimi nipo tu, sina cha kufanya maana kila kitu kwenye maisha yangu kimesimama naomba ushauri juu ya jambo hili
Nichukue hatua zipi.